Tuacheni tabia hizi ni mbaya katika maisha yetu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. Hebu angalia hapo nyumbani kwako!

Vitu msivyovihitaji Leo wala kesho mmeweka vya nini? Umenunua makochi mapya Yale ya zamani mmegawana vyumbani mnaishia kurundika minguo hapo na kufuga mipanya.

Godoro umenunua jipya la zamani umeviringisha juu ya kabati. Kabatini kwako kuna nguo ulivaa ukiwa secondary mpaka Leo unazo eti ukumbusho au utazivaa ukipungua.

Jikoni ndo shida iliposhika hatamu! Mivyombo ya plastiki imepaukiana imeyayuka na moto ipo tu eti vyombo vya watoto. Mahotpot yamekata roho imebaki kuwa sufuria we unalo tuu. Mxiuuu
Ndoo hata hazitumiki zipozipo tu, hata maua hazifai kupandia we unazogo tu huchomi, hutupi wala huzihitaji.. Sa zanini hapo??
1f621.png
1f621.png


Vyombo vya udongo vina mapengo na magego kama vinang'atwaga au vinapiganaga vyenyewe.
1f602.png
1f602.png
. Isitoshe kila kimoja na dizaini yake havifanani coz seti imeshavunjikavunjika hivo ndo vimebaki. Unaboa...
1f60f.png
1f60f.png
1f60f.png


Dressing table imejaa mikopo na mibox haina Kazi, perfume ya mwaka 2000 unayo hapo kisa ukumbusho wa zawadi. Ushamba huooo...
1f62b.png
1f62b.png


Stoo yako mwenyewe ila unaiogopa kuingia coz imejaa vitu visivyohitajika imekuwa ghetto la panya na nyoka kama sio nge badala Ukiweka mnavyohitaji. Ipo siku mtakuta mamba humo..
1f432.png
1f432.png
1f432.png


Nje ya nyumba kuna gari la urithi la babu lipogo tu hapo linafuga ndege na vibaka... Aaalaaaa
1f621.png
1f621.png
1f621.png

Kutupa vitu visivyohitajika hamtupi eti Dhambi na kugawa hamgawi coz mmeviharibu hadi mwisho mtampa nani? Kutwa mnapishana mahospitalini mnaumwa mafua na vifua kila siku.

Kwann msiumwe na mnakaa dampo ? Hivi mnajua km huu ni ugonjwa? Unaitwa hoarder disorder. Tena mnawaambukiza watoto wenu kwani wanajua kwao hata kikopo cha icecream hakitupwagi kinaoshwa kinawekwa hapo.

Halafu bado unaendelea kumuomba Mungu akupe, akupe uweke wapi na kwako pameshajaa?
Kama umemind natuma tena
1f3c3_200d_2642.png
1f3c3_200d_2642.png
1f3c3_200d_2642.png
 
Akiba haiozi mkuu!...

Sent from my itel it1500 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hujui tunayatumia kuwafunza wajukuu kuwa tulikuwa na gramaphone changer? We vip?? Mtoto wa 1990 ataijua hiyo??
 
Duh naona umekereeeeeeka mkuu sasa nyumba sio yako we inakuhusu nn Kama naumwa mafua wewe unanichangiaga hela ya ospitali acha izo unajifanya unanijua saaana
Hela zangu vitu vyangu wewe hunanisaidia. Kwa lolote eti oooh nyumba Inakua dampo ya kwako na hapo ndio sikai kwako nigekaa kwako ingekuaje
Acha kufuatilia maisha ya watu wadau mm nashauri hadi miswaki ikiisha msitupe alaf tumuone atapike


Sent from my RIDGE 4G using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom