Tuache upotoshaji,January na Ngeleja wametumia hekima

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Siku za hivi karibuni kuna audio zilivuja ambapo silisikika sauti za Mzee Makamba,Membe,January,Mzee Kinana na Ngeleja wakimkejeli Rais Magufuli

Mwanzoni sie wengine tulijua labda ni uzushi tu lakini kumbe ni ile audio ni uhalisia mtupu.

January Makamba na William Ngeleja kwa kuongozwa na Hekima wamejutia kitendo chao kwa kumuomba radhi Mwenyekiti wao ambaye pia ni Rais wa Jamhuri wa Muungano Dr John Magufuli

Leo hii Rais Magufuli amenukuliwa akisema kwamba January na Ngeleja walimuomba msamaha na yeye ameamua kuwasamehe

January Makamba na William Ngeleja wameonyesha ukomavu wa fikra na zaidi ghala lililosheheni weledi lukuki kwa kitendo walichofanya

Pia nampongeza Rais Magufuli kwa uungwana wake kwa kukubali kuwasamehe vijana wake

Tuwapuuze wale wote ambao wanawazodoa January na Ngeleja kwa kitendo chao cha kiungwana walichofanya,

Hongera January Hongera Ngeleja na Kongole Mh Rais Magufuli kwa hili

Alex Fredrick
Dar es salaam
 
Hao Voda kuwadukua hao jamaa, wamevunja ile "privacy policy" yao

Tit fir tat.....

Hivi kwa mfano Jiwe akidukukiwa atafurahi kweli??
 
Busara wasingejihusisha na yale waliyofanya, sio unaharibu mambo halafu unakimbilia kuomba msamaha
 
Wameomba msamaha sio kwakuwa wamejutia lolote, ila ni kwakuwa hawana uwezo wowote nje ya siasa za mbeleko. Januari na Ngeleja ni nani kati yao anaweza anaweza kushinda kwenye uchaguzi kihalali bila mbeleko ya vyombo vya dola? Na mwenye uwezo wa kuamrisha vyombo vya dola vihakikishe unatangazwa mshindi ndio huyo waliyemuomba msamaha. Hao jamaa hawakuwa na kosa lolote zaidi ya kuogopa maisha ya nje ya siasa kwani hawana ujanja wowote.
 
Siku za hivi karibuni kuna audio zilivuja ambapo silisikika sauti za Mzee Makamba,Membe,January,Mzee Kinana na Ngeleja wakimkejeli Rais Magufuli

Mwanzoni sie wengine tulijua labda ni uzushi tu lakini kumbe ni ile audio ni uhalisia mtupu.

January Makamba na William Ngeleja kwa kuongozwa na Hekima wamejutia kitendo chao kwa kumuomba radhi Mwenyekiti wao ambaye pia ni Rais wa Jamhuri wa Muungano Dr John Magufuli

Leo hii Rais Magufuli amenukuliwa akisema kwamba January na Ngeleja walimuomba msamaha na yeye ameamua kuwasamehe

January Makamba na William Ngeleja wameonyesha ukomavu wa fikra na zaidi ghala lililosheheni weledi lukuki kwa kitendo walichofanya

Pia nampongeza Rais Magufuli kwa uungwana wake kwa kukubali kuwasamehe vijana wake

Tuwapuuze wale wote ambao wanawazodoa January na Ngeleja kwa kitendo chao cha kiungwana walichofanya,

Hongera January Hongera Ngeleja na Kongole Mh Rais Magufuli kwa hili

Alex Fredrick
Dar es salaam

Sasa wametumia hekima tuache unafiki gani tena?
 
asante bro mi miongoni.mwa wanakula nchi na kuhadaa wanainchi katika mikutano si unajua mwanasiasa haruhusiwi kuingia jimbo mwingine lakini si wasiasiwa tunaruhusiwa kupanda macosta ila saivi mnaudhi bwana mnachukua wale watu kwenye vikundi vya mikopo tu hamlipi poa
Pole yako wewe
 
Back
Top Bottom