Tuanze kufikiri kufundisha lugha ya kichina mashuleni

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,904
Ukiachana na ukweli kwamba china amekua mdau mkubwa wa maendeleo toka taifa letu limepata uhuru, ni taifa ambalo uchumi wake umekua ukikua kwa kasi kubwa na kutishia hata uchumi wa marekani taifa tajiri kabisa.

China ina watu zaidi ya bilioni moja ambayo ni sehemu kubwa tu ya wakazi wa dunia wanaofikia bilioni saba.

Ukubwa wa uchimi wake na wingi wa watu ni kishiria tosha cha uhakika sa soko kama tukiamua kufanya nao biashara seriously.

Tukiwa karibu na hawa watu kuna uhakika wa soko la watu wasiopungua bilioni moja mbili kasoro. Ni mtaji mzuri kibiashara.

Kwakua china inakaribia kuwa taifa lenye nguvu kabisa za kiuchumi na wakati zama za magharibi zikianza kufikia ukingoni ni vyema kuanza kujianda jinsi ya kushirikiana nao ili tusiwe nje ya muda.

Ingawa, dola na lugha ya kimagharibi bado vimebaki kama bidhaa zenye soko duniani sio vibaya kuongeza ubora wa kizazi chetu kua na uwezo wa kufahamu lugha mbali mbali.

Itakua faida ya ziada , katika ajira na pia katika biashara, hatutategemea wakalimani tena ili kuweza kufanya nao mawasiliano.

Ingawa wapo watakaosema kujifunza lugha za wengine ni kuonesha udhaifu na kukaribisha ukoloni, kwangu mimi naona kama ni faida zaidi kuliko hasara.

Wizara husika ingeweka namna ya kuweka utaratibu wa watoto mashuleni kuanza kujifunza lugha hiyo kidogo kidogo ile baadae huko mbeleni wanaweza kulisoma kama somo la ziada.

Kua na taifa la watu competent ni faida kubwa kiusalama na kiuchumi pia.
 
Back
Top Bottom