Tuache hii tabia siku za Ibada

Tuache hii tabia siku za Ibada

DAD'S SON

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2015
Posts
392
Reaction score
466
IBADA kwa tafsiri ya kawaida ni kindi cha mwanadamu kuwa karibu na muumba wake(wasiliana).

Napata tabu sana kujua nini kinatusumbua sisi watu wa karne.Unakuta mtu anaenda ibadani utadhani anaenda kwenye uzinduzi wa album ya msanii wa Bongo fleva!

Tunakwama wapi jamani?? Ebu ifike wakati tujue tunaenda ibadani kufanya nini??.Hatuendi ibadani kwa lengo la fashion show,ni kwa lengo la kupata baraka za Mungu.

Story flani ivi yenye mafunzo.

Kuna mzee mmoja alikuwa na kijana wake ambaye walikuwa wanafanya kazi wote gereji asa kuna siku moja Muda wa kwenda kufanya ibada ukafika baba yule akamwambia kijana wake "Ebu nenda kabadili iyo nguo twende kwenye ibada" kijana yule akasema "MUNGU angalii nguo anaangalia MOYO".Basi baba yule hakusema kitu wakaenda ibadani.

Siku tatu mbele wakiwa pale gereji baba yule akambia kijana wake "leo tumepata mwaliko wa Chakula cha jioni kwa waziri mkuu mida ya saa saba inabidi twende" kijana yule akasema "sawa baba".

Saa saba ikafika yule baba akamwambia kijana wake "Muda ndo huu twende" kijana yule akamwabia baba yake "ngoja nikabadili izi nguo baba ndo twende" baba yake akamwabia "wewe uliwaisema Mungu aangalii nguo anaangilia MOYO leo vipi huoni km mwaliko wa chakula cha jioni kwa waziri mkuu utaangalia TUMBO na si nguo??!" Kijana yule alikosa jibu la kumjibu baba yake.

FUNZO: tukisijifanye Wema kwa binadamu na kuleta dharau kwa aliekuumba,tuheshimu nyumba za ibada km unavyoheshimu unapoharikwa kwa wakuu wa nchi.

HITIMISHO:Tusichukulie vitu poa na kuleta mazoea kwenye mambo msingi,tuheshimu nyumba za ibada ili mtupunguzie majaribu huko ibadani.
 
Hahaha umenikumbusha leo ibadani kuna mwanakwaya kavaa kinguo kimembana mpaka akikaa unamuona huyu anapata tabu...na hapo nje kuna bango kabisaa la mavazi yaliyokatazwa kuvaliwa kanisani...basi kwasababu namfahamu nikamfuata ibada ilipokwisha nikamwambia "masauti leo naona nguo ulizofua hazikukauka vizuri ee"" akabaki aah katibu bwanaa hii nguo sijaivaa siku nyingi ujueee...nikamwambia uwe na amani tuu...

Watu mnaopenda kufanya showoff kwenye nyumba za ibada hasa wakati wa misa mjitafakari sana asee..
 
[emoji4][emoji4] show off zitatupeleka kubaya mwisho wa siku
 
Ni Wapi Pa Kuonesha Mitindo Ya Mavazi Kama Si Penye Mikusanyiko Ya Watu Waliovaa Nadhifu Kama Ibadani? Ila Mavazi Yawe Ya Adabu Na Heshima. Siyo Yale Ya Kuonesha Ramani Ya Maungo Ya Mwili, Na Nusu Uchi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom