Tuachane na ilani za vyama tuwe na ilani ya Taifa

MZALENDOWAKWELIKWELI

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
331
Reaction score
212
Ilani ya uchaguzi ni kama mkataba wa ajira cha kushangaza kwa Tanzania mkataba huu unaandikwa na mwajiriwa (mwanasiasa) badala ya mwajiri(mwananchi). Napendekeza tufanye kinyume chake; kila iishapo miaka mitano wananchi ndio tuwaambie wanasiasa nini tunataka atakayeshinda atufanyie na si wao kutuambia tukiwachagua watufanyie nini, jukumu la mwanasiasa wakati wa kujinadi liwe kutueleza ubunifu atakaoutumia na chama chake kutufikisha pale tunapotaka watanzania...

Tume ya taifa ya uchunguzi ikishirikiana na Tume ya mipango ya Taifa ndio tuwape jukumu la kukusanya maoni ya Watanzania ya kwamba wanataka waione nchi yao iko wapi miaka mitano, kumi, kumi na tano, hamsini ijayo kisha maoni hayo yakiratibiwa na wataalam wa mipango (economists) waitafsiri katika ilani ya Taifa ya miaka mitano mitano.

Uzuri na faida za mfumo huu ni zifuatazo:
1. Nchi inapata dira na mwelekeo unaoeleweka na utendaji wa mwanasiasa naopimika (perfomance appraisal)
2. Ilani hii itakuwa ni 'road map' yenye muafaka wa kitaifa katika mgawanyo wa keki ya taifa hivyo kupunguza pengo ukuaji uchumi na punguzo la umaskini
3. Ilani ya Taifa itaongeza ubunifu wa namna ya kutumia rasilimali za taifa kutuletea maendeleo badala ya misaada kutoka nchi za nje.

Ni katika ilani ya Taifa pekee mwananchi anaweza kutoa masharti yafuatayo kwa mwanasiasa:
1. Tunataka Rais ambaye hata siku moja hatatoka nje ya nchi kwenda kuomba msaada kwa nchi tajiri badala yake akatafute masoko, wataalam wa kuwaajiri kwenye vyuo vyetu ili tutransfe teknoloji yao, partner wa maendeleo na sio doner n.k; ukweli ni kwamba hakuna kinachotudidimiza kwa wanasiasa kusaini mikitaba ya kinyonyaji kama misaada, hata ushoga uko njiani kuletwa tuuingize kwenye katiba chanzo ni bakuli la misaada
2. Sharti la kufungua kiwanda kimoja kila mwaka: ajira, soko la mazao yetu litapatikana
3.Sharti la kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi na sekta ya nyumba na makazi; hii itapelekea ongezeko la wawekezaji kwenye sekta ya ujenzi wa makazi bora yaliyopimwa na bei nafuu hivyo mtanzania kupunguza kuugiaugua kwa chanzo cha makazi duni.
4.Sharti la mfumo wa bima ya afya kwa kila mwananchi kuchangia kidogo wakati yuko mzima ili anapougua michango ya wengi imtibu kwa matibabu bora bila kuilazmu serikali kugharamia chochote
5. Sharti la kuwekeza kwenye elimu si chini ya asilimia 10 ya pato la taifa....kwa kufanya hivyo automatically maprofesa hawatakimbilia siasa inayolipa kwa sasa badala yake watasalia kwenye kufanya tafiti na kufundisha watu wetu na wenye digrii watafundisha shule za msingi. ...tofauti na sasa vilaza ndo wanakimbilia ualimu.
6. N.k

Kama wazo hili la ILANI YA TAIFA ni jema naomba tulipigie debe liingie kwenye katiba.

Nawasilisha.
 
Mkuu MZALENDOWAKWELIKWELI,

Nakubaliana na mawazo/mtazamo wako, baadhi ya Nchi hasa Amerika, huo ndio utaratibu, ikiwa ni malengo ya Taifa na chama chochote kitakachoshika hatamu ya uongozi itabidi kufanya hayo KWANZA, na nyongeza kuwa mipango mizuri ya Taifa inayotokana na chama.

Hii hupunguza kuanza moja kwa kila uongozi, mikwaruzano na kufanya mwelekeo bora kama Taifa. Hii naunga mkono mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani ni SERA badala ya ILANI ya taifa. Mfano mzuri ni US Policy on Terrorism; piga uwa iwe ni Democrat, Conservative, au chama chochote au mgombea yeyote iwe kupitia chama au binafsi; iwe ni Bunge la makabwela au la mamwinyi; ni lazima ILANI, sheria, kanuni, taratibu, au slogan yoyote itakayopitishwa ioane na SERA hiyo ya taifa kuhusu ugaidi.

Haiwezekani, kwa mfano, akaibuka kiongozi au mbunge yeyote mahali popote iwe nje au ndani ya bunge akatangaza kwa mfano anawapa magaidi muda wale Idd na kuomba msamaha na watakaofanya hivyo "watasamehewa". Mbele ya wamarekani utaonekana punguani na kiongozi wa aina hii anapaswa ku-resign mara moja kwa kuwa sera yao hii hairuhusu NEGOTIATION ya aina yoyote na magaidi.

