TTCL Unlimited Download | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TTCL Unlimited Download

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mau, Mar 9, 2012.

 1. Mau

  Mau Senior Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Unlimited downloads Packages[/FONT]

  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #f3f2bc"]
  [TD="class: tabledata, width: 151"]Package Name
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 120"]Max. Download Speed (Kbps)
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 177"]Max. Upload Speed (Kbps)
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 263"]Monthly Price(TZS)
  [/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #fcf8e7"]
  [TD="class: tabledata, width: 151"]Unlimited 256
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 120"]256
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 177"]256
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 263"]45,000.00
  [/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #fcf8e7"]
  [TD="class: tabledata, width: 151"]Unlimited 512
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 120"]512
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 177"]512
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 263"]70,000.00
  [/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #fcf8e7"]
  [TD="class: tabledata, width: 151"]Unlimited 1M
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 120"]1024
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 177"]1024
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 263"]110,000.00
  [/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #fcf8e7"]
  [TD="class: tabledata, width: 151"]Unlimited 2M
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 120"]2048
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 177"]2048
  [/TD]
  [TD="class: tabledata, width: 263"]200,000.00
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Wakuu katika pitapita zangu nimekutana na hizi tarrif za TTCL, hebu ambaye amezitumia atupe maelezo kidogo, zinaonesha ni Unlimited je ninaweza kuzikishea kutwa kucha nikadownload movies za kutosha? mfano nikiwa natumia Unlimited 1M

  Nawasilisha
   
 2. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  TTCL niliwaacha siku nyingi kwa sbb ya ukigeugeu wao. Leo watasema hivi, kesho tena vingine kabisa!
   
 3. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Tatizo langu ni hapo kwenye hizo speed zao, nadhani ni shared, hivo utakuta speed inashuka vibaya mno 1gb ikachukua siku nzima kushuka. Weka link mkuu, maana nimejaribu kufuatilia kwenye website yao sijaona kitu kama hicho!
   
 4. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mimi natumia Moderm ya TTCL na ni excellent ila usitumie hizo hapo juu bali nunua moderm halafu waambie waku connect na huduma ya BANJUKA ambayo ni unlimited kama ifuatavyo:

  saa 12 asub-12 jioni Tshs 1000 kwa saa lakini unlimited
  saa 12jioni hadi saa 3 usiku Tshs 800 kwa saa lakini unlimited
  Saa 3 usiku hadi 12 asubuhi Tshs 500 kwa saa pia ni unlimited

  Kwa hiyo ukiweka shs 1000 na kama kukiwa na speed nzuri unaweza ku download kitu kikubwa sana ila saa ikiisha ukiwa online basi 1000 yako itaisha. Ukimaliza download au kazi yako kabla ya saa moja unaweza kuendelea na salio lako next time.

  Huwa naweka 10,000 na sio rahisi nitumie mfululizo 10hours ila raha yake ni kwamba ukiweka kwa mfano 5000Tshs unaweza kudowload hata 2Gb ya movie au clips within 2-3 hours kutegemea na speed ya mtandao wa TTCL na ukabakiwa na 2000tsh ya kufanya vitu vingine:

  Tahadhari: Unapotumia Banjuka na ukasahau kuondoka online hata kama hufanyi activity yeyote huwa hela yako inaendelea kwisha hivyo ushauri wangu ni ku disconnect moderm mara tu ukimaliza shughuli zako.

  I'm talking from experience na nina moderm karibu zote ila hii kwangu naona inanifaa kwani huwa nami ni downloader mzuri.
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Umehamia wapi kaka?
   
 6. bigboi

  bigboi JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 80
  MIMI LAST MONTH NILIKUWA NATUMIA HIYO UNLIMITED 1M YA LAKI MOJA NA KUMI YAANI KAMA UNATAKA KUJIUNGA ACHA KABISA HIZO SPEED HAPO NI SHARED KWA MFANO UNA DOWNLOAD MOVIE SPEED NI 30Kbps huwezi hata ku stream video youtube unaweza ku save hiyo hela ukajiunga na voda BOMBA 30(NO PROMO) AMBAYO NI 30,000 KWA MWEZI ZILE 2GB ZAO ZIKIISHA UANKUWA SPEED SAWA NA YA TTCL.
   
 7. Mau

  Mau Senior Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapa ndo umenena jambo mkuu kumbe hizo speed zao ni shared, kweli bora nitumia bomba 30 manake Vodacom nikishamaliza hizo 2GB zao nina uhakika wa kushuga movie moja kila siku ya 700MB kwa hiyo speed yao ndogo thanks mkuu
   
 8. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu achana nao hao,utaibiwa bure. Nina zaidi ya mwezi sasa tangu ninunue modem yao, nikawaomba waniconnect kwenye BANJUKA, lakini nilichokikuta ni wizi mtupu. Speed yake ilikuwa ndogo sana, inashindwa hata kustream video za youtube. Kiukweli nilishindwa kutimiza lengo nililokuwa nimekusudia.Ni kweli wameandika speed nzuri tu hapo, ila ukikosea ukajiunga tu ndio utagundua wizi wao ni unlimited!
   
 9. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mi natumia broadband spidi yake ni soo na inamaliza mb balaa asbh hadi jioni mb 700 sijadownload kabisa wanatishaa
   
 10. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  BB umechukua pakeji ya ngapi kaka?
   
