TTCL tumerudi Nyumbani tufungulieni Milango basi!!

TTCL tumerudi Nyumbani tufungulieni Milango basi!!

Kwa nini watanzania hao hao wakiwa kwenye sekta binafsi wana perform kuliko wakiwa serikalini? Shida ni nini hasa?
Tatizo kubwa ni milolongo mirefu ya maamuzi serkalini. Ukiwa serikalini hata kununua karatasi tu kuna mchakato wa kutisha, mafaili yanatembea kwa watu kibao. Pia tatizo lingine ni kuwa serikali ukiwa mbunifu au mchapakazi sana hakuna anayekutambua au hata kuthamini juhudi zako, mwisho wa siku wote mnakula ongezeko moja la mshahara na ikiwezekana mwenzako mzembe mzembe tu anapanda cheo kwa kufaamiana na watu huko juu. Mwisho wa siku kila mtu anafanya kazi kwa average performance
 
Duh, yaani ukiweka line nyingine ndo ushawapoteza! Yawezekana ndo sababu wanapanga eti watengeze simu za TTCL tu.
Kama umewahi kutumia mtandao wao utakubaliana na mimi kuwa wapo vizuri hasa kwenye network ya internet.

Tatizo lao coverage yao ni katikati ya mji tu, hawajasambaa kabisa. Ukitoka hapa kwenda moshi, by the time unafika chalinze unawaaga. Pia hawana network ya 2G, sasa nashindwa kuelewa wale wa vijijini watapataje pesa kwa hiyo T-Pesa? Hawapo serious kabisa!!!
 
Kiukweli nimekubali kuwa mzalendo na kurudi nyumbani ila sasa milango yenu bado umefungwa, kwa nini hamtaki kutufungulia Milango wakati Mmetuita wenyewe?

1. Nilirudi nyumbani pale arusha mjini na mambo yalikuwa poa sana tena nikapewa chakula kitamu cha 4G na mboga za kutosha yaani bundle za maana, kwakuwa natumia line ya chuo nikasema isiwe tabu ngoja nikale na masela wangu.

2. Nikatoka mjini kwenda tu USA river sikuamini macho yangu, nyumba ya Tengeru imefungwa, nyumba ya USA ndio hata kuruka ukuta huwezi, nikaona isiwe tabu, nikaja kwa Mromboo, nako hivyo hivyo, Unga limited nako hivyo hivyo, njiro nako hivyo hivyo dah nikachoka....

3. Kazi yangu ikaisha nikapanda bus, njia nzima toka Arusha mpaka Mwanza hakuna hata nyumba ya kuchimba dawa zote zimefungwa, labda mpaka ukifika stand kuu za mikoa, toka Mwanza kuja Mkoani kwangu ndio hata Nyumba ya kupata chakula cha mchana aipo kabisaaa....

4. Nimerudi wilayani kwangu uku Mkoa mmoja karibia na Burundi, hata kipeperushi cha Rudi nyumbani kumenoga sikioni, zaidi zaidi najifariji na tangazo la kwenye Azam Tv tu.

5. Hivi kwa style hii TTCL mtatushawishi turudi nyumbani, kama nyote mmeamua kuishi mjini tu, nyumba za pembeni mwa mji mmezifunga, au mnategemea wote tuhamie mjini kwenye nyumba moja, tutatosha kweli.

6. Hapa nipo Wilayani na Line yangu kwenye wallet, hata sijui nitarudi lini mjini ili nikafaidi TTCL, kiukweli ampo makini au mna kasi ya konokono, sidhani kama mna wilaya hata moja ya mikoani ambayo mmefika.

7. Mnashindwa na Halotel kampuni ya juzi? Wapo mpaka uku ndani kabisa kijijini kwetu tena tunapata H+, hacheni utani jipangeni

8. Nyumba yenu ya hapa wilayani imefungwa, mimi nipo nje hapa nasubiria mnifungulie, kwa kifupi siwezi kuwaangusha, nimeamua kurudi nyumbani ila mlango bado ina kufuli la chuma SOLEX

9. Tena hapa kwetu kuna mashirika mengi ya wakimbizi, mnaweza hata kujenga nyumba nyingine ikajaa wateja tena wateja wanaolipa kwa fedha za kigeni,

10. Fanyeni haraka mimi nipo hapa mlangoni la sivyo nitalala nje ya nyumba mpaka mtakapokuja kunifungulia, mmeniita wenyewe Nirudi nyumbani, kwanini hamfungui milango hasa nyumba zenu za wilayani? Tupeni taarifa ni Nyumba zipi zipo wazi za wilayani ili tusije lala nje tukienda uko.

RUDI NYUMBANI KUMENOGA
Nimeupenda sana utaratibu wa uwasilishaji. Naamini wamekusikia. Wafuate nyayo za HALOTEL, walianza kufungua milango ya nyumba za vijijini kabisa walivyotokea mjini wala hawakupata tabu ya kujitangaza, kazi hyo tuliifanya ssi wateja.

[HASHTAG]#NYUMBANI[/HASHTAG] KUTANOGA MILANGO IKIWA WAZI.
 
Alafu akija CEO wa kenya mnamkataa eti ni mgeni mnasahau kwamba ana ujuzi wa kutosha. Huyo CEO wenu Omari Nundu ana matatizo gani?

ccm NI janga kama ilivyo UKIMWI wakiingia mahali wanakudhoofisha mpaka unakuwa kirusi.
Nisaidie kushangaa!! Watanzania tumekuwa watu tunaoshindwa kabisa kuzijua na kuzikubali weaknesses zetu, sasa sijui tutajirekebishaje.
 
Tatizo kubwa la TTCL ni Quality of Service. Nafikiri Dr. Kamugisha alikuwa ameanza vizuri kurekebisha hali hiyo. Ni vema Mh. Kindamba akaendeleza Ile mikakati ya Dr kwani amekulia pale pale TTCL.
 
Si hayo tu Mimi nimeomba waje wanifungie huduma ya internet kwenye ofisi yangu, nimepeleka barua ya maombi kwenye ofisi yao iliyopo morogoro town sasa yapata mwezi sijawaona wakija hata kufanya savey ya eneo.Hawa watu bado sana ndio maana tunaenda kwenye mashirika binafsi
 
Serikali bado haijawekeza pesa zakutosha kwenye hili shirika zinatakiwa trilion si bilion mf halotel 3g yao nimpaka vijijini kutokana na pesa wazowekeza 2. uongozi md anatakiwa mtu kama lan ferao au kama kuna mtz aliwahi kuongoza shirika la mawasiliano kwa mafanikio apewe hiyo nafasi.
 
TTCL ni yetu ila hata ukiingia msalani unakuwa offline! Tatizo nini hasa? Nimerudi nyumbani ila wenyeji wananikimbia
They are not serious. Yes thats the truth.
I have been saying that the problem with ttcl is a technical based and marketing based.
You cant do a very good marketing job and then you provide poor service.

If They want to win they will have to invest more in telecommunication infrastructures, and good marketing.
Otherwise kampuni itaendelea kuzama.
 
Si hayo tu Mimi nimeomba waje wanifungie huduma ya internet kwenye ofisi yangu, nimepeleka barua ya maombi kwenye ofisi yao iliyopo morogoro town sasa yapata mwezi sijawaona wakija hata kufanya savey ya eneo.Hawa watu bado sana ndio maana tunaenda kwenye mashirika binafsi
Jaribu ISP wanaitwa habari node. Trust me hautajutia. This guys wana service nzuri ya internet, na bei nafuu kabisa.
 
