Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 407
- 1,054
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kutokana na kuenea kwa elimu ya fedha, kwa sasa Watanzania wengi wamehamasika kuwekeza kwenye soko la hisa la Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).
Cha kusikitisha ni kuwa wawekezaji wanakwama kwa stockbrokers ambao ndio wanahusika kumnunulia au kumuuzia hisa mwekezaji. Kwa sasa mitandaoni kuna malalamiko mbalimbali kuhusu madalali hao kuwa na huduma mbovu, kutojibu malalamiko ya wateja n.k.
Kwenye soko la hisa, muda ni zaidi ya mali. Dalali akikuchelewesha hata siku moja tu tayari ni hasara kubwa kwa sababu bei ya hisa inabadilika kila siku, na kwa soko la hisa la Dar es Salaam bei ya hisa ni kama inapaa kadri siku zinavyozidi kwenda.
Hivyo basi, tupeane uzoefu: dalali gani ana huduma nzuri na yupi ana huduma mbaya. Ili wawekezaji wanaosumbuka na madalali wabaya wawahame, kwa sababu inakera sana.
Mi naanza na dalali wangu msumbufu anaitwa Orbit Securities Co Ltd. Simu hawapokei, meseji hawajibu; yaani ni kama vile mimi ninawalazimisha wanihudumie, tena wanihudumie bure.
Mwanzo hawakuwa hivi, lakini kwa sasa huu usumbufu umenifika kooni, lazima nihame.
Karibuni tusaidiane.