TTCL yetu iliyokuwa ikihujumiwa sasa imeamka

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
Na Wiseman Ficky

Kwa hili la TTCL naipongeza Serikali.
Kwa ufupi.

Tangu kubinafsishwa kwa TTCL hisa zake 35% zilikiuzwa zikiuzwa kwa mkopo kwa utaratibu mpokezano kwa makampuni tofauti yote yakijitambulisha kama wawekezaji wa TTCL

Mlolongo ulikua mrefu kutoka MSI kwenda celtel international 2005, kutoka celtel international kweda zain ya Kuwait 2008 na kutoka Zain ya Kuwait kwenda Barti Airtel ya India mwaka 2010.

Kampuni ya Barti Airtel ndio walikua mmiliki wa mwisho wa TTCL mpaka pale serikali ilipoamua kurudisha hiza zake zote kwa 100%.

Wawekezaji wote hao hawakuwahi kutoa fedha zozote kwa ajili ya kuiimarisha TTCL kibiashara, celtel, zain airtel walikua wawekezaji na wakati huo huo washindani wa TTCL katika sekta ya mawasiliano nchini.

Kutokana na mgongano huo wa kimaslahi makampuni hayo yalikua kwa muda mrefu yakiihujumu TTCL isweze kuinuka kibiashara.

Ndio sababu kwa miaka yote TTCL ndio ilikua kampuni inayotumia mfumo duni wa mawasiliano ukilinganisha na mitandao mingine huku ikikumbana na vikwazo luluki.

Wakati tigo, Voda na airtel wakitumia mfumo wa Global System for Mobile Communications (GSM) TTCL walikua wakitumia teknolojia ya kizamni ya Code Division Multiple Access (CDMA)

Kwa muda mrefu shirika hili la kizalendo limekua likijikongoja kwa mtindo huo huku ikidaiwa kwamba kwa mikataba waliyoingia na wawekezaji hawa kwamba TTCL haina ruhusa ya kuwa mfumo wa GSM na kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na makubaliano. Ndio maana hawakuwa na 2G,3G, 4G nk

Kulikua na mkataba wa hovyo, viongozi mafisadi wachache wenye kumiliki hisa katika katika kampuni hizi binafsi za simu kwa muda mrefu na kwa makusudi walikua wakilihujumu shirika letu hili kwa mbinu na mikakati ili wao waendelee kuneemeka kwa faida na gawio la hisa zao huko kwenye makampuni binafsi ya simu.

TTCL kwa muda mrefu ilikua na hali mbaya licha ya kwamba hili ndio shirika pekee lenye rasilimali yakiwemo majengo zilizotapakaa karibu nchini pote.

Hivi ni mkoa gani Tanzania utakwenda ukose ofisi au jengo la posta na simu?

Wawekezaji hawa uchwara walikua wakitumia rasilimali za TTCL kuweka bondi kwenye taasisi za fedha kupata mikopo na kuboresha makampuni yao huku yakiicha TTCL ikiwa hoi bin taabani ni aina fulani ufisadi ulioumiza sana Taifa hili.

Kwa rasilimali ilizonazo TTCL kama ingekua huru kibiashara tangu kipindi kile saa hizi ingekua mbali sana na pengine 80% ya watumiaji wa simu tungekua tunatumia mtandao huu.

Sote tunaona baada tu ya serikali kuirudisha TTCL kwa 100% na kuvunja mfumo wa kifisadi ulikokua ukihujumu shirika hili tunashuhudia mabadiliko ya kasi sana kwa shirika letu hili.

Ilianza mawasiliano kwa mfumo GSM, TTCL 4G na hivi majuzi imezinduliwa TTCL pesa.

Hii ni hatua kubwa sana niipongeze menejimenti nzima ya TTCL chini ya mukurugenzi mzalendo

Waziri Waziri Kindamba kwa hatua hizi, ninauona uzalendo wao ninaiona dhamira yao ya dhati kabisa ya kutaka kulifikisha mbali zaidi shirika letu hili kwa moyo wa dhati mimi Mtazania ninawaunga mkono.

Kiukweli mimi nafarijika sana ni jambo la kujivunia mtanzania kutumia mtandao wa nchi yako.Uzalendo ni pamoja na kuthamini vya nchi yako. Nimeanza kutumia huduma zao ni nzuri na zinaridhisha.

Shime watanzania wenzangu tulisapoti shirika hili tutumie huduma zao ili pesa zetu watanzania zibaki Tanzania zihudumie watanzania.

KERO SASA BASI...
Ni muda mrefu kumekua na malalamiko ya kampuni za simu watu kuibiwa Salio,Mb, Huduma mbovu nk basi sasa ifike mwisho kutumia mitandao ya wageni ambao hutengeneza faida nono na kuzipekeleka kwenye nchi zao huku wakituacha na kodi kiduchu zisizokidhi.

Niiombe menejimenti ya TTCL chini ya Waziri K mjipange hasa kutupatia huduma bora kabisa tena kwa gharama nafuu mmeanza vizuri sana kuna mambo machache ya kurekebisha (nitakwambia haya binafsi) ikiwa hivyo watanzania hawatakua na sababu ya kuendelea kutumia gharama kubwa za mawasiano chini ya makampuni mengine watanzania tutakua nanyi bega kwa bega.

#KuwaMzalendo
#RudiNyumbani
#NyumbaniKuzuri

Make TTCL Great Again
 
Nina line za mitandao ya kutosha hapa na sina TTCL. unaweza kudhani labda sio mzalendo..., hapana mimi ni mzalendo..., sasa shida ni nini ?

Nadhani tatizo ni kwamba huduma zao ni mbovu kulinganisha na hao wengine....
 
Nina line za mitandao ya kutosha hapa na sina TTCL..., unaweza kudhani labda sio mzalendo..., hapana mimi ni mzalendo..., sasa shida ni nini ?

Nadhani tatizo ni kwamba huduma zao ni mbovu kulinganisha na hao wengine....
Tafuta laini hautojutia
 
labda kwa Matajiri, ila kwa sisi walalahoi hatutoboi braza
Screenshot_20200804-142049.jpg
 
Nilishakuwa na line ya hawa jamaa kipindi hicho nikitumia banjuka..., nikiwa mbali na town mtandao hakuna...

Now niambie naweza kupata 1 gb kwa wiki kwa buku au 7gb kwa wiki kwa buku tano na mtandao kushika pande nyingi za hiki kijiji....., (kwa taarifa yako hao ni Halotel)
GB 8 kwa wiki kipo kwa bei ya 5000
 
Hawa TTCL watabaki jina tu kama ATCL.
Kama ofisi za serikali zisingelazimishwa kuwa na land line za TTCL kampuni ingekuwa imeshakufa siku nyingi sana.

Kampuni za serikali huwa hazifanyi vizuri.

Bora wangeendelea kuwa na ubia na bhart airtel wale wahindi waliisha kubali kuumia kwa miaka mitano mingine ya Magufuli.

Mwisho mtaiuza kwa reja reja maana mwisho mtabaki na majengo na jina basi.
 
Back
Top Bottom