TTB yajitosa Ligi Kuu ya England

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,920
31,150
• Utitiri wa Mali Asili za Tanzania kutangazwa viwanja sita



WIZARA ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Taasisi za Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), TANAPA na Hifadhi ya Ngorongoro, zimeingia mkataba wa sh mil. 800 kutangaza vivutio vya utalii kupitia udhamini katika mechi 114 za Ligi Kuu ya England kwa msimu huu wa 2010/11. Mkataba huo ni sehemu ya mikakati ya Tanzania kutumia michezo kutangaza vivutio vya utalii kote duniani ambapo kwa Afrika, Tanzania ni ya kwanza kutumia aina hiyo ya uhamasishaji katika utalii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusu mkataba huo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Aloyce Nzuki, alisema wameingia mkataba na Kampuni ya Uwakala ya Lantech Services Ltd ambapo viwanja timu sita vya ligi hiyo, vitahusika kurusha matangazo ya vivutio vya utalii vya Tanzania.
Alizitaja timu zitakazohusika kurusha matangazo hayo chini ya uwakala wa kampuni hiyo ni Blackburn Rovers, Newcastle Utd, Stoke City,
Sunderland, West Brom na Wolves.
Alisema, kampeni kuu tatu za uhamasishaji, zitatumika kutangaza utalii katika matangazo husika na kuzitaja kuwa ni pamoja na Kupanda Mlima, Wanyama Pori na Fukwe.
“Ni mkataba wa udhamini wa kuonyeshwa kwa matangazo yetu katika michezo ya Ligi Kuu ya timu hizo ambapo mechi 114 itahusika na kampeni tatu kuu za uhamasishaji zitatumika,” alisema Nzuki.
Alifafanua kwamba matangazo hayo yenye ujumbe unaolenga kampeni hizo tatu, yatakuwa yakionyeshwa kwenye kuta maalumu za matangazo za viwanja vya timu hizo katika mechi tofauti kwa msimu huu.
Alisema tayari matangazo hayo yameanza kuonekana katika michezo
iliyochezwa na timu husika tangu kuanza kwa ligi hiyo na kutolea mfano wa matangazo yalianza kuonyeshwa kwenye mechi za Agosti 14 kati ya Blackburn dhidi ya Everton, Sunderland vs Birmingham na Wolves vs Stoke City.
Akizungumzia maamuzi ya udhamini huo, Nzuki alisema ni mikakati ya kawaida ya kujiimarisha kiutendaji na kwamba hatua hiyo imelenga kuongeza mara dufu idadi ya watalii na hatimaye kukuza pato la taifa.
Alisema hatua hiyo haimaanishi kuwa walikuwa hawafanyi chochote katika kujitangaza kimataifa huko nyuma, lakini tukio la kuingiza matangazo husika katika ligi hiyo bora inayoangaliwa na takriban watu bilioni 3 duniani, ni cha kujivunia.
“Tunajivunia hatua hii kubwa kwani pamoja na jitihada zetu za uhamasishaji za huko nyuma, hatua hii inaonyesha kuwa ya mafanikio zaidi kwetu na taifa kwa ujumla kutokana na idadi kubwa ya watu tutakaowafikia na kupata ujumbe kupitia ligi hiyo,” alisema.
Ligi Kuu ya England ni kati ya ligi bora na zenye mvuto zaidi duniani huku takwimu za watafiti zikionyesha takribani watu bilioni 2.85 huangalia ligi hiyo duniani, hivyo mechi zinazohusisha timu kubwa za ligi hiyo huangaliwa na watu milioni 3.5 kwa wakati mmoja duniani.

Source:Tanzania Daima.


My Take.

Bila shaka huu ni mwanzo mzuri.Hongera wote mliofanikisha kuitangaza Tanzania na vivutio vya utalii.
 
Big up TTB. Angalizo hapo ni kwamba, watalii pamoja na fedha zitokanazo na utalii vinahitaji management nzuri.
 
Ni vema serikali ikaongeza uchakarikaji wa kutafuta pesa.. serikali bila pesa na sawa na baba-suruali.
 
At least this one make sense maaana kuna wakati nilishngaa eti walitangaza tanzania kwenye mabasi ya uwanja wa ndege huko Heathrow. Ilinichekesha sana

Lakini na hii tusubiri tune ukubwa na location ya hayo matangazo
 
Wakati serikali inatumia kodi za wavuja jasho kutangaza hivyo vivutio, ni shurti basi ikapima kuona watz wanafaidikaje..isije ikawa mvuja jasho anakamuliwa halafu kumbe mwisho wa siku mgeni ndio anafaidika kwa mahoteli yao, makampuni ya kuongoza watalii nk. Huo utakuwa ulimbukeni. Inabidi kuepo na justification kwenye mambo kama haya.
 
Ahahah.... sasa hivi tuna Sizonje anaangaika na bombadier kuleta watalii bongo na waziri wake Kigwangwala yuko bize facebook kututangazia utalii kupitia selfie zake kwenye gym na ziara zake za utalii mbugani.
 
Hii deal nadhani alipewaga mtoto wa town Juma Pinto akajipigia hela yake safiiiiii.
Wakati huo Lemtumboz alikuwa hakosekani pale sports lounge posta kwa Pinto.
 
Ahahah.... sasa hivi tuna Sizonje anaangaika na bombadier kuleta watalii bongo na waziri wake Kigwangwala yuko bize facebook kututangazia utalii kupitia selfie zake kwenye gym na ziara zake za utalii mbugani.
Mkuu watu walipiga pesa vizuri sana katika hili deal. Pinto katajirikia na hili deal.
 
Hii deal nadhani alipewaga mtoto wa town Juma Pinto akajipigia hela yake safiiiiii.
Wakati huo Lemtumboz alikuwa hakosekani pale sports lounge posta kwa Pinto.

Si ndiyo wakati huo mtoto wa mfalme R1 naye alikua uingereza masomoni mkuu ama umesahau? Hii nchi watu wameitafuna acha tu watu wamchukie Jiwe wampachike majina yote ya ajabu anastahili. Huwezi kuwafanyia watu roho mbaya kama hivi.
 
Back
Top Bottom