Tuache kukuza mabilionea uchwara wa madini (tanzanite)

BlackBox

Senior Member
Nov 26, 2016
109
77
Leo waziri Biteko gavana wa benki kuu ndg Luoga, wakuu wa mikoa ya Manyara na Kilimanjaro pamoja na viongozi wengine walikua mererani kwaajili ya makabidhiano ya mawe mawili ya tanzanite yenye ukubwa tofauti. Katika zoezi hilo serikali imepata kodi ya 7% zaidi ya milioni 900.

Thamani ya mawe hayo ni bilioni 2.245 swali langu ni namna walivyosherehesha kuwa bwana Anselm Kawishe mmiliki wa mawe hayo amekua tena billionaire wa madini wakati ukitoa kodi na matumizi mengine hawezi kubakiwa hata na bilioni moja, baada ya muda wanapofilisika inaonekana walipokea fedha nyingi wakazichezea kumbe siasa ilipita humo ndani.

Waweke uhalisia huyo mfanyabiashara hajawa bilionea ni milionea tu wa kawaida hapa nchini.

Serikali inafanya kazi nzuri tumepata kodi tofauti na zamani lakini waache siasa za ubilionea uchwara.
 
LAIZER YUKO WAPI?
wazee hawa wakishapiga kodi na 10% zao ni mbio ubilionea unabakinao kiusikojulikana.

Inatosha kwenda kuchukua kodi lakini siasa zinakua nyingi zanini sana mara bilionea mpya mjini mara bilionea mwingine n.k na kesho hiyo ndo habari kuu kwenye magazeti yetu.
 
Leo waziri Biteko gavana wa benki kuu ndg Luoga, wakuu wa mikoa ya Manyara na Kilimanjaro pamoja na viongozi wengine walikua mererani kwaajili ya makabidhiano ya mawe mawili ya tanzanite yenye ukubwa tofauti. Katika zoezi hilo serikali imepata kodi ya 7% zaidi ya milioni 900. Thamani ya mawe hayo ni bilioni 2.45 swali langu ni namna walivyosherehesha kuwa bwana Anselm Kawishe mmiliki wa mawe hayo amekua tena billionaire wa madini wakati ukitoa kodi na matumizi mengine hawezi kubakiwa hata na bilioni moja, baada ya muda wanapofilisika inaonekana walipokea fedha nyingi wakazichezea kumbe siasa ilipita humo ndani. Waweke uhalisia huyo mfanyabiashara hajawa bilionea ni milionea tu wa kawaida hapa nchini. Serikali inafanya kazi nzuri tumepata kodi tofauti na zamani lakini waache siasa za ubilionea uchwara.
Hayo ni moja ya mawe madogo sana yanayopatikana huko mereran.

Hao wafanya biashara ukiona ameonyesha wazwaz hvyo ujue ana mzigo ndan wa ajabu.. wanayoijua biashara ya mawe watanielewa.. hata sku ile lile la laizer kuna watu arusha walikua wanaacheka tu..
 
Mna Roho mbaya tu waswahili. Whether ni bilionea au milionea hela ni zake na family yake. Akila akimaliza ni zake Sasa Roho zinawauma kwa sababu gani. Nendeni mkachimbe nanyi muwe ma trilionea wa ukweli. Nyambaf
Our minds are hard reinforced wired to avoid both physical and emotional pains. Everybody understands the nature of avoiding of physical pains. Accidentally set your hand on a hot burner, and your hand moves away from heat automatically; it's an instinctive reaction. Our minds have a number of ways to shield us from information that we have learned to perceive as painful. For example, at a concious level, we can rationalize, justify, or make a case for staying in losing,wrong or unsuitable reality. Some of the more typical ways we do this are to call our close buddies, talk to our gods, or look at indicators we never see, all for the express purpose of gathering nonpainful information in order to deny the validity of the of the painful information. At a subconscious level, our minds will automatically alter, distort, or specifically exclude information from our concious awareness. In other words, we don't know at a concious level that our pain-avoidance mechanisms are either excluding or altering the information being offered by the real life/relationship/business/market/poverty.
You'll pick and choose information that's consistent with what I expect, so that I can maintain a pain - free state of mind
 
Mna Roho mbaya tu waswahili. Whether ni bilionea au milionea hela ni zake na family yake. Akila akimaliza ni zake Sasa Roho zinawauma kwa sababu gani. Nendeni mkachimbe nanyi muwe ma trilionea wa ukweli. Nyambaf
Wala hatunaroho ya hivyo ni za kwake tunachojadili hapa ni uhalisia wa huo ubilionea wenye siasa lukuki za kuupiga mwingi, hivi wangeyanunua watoze kodi maisha yaendelee kulikua na shida gani. Tatizo bongo kitu kidogo siasa inapigwa mpk unaweza fikiri ni jambo kubwa la ajabu sana. Huyo waliyemuita bilionea atakapofilisika tunaanza mara alifuja mara hivi ila kiuhalisia alipokea hela ndogo sana.
 
Leo waziri Biteko gavana wa benki kuu ndg Luoga, wakuu wa mikoa ya Manyara na Kilimanjaro pamoja na viongozi wengine walikua mererani kwaajili ya makabidhiano ya mawe mawili ya tanzanite yenye ukubwa tofauti. Katika zoezi hilo serikali imepata kodi ya 7% zaidi ya milioni 900.

Thamani ya mawe hayo ni bilioni 2.45 swali langu ni namna walivyosherehesha kuwa bwana Anselm Kawishe mmiliki wa mawe hayo amekua tena billionaire wa madini wakati ukitoa kodi na matumizi mengine hawezi kubakiwa hata na bilioni moja, baada ya muda wanapofilisika inaonekana walipokea fedha nyingi wakazichezea kumbe siasa ilipita humo ndani.

Waweke uhalisia huyo mfanyabiashara hajawa bilionea ni milionea tu wa kawaida hapa nchini.

Serikali inafanya kazi nzuri tumepata kodi tofauti na zamani lakini waache siasa za ubilionea uchwara.
Cc Robot la Matope mzee wakukuza Hawa wachimba madini (gold diggers)
 
Mna Roho mbaya tu waswahili. Whether ni bilionea au milionea hela ni zake na family yake. Akila akimaliza ni zake Sasa Roho zinawauma kwa sababu gani. Nendeni mkachimbe nanyi muwe ma trilionea wa ukweli. Nyambaf
Waswahili tunasema wana 'kidakatonge' kimewakaa, yaani hawapendi chakula kipite kwa amani mdomoni kwenda tumboni.
 
Wacha ujinga mwamba! Yaani 7% iwe zaidi ya milioni 900? Kwa hesabu gani?
Unajua hata mimi nimeshangaa kitu kimoja maana mimi sio mdau wa madini, mkuu wa mkoa wa Manyara amesema serikali inapata zaidi ya milioni 900 wafanyabiashara wa madini nao wakapongeza kodi kupunguzwa kutoka 13% mpaka 7% sasa nafikiri kuna kodi nyingine zimefichwa hapo kama za halmashauri ama mkoa hapo sijui. Lakini kilichoelezwa namimi nimekieleza hivyo japokua kama kuna wahusika humu wanaweza kutuelezea zaidi.
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi. Maana ukiangalia hiyo 7% kwa hizo 2.45b ni kama 170m sasa huyo RC anayesema 900m ameitoa wapi? Serikali ya waongo hii na kutafuta sifa za kijinga! Makongoro naye huwa anaropoka sana!
 
Back
Top Bottom