Tuache usanii wa kuvaa barakoa

Lorenzo Samike

JF-Expert Member
Jun 18, 2021
1,188
1,912
Haya mabarakoa yamejaa usanii mtupu.

Ukiingia ofisi ya umma unalivaa. Ukitoka unalivua.

Hata mama yetu akiwa ughaibuni analivaa. Akishuka uwanja wa ndege analivua anaendelea kupuyanga.

Mabarakoa yamekuwa kama fasheni ya kubandika na kubandua. Unaangalia tu mazingira muafaka.

Barakoa imepoteza ile dhima yake ya msingi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa bandia wa uviko.

Ni likitambaa tu linalovaliwa kulingana na muktadha wa eneo husika.

Ukimuona beberu unalivaa, akiondoka unalibandua.

Kuna haja ya kuendelea kuigiza?
 
Back
Top Bottom