TTCL tumerudi Nyumbani tufungulieni Milango basi!!

TTCL tumerudi Nyumbani tufungulieni Milango basi!!

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
3,547
Reaction score
2,194
Kiukweli nimekubali kuwa mzalendo na kurudi nyumbani ila sasa milango yenu bado umefungwa, kwa nini hamtaki kutufungulia Milango wakati Mmetuita wenyewe?

1. Nilirudi nyumbani pale arusha mjini na mambo yalikuwa poa sana tena nikapewa chakula kitamu cha 4G na mboga za kutosha yaani bundle za maana, kwakuwa natumia line ya chuo nikasema isiwe tabu ngoja nikale na masela wangu.

2. Nikatoka mjini kwenda tu USA river sikuamini macho yangu, nyumba ya Tengeru imefungwa, nyumba ya USA ndio hata kuruka ukuta huwezi, nikaona isiwe tabu, nikaja kwa Mromboo, nako hivyo hivyo, Unga limited nako hivyo hivyo, njiro nako hivyo hivyo dah nikachoka....

3. Kazi yangu ikaisha nikapanda bus, njia nzima toka Arusha mpaka Mwanza hakuna hata nyumba ya kuchimba dawa zote zimefungwa, labda mpaka ukifika stand kuu za mikoa, toka Mwanza kuja Mkoani kwangu ndio hata Nyumba ya kupata chakula cha mchana aipo kabisaaa....

4. Nimerudi wilayani kwangu uku Mkoa mmoja karibia na Burundi, hata kipeperushi cha Rudi nyumbani kumenoga sikioni, zaidi zaidi najifariji na tangazo la kwenye Azam Tv tu.

5. Hivi kwa style hii TTCL mtatushawishi turudi nyumbani, kama nyote mmeamua kuishi mjini tu, nyumba za pembeni mwa mji mmezifunga, au mnategemea wote tuhamie mjini kwenye nyumba moja, tutatosha kweli.

6. Hapa nipo Wilayani na Line yangu kwenye wallet, hata sijui nitarudi lini mjini ili nikafaidi TTCL, kiukweli ampo makini au mna kasi ya konokono, sidhani kama mna wilaya hata moja ya mikoani ambayo mmefika.

7. Mnashindwa na Halotel kampuni ya juzi? Wapo mpaka uku ndani kabisa kijijini kwetu tena tunapata H+, hacheni utani jipangeni

8. Nyumba yenu ya hapa wilayani imefungwa, mimi nipo nje hapa nasubiria mnifungulie, kwa kifupi siwezi kuwaangusha, nimeamua kurudi nyumbani ila mlango bado ina kufuli la chuma SOLEX

9. Tena hapa kwetu kuna mashirika mengi ya wakimbizi, mnaweza hata kujenga nyumba nyingine ikajaa wateja tena wateja wanaolipa kwa fedha za kigeni,

10. Fanyeni haraka mimi nipo hapa mlangoni la sivyo nitalala nje ya nyumba mpaka mtakapokuja kunifungulia, mmeniita wenyewe Nirudi nyumbani, kwanini hamfungui milango hasa nyumba zenu za wilayani? Tupeni taarifa ni Nyumba zipi zipo wazi za wilayani ili tusije lala nje tukienda uko.

RUDI NYUMBANI KUMENOGA
 
Mimi binafsi nilisha fikia hitimisho kua hakuna shirika la umma linaloweza kufanya biashara, serikali ibakie na mashirika yanayotoa huduma kwa jamii (pasi na lengo la kuingiza faida). Mengine wayauze tu maana kwa uzoefu wa zaidi ya miaka 40 imethibitika pasi na shaka yoyote kua biashara haifanywi na serikali ikafanikiwa. Serikali ijikite kwenye kukusanya kodi, kutengeneza mazingira mazuri kwa sekta binafsi
 
Pia nashindwa kuelewa kwa nini hawa TTCL wame-opt 3G na 4G wakaacha 2G, hadi sasa sielewi sababu za msingi za wao kutokuwa na 2nd generation. Simu ndogo huwezi access mtandao wao, ukibadilisha settings za network kwenye simu yako na kuweka line nyingine kutumia 4G Ile ya TTCL inakuwa kasha haina network.

