Tuacheni udhalilishaji, imetosha sasa


Mkuu umesema ukweli kabisa tabia hii ni bora watu wa pande zote mbili tungezingatia utu
kwanza.iwe ccm au upinzani, tungethaminiana. Tumezidi mipaka sana!

Lakini mkuu naona umesema vijana wa CCM ndo wanatukana, mimi katika hilo siwezi kusema ni kweli au hapana. Kwa mtazamo wangu naona wanao ongoza na kufundisha kutukana ni Mkurugenzi wa TCRA na wafanyakazi wake kwa kushindwa kukemea kashfa hizo au kuzichukulia hatua.

Sasa kama upinzani wanatukana na hata ccm wanatukana na kusambaza picha za kashfa mfano kama picha tajwa hapo juu, TCRA haitakiwi kulifumbia macho kamwe kwasababu ndo wame anzisha sheria za mtandaoni.


Katika maelekezo ya mwanzo ya TCRA, walisema mtu ukitoa taharifa ya kudharirisha, au uongo, au picha kutuma na kupokea picha za kudharirisha, muhusika atakuwa amevunja sheria na pia na faini za sheria hizo walizitaja.


Katika hali ya kusikitisha ten asana, huyu mkurugenzi wa TCRA na watu wake, wamekuwa wakifumbia macho Video za kashifa zinasambaa hovyo na ku-dharirisha au kushusha utu wa mtu. Lakini akisemwa kiongozi tu wa selikari, utasikia wanajitokeza kuwa mtu kakamatwa!!!


Nachukua hatua hii kukuaonya wewe mkurugenzi wa TCRA
, Tafadhari simamia sheria hii kwa ku-balance na kutenda haki. Siyo watu humu kipindi hiki wanadharirishwa sana, mtu anaibua kashfa za aibu anatuma na nyie mko kimia, mnasubiria asemwe Mkuu wa majeshi ndo tunakuja kuwaona kwenye TV. Picha tajwa ya huyu mwanamke kiukweli ni udharirishaji kabisa, TCRA haikutakiwa kuifumbia macho hata kwa kumuonya muhusika.



JESHI LA POLICE
Mchungaji Gwajima, akiwa kanisani kwakwe, alisema maneno juu ya Askofu wa kanisa katoliki, ambayo maneno hayo, mimi siwezi kusema alikosea au hakukosea , ila nyie Jeshi la police mlitafisili amekosea na mim si walahum kwa hilo na hivyo kumkamata na kumhoji. Wakati huo huo Askofu wa kanisa katoliki yeye alitoa msamaha akamuachia Mungu nyie police mkakomaa, Gwajima. Gwajima mkidai ametukana!!


Sasa niwahulize nyie police
, Je maneno aliyo yasema Bwn Mwigulu Nchemba kule tarime kuhusu Lowassa, maneno makali, matusi ya aibu tena ya nguoni, mbona mme kaa kimia?


Kiukweli na nyie mnachangia kupotosha na kuharibu mahadili ya nchi yetu kwa ku-tobalance kazi zenu. Naomba niwakumbushe. Tafadhari tendeni haki msije mkafikili siku ya kihama haipo. Hipo vizuri na Kila mtu atahukumiwa kwa kazi zake.



Mwisho: ombi langu sisi wenyewe wananchi,kama mtoa mada alivyo sema ni bora hata bila sheria tukaheshim utu wa mtu awe CCM au ukawa au asiye kuwa na chama. Mwenye hati miliki ya maisha ya mwanadam ni Mungu tu.
 
wewe endelea kumaanisha utakavyo wewe kauli za siasa, kama una mzazi wa kike hauwezi kushabikia udhalilishaji huu.... tena inaonekana kabisa ni sexual harassment..... sasa kama una mama ungeelewa....



Ninaye mama, dada, shangazi, mama wadogo/wakubwa lkn siyo Mafisadi na hiyo ndiyo tofauti! Dhidi ya fisadi Lowasa na Genge lake hakuna ustaarabu wala heshima kila kitu kinaruhusiwa hata Mungu ameruhusu hilio!
 