Vivyo kwa sera nyingine za taifa kama ile ya Mashariki ya Kati, n.k. Marais wote wa Marekani wanafungwa na sera hii ambayo inataka Israel ilindwe dhidi ya maadaui zake.

So, in short, nakubaliana na wewe kwamba tuwe na sera za kitaifa ambazo ilani zote za vyama ni lazima zioane na sera hizi. Kwa mfano suala la MAJIMBO ni suala kubwa na zito lakini kwa kuwa hakuna sera za kitaifa zinazoeleweka kuhusiana na mipaka ya kimaeneo ya nchi yetu vyama kama Chadema vimekuja na sera zao za MAJIMBO (kimsingi wako sahihi), kesho kitaibuka chama kingine kitakuja na sera yake tofauti na hii, n.k.

CCM wao wako na sera ya kugawa nchi fasta kadiri inavyowezekana simply kwa kuwa hakuna sera wala taratibu zinazoeleweka zaidi ya Rais kutumia mamlaka yake aliyopewa kikatiba bila kuwa na udhibiti wowote.
 
Unachsema ni kitu kizuri sana ifike mahala tuwe na ilani ya Taifa maana itasaidia mwendelezo wa jambo hata kama utawala utaenda kwa chama pinzani
 
U r very vry right....kilichopo sasa kila mtu akiamka anafanya alichoshauriana na mkewe usiku wa jana yake....we don't have what we call "national interests"....siku ukija ukaingia upinzani unapindua kila kila kitu kichwa chini miguu juu....mwisho wa siku ni maktaim hatupigi maendeleo. ....
 
MKUKUTA na MKURABITA sio vitu kama hivyo? Lakini kuna kitu unacho!
 
Ilani ya uchaguzi ni kama mkataba wa ajira cha kushangaza kwa Tanzania mkataba huu unaandikwa na mwajiriwa (mwanasiasa) badala ya mwajiri(mwananchi). Napendekeza tufanye kinyume chake; kila iishapo miaka mitano wananchi ndio tuwaambie wanasiasa nini tunataka atakayeshinda atufanyie na si wao kutuambia tukiwachagua watufanyie nini, jukumu la mwanasiasa wakati wa kujinadi liwe kutueleza ubunifu atakaoutumia na chama chake kutufikisha pale tunapotaka watanzania...

Tume ya taifa ya uchunguzi ikishirikiana na Tume ya mipango ya Taifa ndio tuwape jukumu la kukusanya maoni ya Watanzania ya kwamba wanataka waione nchi yao iko wapi miaka mitano, kumi, kumi na tano, hamsini ijayo kisha maoni hayo yakiratibiwa na wataalam wa mipango (economists) waitafsiri katika ilani ya Taifa ya miaka mitano mitano.

Uzuri na faida za mfumo huu ni zifuatazo:
1. Nchi inapata dira na mwelekeo unaoeleweka na utendaji wa mwanasiasa naopimika (perfomance appraisal)
2. Ilani hii itakuwa ni 'road map' yenye muafaka wa kitaifa katika mgawanyo wa keki ya taifa hivyo kupunguza pengo ukuaji uchumi na punguzo la umaskini
3. Ilani ya Taifa itaongeza ubunifu wa namna ya kutumia rasilimali za taifa kutuletea maendeleo badala ya misaada kutoka nchi za nje.

Ni katika ilani ya Taifa pekee mwananchi anaweza kutoa masharti yafuatayo kwa mwanasiasa:
1. Tunataka Rais ambaye hata siku moja hatatoka nje ya nchi kwenda kuomba msaada kwa nchi tajiri badala yake akatafute masoko, wataalam wa kuwaajiri kwenye vyuo vyetu ili tutransfe teknoloji yao, partner wa maendeleo na sio doner n.k; ukweli ni kwamba hakuna kinachotudidimiza kwa wanasiasa kusaini mikitaba ya kinyonyaji kama misaada, hata ushoga uko njiani kuletwa tuuingize kwenye katiba chanzo ni bakuli la misaada
2. Sharti la kufungua kiwanda kimoja kila mwaka: ajira, soko la mazao yetu litapatikana
3.Sharti la kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi na sekta ya nyumba na makazi; hii itapelekea ongezeko la wawekezaji kwenye sekta ya ujenzi wa makazi bora yaliyopimwa na bei nafuu hivyo mtanzania kupunguza kuugiaugua kwa chanzo cha makazi duni.
4.Sharti la mfumo wa bima ya afya kwa kila mwananchi kuchangia kidogo wakati yuko mzima ili anapougua michango ya wengi imtibu kwa matibabu bora bila kuilazmu serikali kugharamia chochote
5. Sharti la kuwekeza kwenye elimu si chini ya asilimia 10 ya pato la taifa....kwa kufanya hivyo automatically maprofesa hawatakimbilia siasa inayolipa kwa sasa badala yake watasalia kwenye kufanya tafiti na kufundisha watu wetu na wenye digrii watafundisha shule za msingi. ...tofauti na sasa vilaza ndo wanakimbilia ualimu.
6. N.k

Kama wazo hili la ILANI YA TAIFA ni jema naomba tulipigie debe liingie kwenye katiba.

Nawasilisha.

Shikamoo mwanzisha mada, hili wazo nimekuwa nikitamani litokee mda mrefu, kwanza itakuwa ndo mwisho wa mafisadi kuinajisi nchi yetu tukufu. Siku hii kitu ikifanyika Tanzania ndo siku na mi nitakuwa mwanasiasa. Asante mkuu kwa kuja na wazo tangu kama hili. Shikamoo tena.
 
MZALENDOWAKWELI maoni ya dudus ni sahihi. Katika mfumo wa vyama vingi hauwezi kuwa na Ilani inayofanana kwa vyama vya siasa. Ilani kwa tafasiri nyepesi ni mkakati wa chama cha siasa kutekeleza sera za nchi za maendeleo, usalama na kadhalika. Kwa hiyo vitu tunavyotakiwa kuwa navyo ili kila chama chochote kitakachoingia madarakani kitafuata ni Katiba ya nchi, sera na sheria zilizopitishwa na Bunge.

Ilani ya vyama inatakiwa kuainishwa mikakati ya chama kutekeleza Katiba na sera ya nchi ili kutuwezesha kupata maendeleo na usalama wa nchi yetu. Mikakati ingawa inasemwa kuwa ni mkataba kati ya chama na wananchi, lakini inaweza kubadilishwa wakati wowote na chama kinapoingia madarakani na au hata kuongeza mambo mengine yasiyokuwemo ndani ya ilani yake waliyoiuza kwa wananchi.

Ndiyo maana kwenye nchi ambazo zinaruhusu vyama kuungana ili kuunda Serikali, wanapokubaliana pia wanatengeneza ilani yao ya mambo yatakayotekelezwa na Serikali wanayoiunda.
 
Hitimisho la Ndumbayeye "lakini kuna kitu unacho " linaashiria ameona ilani ya taifa ni zaidi ya sera; sera huwa inakuja baadae kutoa muongozo wa jambo mahususi lililomo ndani ya ilani....jukumu kubwa la ilani ya Taifa ni ku play part kama corner stone ya sera zote za nchi....ndugu Getstart, ilani ya Taifa inasimama kama dira ya Taifa, ni wapi kama watanzania tunataka tujione baada ya miaka mitano. ...inasimama kama benchmark au corner stone ya kupima ufanisi wa utendaji wa chama kitachoshika hatamu....baada ya ilani ya Taifa kutolewa kazi ya vya siasa ni kutengeneza mpango mkakati (unaweza kuziita ilani za vyama) wa utekelezaji wa ILANI YA TAIFA na hata zaidi ya hapo na kazi ya mwananchi ni kupima ni yupi plan yake inatekelezeka na kwa rasilimali zipi alizozipendekeza.....mfano ilani ya Taifa inaweza kusema baada ya kupata maoni ya wengi kipaumbele cha kwanza kiwe elimu na uwekezaji wake uwe 10% ya pato la Taifa....chama A ruksa kuja na mkakati wa kuwekeza 12%, chama B 15 % but si chini ya asilimia 10 iliyowekwa na Watanzania katika ilani ya Taifa ama si ruksa chama Q kuja na kipaumbele cha kununua ndege ya Rais hata kama ni kwa gharama ya watoto kwenda shule....kwa sasa ni rahisi serikali kujigamba imejenga mfano km. 1,000 za lami ambayo haikuwako tukipata uhuru LAKINI hatujiulizi wala kuwakosoa pengine kwa rasilimali zilizopo walipaswa kujenga 2,000. Kasoro hii ingetatuliwa na ILANI ya Taifa!
 
... Kuwe na sera ya Kuifuta CCM na matendo maovu yote ya CCM katika Historia ya Nchi hii... Bila kufanya hivyo kunahatari kubwa ya kujenga Taifa lenye kuwashangilia WAHUJUMU uchumi! CCM imesababisha Watanzania kutokuona aibu kwa kushindwa kuwajibika, hawaoni aibu kuomba na kutoa rushwa! Wafanyakazi wengi wako kwenye Salary Maintenance program... Mawaziri wamekuwa makanjanja wa kuuza Mali za Watanzania... Taasisi ya Urais iko holiday toka walipoingia ikulu kazi yao ni Utalii Duniani kote...kila mtu sasa anatamani kuwa mtalii... Sera za nchi zianishe kwa uwazi majukumu na wajibu wa kila Idara na Vitengo nyeti vya nchi hii! Pawepo na Uwajibikaji plus adhabu kali kwa wahujumu Uchumi kama wafanyavyo Wachina!!! Rasilimali Za Watanzania Ziwanufaishe Watanzania kwa 97% kama ambavyo Australia na nchi nyingine wafanyavyo! Mishahara ya Watanzania waliko kwenye MNCs ziendane na za Wazungu ili faida ya uwekezaji ionekane, Marufuku Kuwinda kusafirisha Wanyama wetu! Sekta ya Utalii imilikiwe na Watanzania 100% ... Critical Infrastructures kama Barabara, Ndege, Umeme, Maji, Gesi imilikiwe na serikali 100% ... Tuepuke kununua umeme wa magenerator za Symbion et al... Benki Kuu iache ujinga wa kusimamia "Price Stability" wakati haina udhibiti wa bei ya Mafuta kwenye soko la Dunia! Badala yake ijikite kwenye zile Objectives za Kuwawezesha Wazawa wamiliki Migodi Mikubwa, Viwanda, Mashamba na sekta za Uzalishaji, Sera za IMF/WB haiwezi kutusaidia kamwe...
 
Nadhani ni SERA badala ya ILANI ya taifa. Mfano mzuri ni US Policy on Terrorism; piga uwa iwe ni Democrat, Conservative, au chama chochote au mgombea yeyote iwe kupitia chama au binafsi; iwe ni Bunge la makabwela au la mamwinyi; ni lazima ILANI, sheria, kanuni, taratibu, au slogan yoyote itakayopitishwa ioane na SERA hiyo ya taifa kuhusu ugaidi.

Haiwezekani, kwa mfano, akaibuka kiongozi au mbunge yeyote mahali popote iwe nje au ndani ya bunge akatangaza kwa mfano anawapa magaidi muda wale Idd na kuomba msamaha na watakaofanya hivyo "watasamehewa". Mbele ya wamarekani utaonekana punguani na kiongozi wa aina hii anapaswa ku-resign mara moja kwa kuwa sera yao hii hairuhusu NEGOTIATION ya aina yoyote na magaidi.

Vivyo kwa sera nyingine za taifa kama ile ya Mashariki ya Kati, n.k. Marais wote wa Marekani wanafungwa na sera hii ambayo inataka Israel ilindwe dhidi ya maadaui zake.

So, in short, nakubaliana na wewe kwamba tuwe na sera za kitaifa ambazo ilani zote za vyama ni lazima zioane na sera hizi. Kwa mfano suala la MAJIMBO ni suala kubwa na zito lakini kwa kuwa hakuna sera za kitaifa zinazoeleweka kuhusiana na mipaka ya kimaeneo ya nchi yetu vyama kama Chadema vimekuja na sera zao za MAJIMBO (kimsingi wako sahihi), kesho kitaibuka chama kingine kitakuja na sera yake tofauti na hii, n.k.

CCM wao wako na sera ya kugawa nchi fasta kadiri inavyowezekana simply kwa kuwa hakuna sera wala taratibu zinazoeleweka zaidi ya Rais kutumia mamlaka yake aliyopewa kikatiba bila kuwa na udhibiti wowote.

DUDUS achana na uvyama hapa jamaa kaomba kuungwa mkono wewe unaanza na sera za vyama. Chadema na CCM vimetoka wapi kwenye maelelzo ya mtoa maada. Majimbo maana yake nini kama siyo bangi na gongo ndo zinakusumbua.
 
... Kuwe na sera ya Kuifuta CCM na matendo maovu yote ya CCM katika Historia ya Nchi hii... Bila kufanya hivyo kunahatari kubwa ya kujenga Taifa lenye kuwashangilia WAHUJUMU uchumi! CCM imesababisha Watanzania kutokuona aibu kwa kushindwa kuwajibika, hawaoni aibu kuomba na kutoa rushwa! Wafanyakazi wengi wako kwenye Salary Maintenance program... Mawaziri wamekuwa makanjanja wa kuuza Mali za Watanzania... Taasisi ya Urais iko holiday toka walipoingia ikulu kazi yao ni Utalii Duniani kote...kila mtu sasa anatamani kuwa mtalii... Sera za nchi zianishe kwa uwazi majukumu na wajibu wa kila Idara na Vitengo nyeti vya nchi hii! Pawepo na Uwajibikaji plus adhabu kali kwa wahujumu Uchumi kama wafanyavyo Wachina!!! Rasilimali Za Watanzania Ziwanufaishe Watanzania kwa 97% kama ambavyo Australia na nchi nyingine wafanyavyo! Mishahara ya Watanzania waliko kwenye MNCs ziendane na za Wazungu ili faida ya uwekezaji ionekane, Marufuku Kuwinda kusafirisha Wanyama wetu! Sekta ya Utalii imilikiwe na Watanzania 100% ... Critical Infrastructures kama Barabara, Ndege, Umeme, Maji, Gesi imilikiwe na serikali 100% ... Tuepuke kununua umeme wa magenerator za Symbion et al... Benki Kuu iache ujinga wa kusimamia "Price Stability" wakati haina udhibiti wa bei ya Mafuta kwenye soko la Dunia! Badala yake ijikite kwenye zile Objectives za Kuwawezesha Wazawa wamiliki Migodi Mikubwa, Viwanda, Mashamba na sekta za Uzalishaji, Sera za IMF/WB haiwezi kutusaidia kamwe...

Kijana una point nzuri sana lakini na wewe unaonekana akili yako iko kisiasa zaidi na ushabiki usiyo kuwa na suruhisho la matatizo tuliyonayo. Naona unajitoa ufahamu kwa kusema sera za IMF/WB haziwezi kutusaidia kwa maana halisi ni kwamba sasa Tanzania ijitoe Umoja wa Mataifa na ianzishe umoja wake binafsi ambao kwa akili ya kawaida ni wa kufikirika
Umesema sekta ya utalii imilikiwe na Watanzania 100%. labda hao watanzania watoke sayari nyingine na hii tunayoishi. Kwasababu mpaka sasa hivi sijamuona mtanzania mwenye uchungu na hii nchi. Tulionao wote ni majingiri tu awe kutoka chama tawala au upinzani. Ruzuku tu wanazopata zinakuwa za kulipana madeni akipewa nchi itakuwaje. Kwahiyo basi hakuna mtanzania mwenye uchungu ukiwemo na wewe.
 
Hitimisho la Ndumbayeye "lakini kuna kitu unacho " linaashiria ameona ilani ya taifa ni zaidi ya sera; sera huwa inakuja baadae kutoa muongozo wa jambo mahususi lililomo ndani ya ilani....jukumu kubwa la ilani ya Taifa ni ku play part kama corner stone ya sera zote za nchi....ndugu Getstart, ilani ya Taifa inasimama kama dira ya Taifa, ni wapi kama watanzania tunataka tujione baada ya miaka mitano. ...inasimama kama benchmark au corner stone ya kupima ufanisi wa utendaji wa chama kitachoshika hatamu....baada ya ilani ya Taifa kutolewa kazi ya vya siasa ni kutengeneza mpango mkakati (unaweza kuziita ilani za vyama) wa utekelezaji wa ILANI YA TAIFA na hata zaidi ya hapo na kazi ya mwananchi ni kupima ni yupi plan yake inatekelezeka na kwa rasilimali zipi alizozipendekeza.....mfano ilani ya Taifa inaweza kusema baada ya kupata maoni ya wengi kipaumbele cha kwanza kiwe elimu na uwekezaji wake uwe 10% ya pato la Taifa....chama A ruksa kuja na mkakati wa kuwekeza 12%, chama B 15 % but si chini ya asilimia 10 iliyowekwa na Watanzania katika ilani ya Taifa ama si ruksa chama Q kuja na kipaumbele cha kununua ndege ya Rais hata kama ni kwa gharama ya watoto kwenda shule....kwa sasa ni rahisi serikali kujigamba imejenga mfano km. 1,000 za lami ambayo haikuwako tukipata uhuru LAKINI hatujiulizi wala kuwakosoa pengine kwa rasilimali zilizopo walipaswa kujenga 2,000. Kasoro hii ingetatuliwa na ILANI ya Taifa!
Pengine tunazungumza kitu kilekile lakini kwa majina tofauti. Ilani za vyama vya siasa kwangu mimi bado ni mpango mkakati wa kutekeleza mambo ambayo kama taifa tumekubaliana tuyatende kufikia au kuleta maendeleo ya nchi (katika seta zote kiuchumi, kijamii na usalama). Hiyo ndiyo ilani. Sasa mambo tunayokubaliana kama taifa kwangu mimi yakiwa katika Katiba, sheria zetu, sera za kitaifa ambazo zinaambatana pia na mipango ya muda mrefu na muda mfupi.

Tatizo letu liko katika mipango yetu ya maendeleo ambayo kwa muda mrefu hatukuwa nayo. Nchi ilikuwa inakwenda kwa bajeti za mwaka mmoja mmoja tu ambazo hazikuoainishwa na mipango ya kitaifa ya muda mrefu wala mfupi. Hata pale tulipotengeneza mpango wetu wa muda mrefu (nafikiri unaitwa 2025) ulibaki katika karatasi tu bila kuoanisha utekelezaji wake na mipango na bajeti za kila mwaka. Bahati mbaya mpango wenyewe ulitengenezwa kichama (ukaingia katika siasa) badala ya kuwa wa kitaifa (unganishi). Na ninaona hata Katiba nayo tunakwenda huko huko. Kwa mabarabara uliyoyataja ni mfano mzuri, yawezekana yako katika mpango wetu wa kitaifa, lakini je mkakati wa utekelezaji wake ni wa ufanisi na unafuata mpango ulio sahihi? Bahati mbaya ujenzi wa barabara umekuwa ni wa kisiasa wa kuvutia kura katika majimbo. Kwa upande wa sera, ni kweli zippo sera zinazotafasiri mpango wa kitaifa tuliokubaliana ili utekelezwe, lakini pia kuna sera ambazo zinaelekeza mwelekeo wa kitaifa ya kisekta au kimaeneo. Yote haya ni lazima yapitishwe kwenye Bunge au mchakato unganishi kukubalika kitaifa. Ukishapitishwa kwa njia hiyo unakuwa wa kitaifa na hakuna chama kinachoweza kuubadilisha bila kupitia njia hiyo hiyo uliopitishwa.

Kama mipango yetu ya muda mrefu ingekuwa ya kitaifa kwa maana ya kutuunganisha na kukubalika na wote, basi ilani za vyama zingekuwa ni utekelezaji huo na wao wanaweka au wanauza mikakati ya utekelezaji na sisi wapiga kura tunachagua mkakati ulio bora.
 
Hitimisho la Ndumbayeye "lakini kuna kitu unacho " linaashiria ameona ilani ya taifa ni zaidi ya sera; sera huwa inakuja baadae kutoa muongozo wa jambo mahususi lililomo ndani ya ilani....j

No thank you! SERA (POLICY) ni malengo ya muda mrefu; ni muongozo wa kitaifa wa jamii nzima (kila mwananchi au taasisi). ILANI (MANIFESTO) ni malengo mahsusi ya muda mfupi hususan kwa ajili ya kushawishi mambo fulani katika jamii aghlabu katika muktadha wa kisiasa.

