Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,073
- 34,844
Kwenye moja ya safari zangu nilimkuta kijana ( pichani) akitoka shuleni. Kichwani amebeba kifurushi cha unga wa mahindi. Miguuni amevaa makatambuga. Yawezekana kabisa aliambiwa; " Ukitoka shule pitia mashineni". Wengi wetu tumetoka katika mazingira hayo. Na ni wepesi sana wa kusahau tulikotoka.