Mkurugenzi wa TTCL ajitathmini coz hicho walichoamua hawatawafikia watu wa vijijini, lakini pia watalazimika kufunga 3G network systems nchi nzima(which is costly).
 
Alafu akija CEO wa kenya mnamkataa eti ni mgeni mnasahau kwamba ana ujuzi wa kutosha. Huyo CEO wenu Omari Nundu ana matatizo gani?

ccm NI janga kama ilivyo UKIMWI wakiingia mahali wanakudhoofisha mpaka unakuwa kirusi.
CEO wa TTCL ni Shushushu Waziri Kindamba! Omary Nundu ni mwenyekiti wa bodi ya TTCL
 
Huu mtandao kwa kweli ni shida yaaani unazidiwa hata ns tigo......toka juzi internet hakuna ukiwapigia wanasema wana tatizo la mtandao...
 
TTCL ni yetu ila hata ukiingia msalani unakuwa offline! Tatizo nini hasa? Nimerudi nyumbani ila wenyeji wananikimbia
Ukisikia kocha ka-bet ndo hiyo, haiingii akilini mitandao inayochukulia kwao internet ni stable kuliko wao wanaoitoa. Nafikiri kuna kuripua flani wanafanya.
 
Mimi binafsi nilisha fikia hitimisho kua hakuna shirika la umma linaloweza kufanya biashara, serikali ibakie na mashirika yanayotoa huduma kwa jamii (pasi na lengo la kuingiza faida). Mengine wayauze tu maana kwa uzoefu wa zaidi ya miaka 40 imethibitika pasi na shaka yoyote kua biashara haifanywi na serikali ikafanikiwa. Serikali ijikite kwenye kukusanya kodi, kutengeneza mazingira mazuri kwa sekta binafsi
Kwa nini watanzania hao hao wakiwa kwenye sekta binafsi wana perform kuliko wakiwa serikalini? Shida ni nini hasa?
 
Utumie ushushushu wake kuboresha kampuni. Tatizo mipango mikubwa utekelezaji kisoda.
Anaweza kuja na plan nzuri sana,but akaangushwa na jiwe,kumbuka kuna kipindi walileta usanii kwenye company ya Airtel,kwamba ni mali ya Serikali na inabidi iwe chini ya TCCL kina Kindamba na Mpango,wakaja mbele ya makamera kutuaminisha watanzania! Mwisho wa siku hakuna any feedback
 
Pia nashindwa kuelewa kwa nini hawa TTCL wame-opt 3G na 4G wakaacha 2G, hadi sasa sielewi sababu za msingi za wao kutokuwa na 2nd generation. Simu ndogo huwezi access mtandao wao, ukibadilisha settings za network kwenye simu yako na kuweka line nyingine kutumia 4G Ile ya TTCL inakuwa kasha haina network.

Mkurugenzi wa TTCL ajitathmini coz hicho walichoamua hawatawafikia watu wa vijijini, lakini pia watalazimika kufunga 3G network systems nchi nzima(which is costly).
Duh, yaani ukiweka line nyingine ndo ushawapoteza! Yawezekana ndo sababu wanapanga eti watengeze simu za TTCL tu.
 
TTCL ni kundi moja na TBC uzalendo umenishinda sijishughulishi hata kidogo kuwa nao wao wapo busy kutangaza huduma zao huku hawajajipanga kufanya biashara na kutaka tupate huduma kwa kigezo cha uzalendo hapana...hao TBC ndio kabisa vipindi vingi vya hovyo hovyo hata kutangaza natural resource tulizonazo ambazo hazitambuliki wao hapana kila kukicha na maharusi...
 
Back
Top Bottom