Good morning Jf!!
Kuna msemo huwa unasema maisha ni kama duara tunazunguka na tutakutana. Thread hii inawahusu wote wenye tabia kama hzi. Kuna watu wwngi kwenye jamii zetu wakifanikiwa huwa wanasahau walikotoka % kubwa ya waafrica tupo hivi to be honesty.
Since naanza 1st yr nilikua na brother wangu wa kitaa ambae yeye alikuwa amegraduate chuo, alikuwa hana kazi wala mshe yoyote. Kipind hicho alikuwa ananioomba sana vocha, pesa za nauli kwenda kufanya interviews nk. Ofcoz nilikua nampa sana namsaidia. Mwaka 2018 alipata kaz kwenye taasisi kubwa hapa nchin binafsi nilikua sijui kama amepata kaz lkn niliskia kwa wana kitaa jamaa kala shavu na alikuw kashakata mawasiliano na mimi muda. Nilijarib sana kumtafuta lkn alikuwa hapokei sim, mara akwambie yuko busy na hakutafuti ila insta anapost, whatsapp nk nikapotezea.
Wanangu wengi tu waliontangulia kupata kaz walichange kabisa walikata mawasiliano ni wana wachache sana ambao tulikuwa pamoja. Kibaya kinauma sana kuna mtu nimemsaidia sana chuo bila mm angekua alidisco nmesave sana kwenye tests, UE amepata kazi kwenye Organization huko KENYA ina deal na projects kanipotezea wtf?? Hawa ni mfano tu ila wapo wwngi.
Narud kwenye thread, mnajua huku kwenye campun, Organizations kuna kazi nyingi hta part time huwa zinatokeaga na wengi ambao huwa wanajulishwa ni wafanyakaz walete watu haraka, lakin utakuta rafiki yako anajua fika kabisa huna kazi ila anaona kinyongo kukupa hio fursa.
Mfano mimi mpaka sasa nimesaidia watu5 wamepata permanent jobs. Ukisha kuwa kwenye system ya ajira kupata connections ni easy sana coz kuna meetings, seminars tofaut na mnakutana na watu tofauti.
Tuache roho mbaya jiulize umesaidia watu wangap mpaka sasa? Ukiwa na roho ya dizain hii huwez fanikiwa hta siku moja. Kumsaidia mtu sio kumpa pesa au kumpaa offa za bia kila siku bali msaidie apate kazi hapo umesaidia, tusisahau tuliko toka. Kuna watu wana suffer kitaa years ila siku anapata kaz yenye maslahi na anakuzid kimaendeleo. Kuwai pata kazi sio kutoboa maisha kama wengi wanavyodhani ila kutakuw na magap tu.
Ukiwa na rafiki yako aliyeajiriwa ni rahis sana kukupa connectio ww hata kama sio leo wala kesho ni rahis sana ku connekt. Mfano mimi nimeskia kuna mtu anahitajika nikamfata manager/hr nimwambie na mtu anaweza kufit please nipe iyo chance tunampa mwez akishindwa kufit tunamtoa unadhan atakataaa? Sio rahis sema wabongo wengi hatuna roho ya kusaidiana ila tumejaa wivu na roho mbaya.
Mpaka sasa mimi nimesaidia watu wengi tu ila wa5 hawa wamepata parmanent jobs na mmoja yumo humu jf. Na nitaendelea na roho hii hii ya kusaidia wengine no matter what. Mimi nilisaidiwa kupata kazi na mtu ambae nilikutana nae Bar simjui akanitafutia kazi yenye maslah why me nishindwe saidia wengine?? Na siku zote usimtegemee ndugu au rafiki kukusaidia mtu atakae kusaidia ni mwingine kabsa ambae hata humjui...
Mwisho, tusikate tamaa kama huna kazi endelea ktuma maombi ipo siku mambo yatatiki, kila mtu ana siku yake aliyopangiwa na mwenyezi Mungu. Waliokutangulia kupata kazi inajua huwa inauma sana afu unakuta ndo kakupotezea mazima achana nao fanya yako, kingine ishi kama huna elim maisha yatakuw simple sana jichanganye na watu usiogope. Kwenye ma bar makubwa, kanisan huko ndo connection zilipo wwngi hatujui tu. NICE DAY