TTCL inafanya nini kushindana sokoni?

TTCL inafanya nini kushindana sokoni?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638
Licha ya kwamba TTCL imepiga hatua kidogo bado menejimenti ya kampuni hiyo watakuwa na kibarua kigumu katika kukuza idadi ya watumiaji wa huduma mbalimbali za simu zikiwemo intaneti, huduma za kifedha na sauti baada ya kampuni kubwa tatu za Vodacom, Tigo na Airtel kuchukua sehemu kubwa ya soko.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema kuwa wanaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali kuikuza kampuni hiyo ikiwemo kusogeza huduma kwa wananchi na kuongeza uwekezaji wa teknolojia, matangazo na utendaji wa ndani ili kuwafikia watu wengi hasa vijijini.

“Tumejitahidi kwenda kwa wananchi na kujitangaza mkoa kwa mkoa tukawaeleza faida za kutumia huduma za TTCL,” amesema Kindamba.
Juni 2016, TTCL ilipata nguvu zaidi baada ya kampuni ya Bharti Airtel ya India kuingia makubaliano na Serikali ya kuachia hisa zao za asilimia 35 walizokuwa wakimiliki katika kampuni hiyo na imilikiwe na Serikali kwa asilimia 100.

Hata hivyo, Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi amesema wameelekeza nguvu katika uwekezaji wa kituo cha data na kutumia vizuri fursa ya kuunganisha wizara na taasisi za Serikali na usimamizi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ( NICTBB ) ili kuendelea kutoa ushindani kwa kampuni zingine.

“Kwa fursa hizi zinatupa nafasi ya kuongoza katika soko kwa maana ya viwango, gharama vyote tukiweka vizuri inaonyesha kabisa tuna nafasi ya kukua kwa haraka kwenda kutoa ushindani,” amesema Mushi.

Januari 2018 TTCL ilitoa gawio la Sh1.5 bilioni kwa Serikali baada ya kupata faida ya Sh28.5 bilioni mwaka 2017.
 
Tangu walipotoa bundle lao la usiku na kupunguza baadhi ya vifurushi vya Data nimewavua nyota zote na sidhani kama nitawaamini, nilijua watakuwa mbadala wa halotel kumbe ndio kabisa
Jaribu kifurushi cha BANDIKA BANDUA cha GB 4 kipo poa sana.
 
Back
Top Bottom