Kwa mifano niliyotoa kabla; Sera ya Marekani kuhusu ugaidi haitarajiwi kubadilika leo au kesho kwa sababu ni muafaka wa kijamii (ya wamarekani) bali Ilani ya Democrats ya uchaguzi mkuu uliopita (mf. kuhusu ushoga ambao Obama aliupigia sana upatu) sio lazima iwe hiyo hiyo miaka minne baadaye katika uchaguzi utakaofuata.

So, unaweza kuona ILANI ina tabia ya "kusikilizia" jamii inataka nini "wakati huu" then inakuwa fabricated kuendana na mahitaji ya jamii ya muda mfupi bali sera ni kwamba jamii nzima (na sio vyama au taasisi moja moja) ilishaamua tunataka hivi na ni lazima tuende hivi kama taifa/jamii.
 
Ilani ya uchaguzi ni kama mkataba wa ajira cha kushangaza kwa Tanzania mkataba huu unaandikwa na mwajiriwa (mwanasiasa) badala ya mwajiri(mwananchi). Napendekeza tufanye kinyume chake; kila iishapo miaka mitano wananchi ndio tuwaambie wanasiasa nini tunataka atakayeshinda atufanyie na si wao kutuambia tukiwachagua watufanyie nini, jukumu la mwanasiasa wakati wa kujinadi liwe kutueleza ubunifu atakaoutumia na chama chake kutufikisha pale tunapotaka watanzania...

Tume ya taifa ya uchunguzi ikishirikiana na Tume ya mipango ya Taifa ndio tuwape jukumu la kukusanya maoni ya Watanzania ya kwamba wanataka waione nchi yao iko wapi miaka mitano, kumi, kumi na tano, hamsini ijayo kisha maoni hayo yakiratibiwa na wataalam wa mipango (economists) waitafsiri katika ilani ya Taifa ya miaka mitano mitano.

Uzuri na faida za mfumo huu ni zifuatazo:
1. Nchi inapata dira na mwelekeo unaoeleweka na utendaji wa mwanasiasa naopimika (perfomance appraisal)
2. Ilani hii itakuwa ni 'road map' yenye muafaka wa kitaifa katika mgawanyo wa keki ya taifa hivyo kupunguza pengo ukuaji uchumi na punguzo la umaskini
3. Ilani ya Taifa itaongeza ubunifu wa namna ya kutumia rasilimali za taifa kutuletea maendeleo badala ya misaada kutoka nchi za nje.

Ni katika ilani ya Taifa pekee mwananchi anaweza kutoa masharti yafuatayo kwa mwanasiasa:
1. Tunataka Rais ambaye hata siku moja hatatoka nje ya nchi kwenda kuomba msaada kwa nchi tajiri badala yake akatafute masoko, wataalam wa kuwaajiri kwenye vyuo vyetu ili tutransfe teknoloji yao, partner wa maendeleo na sio doner n.k; ukweli ni kwamba hakuna kinachotudidimiza kwa wanasiasa kusaini mikitaba ya kinyonyaji kama misaada, hata ushoga uko njiani kuletwa tuuingize kwenye katiba chanzo ni bakuli la misaada
2. Sharti la kufungua kiwanda kimoja kila mwaka: ajira, soko la mazao yetu litapatikana
3.Sharti la kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi na sekta ya nyumba na makazi; hii itapelekea ongezeko la wawekezaji kwenye sekta ya ujenzi wa makazi bora yaliyopimwa na bei nafuu hivyo mtanzania kupunguza kuugiaugua kwa chanzo cha makazi duni.
4.Sharti la mfumo wa bima ya afya kwa kila mwananchi kuchangia kidogo wakati yuko mzima ili anapougua michango ya wengi imtibu kwa matibabu bora bila kuilazmu serikali kugharamia chochote
5. Sharti la kuwekeza kwenye elimu si chini ya asilimia 10 ya pato la taifa....kwa kufanya hivyo automatically maprofesa hawatakimbilia siasa inayolipa kwa sasa badala yake watasalia kwenye kufanya tafiti na kufundisha watu wetu na wenye digrii watafundisha shule za msingi. ...tofauti na sasa vilaza ndo wanakimbilia ualimu.
6. N.k

Kama wazo hili la ILANI YA TAIFA ni jema naomba tulipigie debe liingie kwenye katiba.

Nawasilisha.

