Ttcl napo panahitaji mtu kama prof. Muhongo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ttcl napo panahitaji mtu kama prof. Muhongo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zacha, Aug 20, 2012.

 1. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 487
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 60
  Shirika hili la umma limekuja kwa kasi kubwa sana kipindi fulani kwa huduma hii ya broadband lakini kadri siku zinavyodhidi kwenda shirika hili linakosa mvuto kwa wateja wake wengi ambao liliwapata katika miaka ya 2008-20011 na mwanzoni mwa 20012. Kwa upeo wangu na data Fulani kutoka ndani ya shirika hilo ni kwamba kuna uozo mkubwa sana kama ule uliokuwa pale Tanesco kabla ya ujio wa Prof Mhongo.
  Shirika hili limekuwa likihujumiwa na baadhi ya watu Fulani ambao wako pale ndani ya shirika na watu hawa inaonekana hawataki kabisa hili shirika liendelee kutoa huduma hiyo ya data (internet) kwa kuwa wao wana hisa katika baadhi ya makampuni binafsi yanayotoa huduma sawa na ttcl kwa vile wanafahamu dhahiri kuwa huduma za ttcl ni nafuu na mtu wa kawaida anaweza kuzimudu katika shughuli zake za kutumia mtandao au biashara.
  Hujuma hizi zimekuwa zikifanywa na watu hawa kupitia kwa mafundi mbalimbali ndani ya shirika kwa kukata baadhi ya nyaya sehemu Fulani au kuiba (switch) na kukwamisha kutoa maamuzi juu ya kutengeneza baadhi ya matatizo yanayotokea kwa wateja wake sehemu Fulani, ambavyo hili suala limewafanya wateja wengi sana kulikimbia shirika hili na kwenda kwenye makampuni ya hao “mabwana maslahi”
  CABLE, DP na CAB nyingi za shirika hili zimechakaa sana mpaka kushindwa upitishwaji wa data kuwa mbovu mno, na hiyo idara ya Technical imeshindwa kabisa kufanya kazi yake kutokana na baadhi ya mafundi kuwa wazito sana na wengine wana diriki kusema kuwa wanasikiliza kauli za juu ambazo ni za hao mabwana tumbo!
  Vile vile hawa watu wamekuwa ni vikwazo pale shirika linapokuwa linataka kuomba mkopo katika bank mbali mbali hapa nchini au nje na kama shirika linahitaji kuomba serikali iwe mdhamini ili kupata hiyo mikopo hawa watu wamekuwa wakizuia kwa maslahi yao wanayo yajua wao!
  Hitimisho, Namwomba sana mhusika anaehuska na uteuzi wa viongozi wa juu wa shirika hili aupitie upya ili kulisaidia shirika hili maana linako elekea ni kuanguka,
  Idara ya huduma kwa wateja hasa ya wale mafundi ni kichefu chefu mtu anaingia ofisini saa sita mchana na saa kumi kamili jioni anaondoka, shirika limegeuzwa shamba la bibi, mi naona niishie hapa, kama una madudu mengine we mwaga hapa usiogope.
  TTCL KIVUENI HICHO KIATU NA MBORESHE HUDUMA KWA WATEJA WENU WA DATA NA UZALENDO UZINGATIWE.
   
 2. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,094
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  ungewataja hao ambao wana hisa kwenye mashirika binafsi ili tupate pa kuanzia
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,686
  Trophy Points: 280
  Kiongozi namba moja wa ujangili TTCL ni mama mmoja senior, ntamtaja baadae....
   
 4. aye

  aye JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,987
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  dah uyu mama ameitaduna hasa nlisikia anaondoka sa sjui tayari kusema kweli management inalimalizashirika hasa sjui kwanini hatua hazichukuliwi kukinusuru
   
 5. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wauaji wa Tanzania ni watanzania wenyewe, siamini kwamba viongozi wa juu hawafahamu kuhusu hili sasa ni hatua gani zimeshachukuliwa baada ya taarifa hizi ambazo kwa kweli sio ngeni miongoni mwa wengi wanaofuatilia mali za nchi hii.

  Tatizo tulilonalo ni kwamba hatujui hata wapi pa kuanzia ukizingatia kwamba hakuna wa kumuamini hata mmoja, tuna aina ya viongozi ambao hawana maamuzi na hii ni hatari kuliko maelezo yoyote ambayo naweza kuyapata kutokana na utaalamu mdogo wa lugha nilionao!
   
Loading...