Wakuu yajayo katika hili shirika yanafurahisha sana. Wengi hawaifuatilii hili shirika vzr. Mwaka moja au miwili nyuma ndiyo wametoka kuwalipa waliokuwa wabia na kuwa ya umma 100%. Kwasasa wanafanya mabadiliko ya ndani ( structuring) lakini wanaendelea kuboresha huduma ikiwemo kuongeza minara. TTCL pesa imeweza kuunganishwa na mitandao mingine kama tigo pesa , M -pesa na airtel money. Kuna jamaa yangu yuko huko anasema wanataka kufanya kitu kinaitwa roaming ( cjui kama nimepatia) na airtel kwahiyo penye airtel patakuwa na TTCL pia. Lakini kusema kweli bado wana safari ndefu tena inayohitaji hela nyingi sana. Watu wanasema hallotel imeanza juzi juzi tu inazidi TTCL. Shida si kuanza juzi, shida ni uwekezaji, hao hallotel wamefanya uwekezaji mkubwa sana. Ukiwa na pesa kila kitu kinakwenda vzr. Mimi kama mzalendo nashauri ttcl wafanye haya.
1. Waongeze minara tena yenye nguvu. Ukiwa wilaya kama tarime unapata signal ya safaricom iliyoko kisumu kilomita kibao kutoka tarime . Ila bonge mnara uko kimara mtu wa tabata hapati signal.
2. Waimarishe kitengo cha mafundi, wawe na vijana wenye uwezo , speed na hari ya kazi. Vijana flexible and capable siyo wazee wanaoshindwa kurespond kwa haraka.
3. Wawalipe wazee ambao wameanza toka enzi ya posta na simu waondoke au wahamishiwe huko serikali. Wazee wako wengi sana TTCL kunzia makao makuu hadi mikoani. Wazee hawa nadhani kwasasa hawana morali ya kazi, ubunifu , speed and flexibility hizi nafasi wapewe vijana.
4. Waanzishe 2g, na 3g ili wawafikie watanzania wengi zaidi.
5. Waongee na voda, tigo, airtel na hallotel fanye hiyo roaming ili penye mitandao hiyo TTCL pia ipatikane.
6. Sheria za manunuzi ziangaliwe upya hasa kwa hizi public organizations zinazofanya biashara. Yaani kuweka taratibu za manunuzi sawa kwa service na business organizations si sawa.

ILA YAJAYO YANAFURAHISHA TUWAPE MUDA NA WAO PIA WATUMIE MAONI YA WADAU KUBORESHA HUDUMA.
 
Tatizo kubwa ni milolongo mirefu ya maamuzi serkalini. Ukiwa serikalini hata kununua karatasi tu kuna mchakato wa kutisha, mafaili yanatembea kwa watu kibao. Pia tatizo lingine ni kuwa serikali ukiwa mbunifu au mchapakazi sana hakuna anayekutambua au hata kuthamini juhudi zako, mwisho wa siku wote mnakula ongezeko moja la mshahara na ikiwezekana mwenzako mzembe mzembe tu anapanda cheo kwa kufaamiana na watu huko juu. Mwisho wa siku kila mtu anafanya kazi kwa average performance

Hilo ni kweli kabisa mafaili aka madokezo yasiyo na maana
 
MTAZAMO WANGU
1. TTCL walitarget zaidi kupata DATA customers na kusahau kwamba asilimia kubwa ya wanaotumia mitandao wanatumia voice na sms. Hapo lazima waje na solution ya maana ikiwamo kuwa na simu ambazo zinaweza hata kusapoti GSM network mode na sio 3G pekee.
2.Wafanye matangazo ya kutosha kuhusu huduma zao na hasa T-PESA ili wajulikane
3.Waboreshe na kusimika minara imara na yenye nguvu kutoa signals na pia mawasiliano yawe ya uhakika.
 
Pia nashindwa kuelewa kwa nini hawa TTCL wame-opt 3G na 4G wakaacha 2G, hadi sasa sielewi sababu za msingi za wao kutokuwa na 2nd generation. Simu ndogo huwezi access mtandao wao, ukibadilisha settings za network kwenye simu yako na kuweka line nyingine kutumia 4G Ile ya TTCL inakuwa kasha haina network.

Mkurugenzi wa TTCL ajitathmini coz hicho walichoamua hawatawafikia watu wa vijijini, lakini pia watalazimika kufunga 3G network systems nchi nzima(which is costly).
Natumia TTCL hiko ndicho ninacho kiona kwenye simu yangu aina ya CX air techno nikaisi labda haina ya simu
 
TTCL ni yetu ila hata ukiingia msalani unakuwa offline! Tatizo nini hasa? Nimerudi nyumbani ila wenyeji wananikimbia
Walikuwa wanatest Maiki{Mike} hawana uwezo wa kushindana na Tigo na Voda com
To be honest hawana uwezo wa kushindana na makampuni ya wazungu
 
Back
Top Bottom