Mkuu tupe mfano wa nchi yoyote duniani inayotumia utaratibu huo ulioubainisha
 
Ndugu yangu Masalapyetwe inaelekea una upogo wa kielimu! UN na IMF/WB ni entity mbili tofauti... over relaying of IMF/WB imeizamisha nchi hii kwenye lindi la umasikini wakati kiuhalisia sisi ni matajiri wakubwa duniani in terms of Natural resources, good climatical condition, vivution vingi na vya kipekee vya utalii duniani... Pengine wewe ni Mzee hujui game la Wazungu ama Game la Kiuchumi linalochezwa na mataifa makubwa duniani... Ruzuku wanazozipata vyama vya siasa ni % ngapi ukilinganisha na ya CCM? Wewe unaona ni sahihi IMF kututungia Sera ya Uwekezaji na Madini yenye kutulazimisha kutokupata hata sent moja kwenye madini yetu? wewe unaona ni sawa kwa BOT kujikita kwenye nadharia ya Price Stability pekee bila kufanya juhudi za maksudi za kuwawezesha Wazawa kumiliki kampuni kubwa kubwa maslahi mapana ya Watanzania? Wewe unaona ni sahihi Watanzania kuwa vibarua kwenye ardhi yao? Mental Slavery imekuganda mkuu... We can do better without WAZUNGU na sera zao....
Kijana una point nzuri sana lakini na wewe unaonekana akili yako iko kisiasa zaidi na ushabiki usiyo kuwa na suruhisho la matatizo tuliyonayo. Naona unajitoa ufahamu kwa kusema sera za IMF/WB haziwezi kutusaidia kwa maana halisi ni kwamba sasa Tanzania ijitoe Umoja wa Mataifa na ianzishe umoja wake binafsi ambao kwa akili ya kawaida ni wa kufikirika
Umesema sekta ya utalii imilikiwe na Watanzania 100%. labda hao watanzania watoke sayari nyingine na hii tunayoishi. Kwasababu mpaka sasa hivi sijamuona mtanzania mwenye uchungu na hii nchi. Tulionao wote ni majingiri tu awe kutoka chama tawala au upinzani. Ruzuku tu wanazopata zinakuwa za kulipana madeni akipewa nchi itakuwaje. Kwahiyo basi hakuna mtanzania mwenye uchungu ukiwemo na wewe.
 
Wazo ni zur tu, lakini tatizo ni wasimamizi wa hiyo ilani na sera zake, utawapata wapi /chama kipi, watu wenye uadilifu, wanaochukia rushwa, wasiopenda kujilimbikizia mali, watenda haki, wasiopenda kutembelea V8, wasiopenda kumiliki magorofa yao binafsi, wasiopenda mikaba yenye kuwanafaisha wenyewe, Kwahiyo tatizo sio ilani wala sera tatizo ni mtimamo wa kijamii katika utendaji wa shughuli za serikali.Mwisho; KATIBA NZURI+ILANI NZURI+SERA NZURI+VYAMA VYA SIASA+WATU AMBAO SI WAADILIFU=SIFURI
 
Ndugu yangu Masalapyetwe inaelekea una upogo wa kielimu! UN na IMF/WB ni entity mbili tofauti... over relaying of IMF/WB imeizamisha nchi hii kwenye lindi la umasikini wakati kiuhalisia sisi ni matajiri wakubwa duniani in terms of Natural resources, good climatical condition, vivution vingi na vya kipekee vya utalii duniani... Pengine wewe ni Mzee hujui game la Wazungu ama Game la Kiuchumi linalochezwa na mataifa makubwa duniani... Ruzuku wanazozipata vyama vya siasa ni % ngapi ukilinganisha na ya CCM? Wewe unaona ni sahihi IMF kututungia Sera ya Uwekezaji na Madini yenye kutulazimisha kutokupata hata sent moja kwenye madini yetu? wewe unaona ni sawa kwa BOT kujikita kwenye nadharia ya Price Stability pekee bila kufanya juhudi za maksudi za kuwawezesha Wazawa kumiliki kampuni kubwa kubwa maslahi mapana ya Watanzania? Wewe unaona ni sahihi Watanzania kuwa vibarua kwenye ardhi yao? Mental Slavery imekuganda mkuu... We can do better without WAZUNGU na sera zao....

Nimegundua nabishana na mtu ambaye akili yake bado iko chooni. una maana gani kusema UN na IMF/WB ni vitu entity mbili tofauti? Chukua akili yako changanya na maji kidogo angalau iweze kumove kwa sababu naona imeganda kweli kweli. Ufahamu wako ni ule wa kukaririshwa na kuambiwa leo kaandike hivi. Unaweza ukadhibitisha bila hofu yoyote kwamba IMF umetutungia sera ya uwekezaji ya madini, na kama unasupporting documents ili kila mtu approve unayosema ni kweli naomba uziweke kama ushahidi wa yale unayoongea hapa jf. Hoja ya wazawa kumiliki makampuni makubwa kama unavyosema ni ndoto ambazo unajaribu kuota ukiwa chooni. Ni wangapi hao watanzania wanaomiliki tukampuni twakawaida lakini bado wameajiri experts (wazungu)? Unavyosema kwamba we can do better without wazungu na sera zao nashindwa kuelewa uwezo wako wa kufikili na kweli wewe ndo umepprove kwamba umekaririshwa na mtu.

Chukua mfano mdogo sana wa hapa Africa, nchi kama South Africa wamefanya vizuri kutoka na sera nzuri zilizoandaliwa na hao wazungu ambao mpaka sasa wanaamini South Africa haipaswi kuwa kwenye hili bara.
 