 11. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,767
  Likes Received: 7,072
  Trophy Points: 280
  kama mtu una hela laki 1 kwa mwez ya net why usivute wireless yako? Sifahamu kwa dar lakini tanga i know kueka wireless kwa first time dola 300 then kila mwez dola 60 unlimited speed average 120kbps then hii unaweza share na jirani mukalipa 30 kila mtu
   
 12. D

  Dedii Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  unavuta toka kwa nani?
   
 13. i411

  i411 JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Nazani anaongelea RAHA.COM ni noooomaa hawa jamaa na speed yao ya wireless internet hakuna kubabaisha nenda kwenye site yao Raha utapata data zote huko jinsi ya kujiunga. Kitu ambacho siwapendei wanatumia tuu dolazzzzi
   
 14. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Subiri kaka, bado haujaeleweka, njoo tena! Kuvuta wireless kivipi, kutoka kwa provider gani anayekupa donspeed ya 120Kbps kwa dola 60? Tujuzane wakuuu, wengine tunalipa zaidi ya laki 6 kila mwezi kwa huduma za internet pekeee!!!!!!!
   
 15. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,767
  Likes Received: 7,072
  Trophy Points: 280
  mimi kwetu sio dar so sifahamu kama hawa provider wapo dar au vp.
  Jina lao wanaitwa hotnet
  wanakuekea kidishi kile kidogo kimekaa kama antena flani hivi
   
 16. a

  alikhalef JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 707
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  jamani musisumbuke njooni muchukuwe line za tigo. unlimited
   
 17. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #17
  Mar 11, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,767
  Likes Received: 7,072
  Trophy Points: 280
  ni risk hizo line utatoa waraanty? Mi niliwahi kuuza ila unaishia kugombana na watu nyengine zinakaa wiki nyengine hadi miez 3 hazielewek
   
 18. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Dah, kaka mnafaidi maisha!
   
 19. Akthoo

  Akthoo JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 584
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  NEW TARIFF IN TTCL BROADBAND

  Napenda kuwafahamisha kua TTCL imefanya marekebisho ya huduma zake za broadband zisizo na kikomo (unlimited packages) katika maeneo yaliyotajwa hapo chini. Promotion hii inajulikana kama NDUKI PROMOTION. Katika promotion hii neno NDUKI limetumika ili kumaanisha kitu chenye KASI kubwa kuliko vingine, kwa mfano mchezaji wa mpira wa miguu akipiga shuti lenye kasi kubwa inajulikana kwa lugha ya kimpira kua amepiga NDUKI kubwa, mwanariadha akikimbia kwa kasi kubwa pia inajulikana kama mkimbiaji huyo hua anatoka NDUKI.

  Faida za NDUKI BROADBAND:

  Miongoni mwa faida za NDUKI BROADBAND ni kama ifuatavyo:


  • Kumekua na ongezeko la kasi (speed)
  • Kumekua na punguzo kubwa labei (kwa mwezi)
  • Mfumo wa kulipia umebadlika kutoka mwezi kwa mwezi (kalenda month) kua siku 30 toka mteja aongeze salio.
  • Mteja anapata connection kwa siku thelathini (30) toka siku aliyoongeza salio.


  Vifurushi:

  Huduma hii imegawanywa katika vifurushi mbalimbali kulingana na mahitaji na ladha (demand and taste) ya wateja wetu kama ifuatavyo:


  1. 256 kbps – NDUKI Bronze (30,000/-)
  2. 512 kbps – NDUKI Silver (60,000/-)
  3. 1Mbps – NDUKI Gold (100,000/-)
  4. 2Mbps – NDUKI Diamond (200,000 )

  Lengo la internet isiyo na kikomo

  1. Kumwezesha mteja kutumia internet yake kwa siku thelathini (30) bila kukatika
  2. Kumwongezea mteja hali ya kutumia na kuridhika
  3. Kuongeza kasi ya internet
  4. Kuwavuta wateja wengi wadowadogo na wa majumbani


  Faida kwa wateja


  1. Intaneti ya bei nafuu kuliko zote Tanzania. Vifurushi vya gharama ya chini kwa mwezi mzima.


  1. Wigo mpana zaidi wa uchaguzi wa vifurushi vya mwezi (siku 30) kulingana na mahitaji ya mteja
  2. Huduma ya Intaneti yenye ubora na ufanisi wa hali ya juu
   1. Kasi ya ajabu
   2. Intaneti ya uhakika
   3. Kupakua (download) taarifa kwa muda mfupi


  1. Intaneti isiyo na kipimo cha matumizi kwa bei ile ile kwa mwezi mzima (siku 30)


  1. Waweza kuongeza muda wa matumizi ya siku 30 wakati wowote.


  1. Husaidia kupanga bajeti ya matumizi ya intaneti kwa mwezi.


  Vipengere muhimu kwa mteja:


  1. NDUKI BROADBAND haina KIKOMO CHA MATUMIZI.
  2. NDUKI BROADBAND ina KASI KUBWA kuliko internet zote nchini
  3. BEI ya NDUKI BROADBAND kwa mwezi imepunguzwa
  NDUKI BROADBAND ndio internet yenye UHAKIKA wa kumwacha mteja akiwa ameungainishwa kwa mwezi mzima (siku 30).
   
 20. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi modem yangu iliyokuwa imeunganishwa na BANJUKA hata sikumbuki nimeiweka wapi.
  Nadhani ungetuambia namna gani mtu anaweza ku activate. Kwa mfano kwa wale tuliokuwa kwenye promo ya BANJUKA tutaweza vipi kujiunga na hiyo NDUKI. Jitahidi siku nyingine usituwekee hapa taarifa nusu nusu.
   
Loading...