Nakupongeza sana kwa Mara ya kwanza kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa.Ukiendelea na msimamo huu nakutabiria makubwa,ila angalizo hayo maneno yawe yanatoka ndani ya moyo na si kujionyesha kwa watu kuwa unachukia kitendo hicho bila kujali wamefanya wa chama gani.Naomba ukemee na yale yaliyofanyika Mwanza kumdhalilisha Lowasa na yule kijana wa shairi na Magufuli na makada wa CCM kupiga makofi.Mimi binafsi sipendi kuwadhalilisha watu wazima kwa kisingizio cha itikadi ya vyama.
 
Kwasababu mwanamke mwenzako amefanyiwa hivyo ndo umekuja kukemea hapa?
Wakati Lowasa anadhalilishwa ulikuwa wapi?
CCM mmeanzisha hizi siasa. Anza kuwakemea Nape na wenzake.

Mkuu mbona hata huyu mleta uzi anaonekana kama vile ana, ajenda kudhalilisha ingawa kafichama kwenye huo huo udhalilishaji, hebu soma vizuri utaweza kagundua.
 
Katika hili naweka itikadi pembeni shonza umeongea vzr
 
Hayo maneno mpelekee yule msoma utenzi wenu ambaye akitukana Magufuli anabaki anachekelea!
 
Uchuguzi una mengi Kama una Roho nyepesi wallah unajitundika mume anadhalilishwa Kwa kujitakia maana Ni ukweli ila Kwa upande hasa wa huyu Mwana mama mie Leo imeniuma kabisa na Hawa vijana wa Chadema Hawa Kama hamumpendi Lowassa msimdhalilishe Mkewe!

Siyo lazima awe ni CDM inawezekana hata ni CCM ,huyo mtu alikuwa ameshaandaliwa na Wa kachukua video pia.
 
Leo umeongea point sina cha kuongeza

Usimpongeze hana nia nzuri maana wanaoisambaza ni CCM huku wakidai CHADEMA wasiomtaka Lowasa ndio wanaofanya hivyo. Hiyo ni mipango michafu ya CCM kuendelea kudhalilisha watu.
 

Vp na wale watu wanaosambaza picha za nyoso kumuingiza kidelo mchezaji mwenzake wafanywe nin na lile gazeti lililochapisha hadi picha ya lile dolee tuwafanye nin...ukiweza kujibu hapo nahisi tutakuwa tumetenda haki kwa hawa wote wahangaa
 
Akaunti ya Juliana shoza iko hacked? Maana najua yeye huwa anaandika matusi tuuu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbona hata huyu mleta uzi anaonekana kama vile ana, ajenda kudhalilisha ingawa kafichama kwenye huo huo udhalilishaji, hebu soma vizuri utaweza kagundua.

Kweli mkuu Ninaweza. Mleta uzi ana jambo kaliweka nyuma ya pazia katika uzi huu! Vikichanganya tu, ataonesha rangi zake! Tusubiri tuone.
 
Last edited by a moderator:

this is painfull:taifa linakwenda kugawanyika yetu macho.mambo usiyopenda ufanyiwe usimfanyie mwingine mana lazima iko siku utalipia -
 
Usiigope kugawanyika kwa Taifa.....walio asisi hili taifa wako mbele ya haki na watakaoligawa watakwenda mbele ya haki pia.Na watakuja wengine wataliunda upya hili taifa.
 
mama Regina alikua anaongea, pembeni yake kuna kijana akaanza kumshika mkono kumpapasa, mara baada ya kumshika mkono, akaenda mbele zaidi akamshika sehemu ya nyuma katika mwili wake (NYOSSO ACTION). haikua vizuri.

ok mkuu..lakini hata huyu kijana, yeye alikuwa na haki ya kumfanyia mama mheshimiwa mambo hayo, maana haielezwi kama kuna hatua yoyote aliyochukuliwa, zaidi sana inapendekezwa kuwa hatua zichukuliwe kwa aliyechukua video pamoja na wanaozisambaza...
 


Mkuu sio wote unaowaona kwenye kundi wana nia safi na kundi husika, wengine ni mamluki toka kwenye kudi lingine. Kumbuka ile Clip ya Masaburi na wale vijana waliojifanya ni wana Chadema.
 
Nimepata hasira hadi basi,naona kama ni mke wangu kafanyiwa hivo niko tayari kufa nisingeweza vumilia ningemtafuta popote alipo kwa gharama yoyote ile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…