Pole nimekosea kulumbana na wenye kufagilia sera za USHOGA... Crystal clear elimu yako ni ndogo sana, UPE au NGUMBARO! How come kuna nchi ambazo ni Wanachama wa UN lakini si wanachama wa IMF? Unafikiri kwanini BRIC i.e Brazil, India, Russia, na China wameanzisha Benki yao? kwa kufanya hivyo watakuwa wamejitoa UN? akili yangu na yako ipi iko chooni? Bado hujitambui na hutambui kuwa Organs za UN ziko kwa Maslahi ya Magharibi... WHO ilipo ua maelfu ya Raia kule Haiti kwa kuwaambukiza ugonjwa wa kipindu pindu lengo lao lilikuwa nini? wewe mwenye kuabudu Wazungu tueleze Spread of EBOLA kunakofanywa na Wazungu wako Lengo ni nini? AMNEST Int inayotumika kusambaza silaha kwa waasi barani Africa ni SAWA? Killings of Millions of Palestinians kunako fadhiliwa na USA wewe unaona ni sawa kwa kuwa hawastahili kuishi Duniani? Uvunwaji wa dhahabu, Almasi, Uranium, Nickel na sasa Gas bila mgawo kwa Watanzania wewe unaona ni sawa? Sisi hatutaki kuwa na World Class Facilities? Hatutaki Maendeleo? IMF wanaotaka Uchumi wetu ukuwe kwa 0.01% kwenye vitu huku maendeleo ya watu yaki shrink wewe unaona sawa?... Ushahidi Upi unaoutaka wakati Taarifa za kiuchumi za BOT zote zinategemea Data za IMF?... wameku-brain wash hujielewi hujitambui... Bring on ..lete facts siyo porojo na inferiority kuwa Watanzania hawawezi kumiliki makampuni makubwa!! Wao waliwezaje? Do you think kuna mzungu atawaletea Watanzania Maendeleo? Baraka Obama ulimsikiliza vizuri? aliwaambia kuwa Africa isitegemee kuletewa maendeleo badala yake ijiweke tayari kuwa strategic partners kwenye Maendeleo ya kiuchumi... Otherwise Uzee utakuwa unakusumbua ....
Nimegundua nabishana na mtu ambaye akili yake bado iko chooni. una maana gani kusema UN na IMF/WB ni vitu entity mbili tofauti? Chukua akili yako changanya na maji kidogo angalau iweze kumove kwa sababu naona imeganda kweli kweli. Ufahamu wako ni ule wa kukaririshwa na kuambiwa leo kaandike hivi. Unaweza ukadhibitisha bila hofu yoyote kwamba IMF umetutungia sera ya uwekezaji ya madini, na kama unasupporting documents ili kila mtu approve unayosema ni kweli naomba uziweke kama ushahidi wa yale unayoongea hapa jf. Hoja ya wazawa kumiliki makampuni makubwa kama unavyosema ni ndoto ambazo unajaribu kuota ukiwa chooni. Ni wangapi hao watanzania wanaomiliki tukampuni twakawaida lakini bado wameajiri experts (wazungu)? Unavyosema kwamba we can do better without wazungu na sera zao nashindwa kuelewa uwezo wako wa kufikili na kweli wewe ndo umepprove kwamba umekaririshwa na mtu.

Chukua mfano mdogo sana wa hapa Africa, nchi kama South Africa wamefanya vizuri kutoka na sera nzuri zilizoandaliwa na hao wazungu ambao mpaka sasa wanaamini South Africa haipaswi kuwa kwenye hili bara.
 
Ukifuatilia michango ya wengi utagundua sera, ilani, dira vyote ni mipango....kinachokosekana kwa mtizamo wangu ni majibu ya maswali kama "Ni kwa kiwango gani kilichomo ndani ya mipango yote hiyo kimezingatia maslahi mapana ya mtanzania?", "ni kwa kiwango gani mwananchi aliye mlengwa na mtekelezaji wa mipango hiyo ameshiriki na kuiridhia?", "ni kwa namna gani tunapata mrejesho wa utekelezaji na tunaupimaje utekelezaji huo?"....Jambo moja tu linakosekana katika kupata majibu ya maswali hayo....IT'S POLITICAL WILL.....hoja yangu inajaribu kupendekeza mfumo ambao utamlazimisha aliyeko madarakani kufuata mipango iliyoridhiwa kitaifa kupitia ilani ya Taifa. Mahali pekee pa kuipata hiyo political will ni wakati kabla ya uchaguzi ambapo mwananchi anaweza kuingia MoU na vyama vinavyowania madaraka kuja na mikakati itakayojielekeza kujibu masuala ya msingi yatakayoainishwa na ILANI YA TAIFA....mfano ni katika ilani ya Taifa tunaweza kuweka sharti la makampuni ya uchimbaji gesi kuingia ubia na wazawa ama kujiandikisha DSE na kila mwananchi akashiriki uwekezaji huo kupitia hisa....kwa kutokuwa na nyenzo hii muhimu kumepelekea mpaka leo kutokuwako sera ya uchumi wa gesi na maisha yanaendelea.....kwa kuwako na sharti kama hilo katika ilani ya Taifa kungevifanya vyama vya siasa vinapoleta ilani zao kutopuuzia jambo kama hilo badala yake vingeleta mikakati bora zaidi kufanikisha. Wadau hilo mnalionaje? naamini tunao uwezo mzuri tu wa kufikiria tukaja na majibu na nchi zingine wakaja kujifunza kwetu tumewezaje.
 
Back
Top Bottom