Tsh. Billion 200 za vijana mnazipeleka wapi?

Tsh. Billion 200 za vijana mnazipeleka wapi?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,025
Reaction score
16,711
Watanzania wenzangu tuwaondoe vijana wetu kandokando ya barabara kuuza machungwa 20 mezani badala yake twende tukawagawie ardhi iliyoboreshwa wazalishe kabla ardhi yao haijaisha kabisa.

Ningetamani hizo bil 200 zooote zingewekwa kama chambo kwa vijana kwenye kilimo kuwavuta vijana waende kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi.

Tunawadanganya sana vijana wetu kama tukiwaacha kandokando ya barabara, na kuendesha bodaboda huku tukijua kuwa tunawadanganya ili kesho ifike.

Lakini siku itafika ambapo kando ya barabara pia kutajaa na kuanza kugombana wenyewe kwa wenyewe kuwania nafasi za mbele barabarani au kugombana na serikali pale watakapogundua kuwa mliwadanganya kuwa hata kuuza mafenesi 2 ni kazi pia.

Barabara zinaharibika na njia za majitaka zinazibwa na takataka wanazozalisha vijana wetu. Pelekeni fedha nyingi kwenye ardhi kabla ardhi hii haijamezwa na matajiri wa ndani na nje ya Tanzania.
 
Nyingi watazipeleka tumboni. 🫄
Chache ndiyo zitawasaidia hao vijana.
 
Ni uongo tu mkuu Takwimu zote za Nchi yetu ni Uongo.
Hawa vijana wakiachwa waelendelee kufanya hivi ni rahisi kwa kushawishiwa kuichoma nchi yao maana hawana cha kupoteza. Ziko nchi zinaitamani ardhi yetu kwaajili ya ajira ya vijana wao. Ardhi ndio kete ya ushindi kwa vijana wetu vinginevyo hatukuwa na sababu ya maana ya kuitaifisha ardhi na kuiweka chini ya serikali.
 
Nyingi watazipeleka tumboni. 🫄
Chache ndiyo zitawasaidia hao vijana.
Kaka haiwezekani viongozi wetu wazidiwe uwezo kwa kiasi kikubwa na akina Nyerere katika mambo mengi.
Nyerere aliwataka vijana waachane na biashara zisizokuwa na tija kwao na taifa kama zile za kuuza kahawa, maji ya kandoro, karanga na mafesi mijini na kwenda vijijini ambako kuna ardhi kuuuubwa sana ya ufugaji, kilimo, na uvuvi. Mawazo ya Nyerere yanaishi hadi leo na kesho.

Hebu sikiliza wimbo huu

View: https://youtu.be/7ig5SdJnua8?si=16ePf-u4rC_6QtuC
 
Awamu hii watu wachache pekee ndiyo wanamiliki ukwasi. Huku mtaani pesa tunazotumia sisi waru wa kawaida, nyingi zimechakaa kutokana na mzunguko wake kuwa mkubwa.
Nchi imekuwa ya WAHUNI wachache na wale wanaojipendekeza
 
Una uhakika waliopo kwenye kilimo wana maisha kuliko walioko barabarani?

Kilimo cha Tanzania ni another scam project.
 
Una uhakika waliopo kwenye kilimo wana maisha kuliko walioko barabarani?

Kilimo cha Tanzania ni another scam project.
Kwanini tz kilimo kinaonekana kama bahati
Nasibu,wakati huku wenzetu mkulima ana thaminiwa,yaani ukisikia mtu anaitwa mkulima mpaka jamii inamuogopa
Serikali ingekuwa serious haya yote yangewezekana

Ila naona serikali inawataka vijana wawe ma content creator tu+wakata mauno

Ova
 
Awamu hii watu wachache pekee ndiyo wanamiliki ukwasi. Huku mtaani pesa tunazotumia sisi watu wa kawaida, nyingi zimechakaa kutokana na mzunguko wake kuwa mkubwa.
pesa zinazopita mikoni mwa watu zinapunguzwa na matumizi ya digital payments (M-PESA, YAS, AZAM PESA, KADI ZA BENKI, lipa namba, NK), watu wanabakia mikononi za kulipia tu daladala, vifurushi vya mihogo mimichi na karanga na vitu vichache kwa mangi. Nimejenga nyumba ikamalizzika kwa kulipa kwa mitandao ya simu kwenye maduka ya hardware na mafundi.
 
Una uhakika waliopo kwenye kilimo wana maisha kuliko walioko barabarani?

Kilimo cha Tanzania ni another scam project.
Kazi ya serikali ni kuwafanya walioko kwenye kilimo wawe na maisha kuliko walioko barabarani. Trillions and trillions za pesa zinatakiwa zikwekezwe kwa vijana vilioko kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi kabla ya ardhi hii haijachukuliwa na vijana wa Ruto, Kagame na wengine kwa mwamvuli wa mtangamano wa nchi za Afrika mashariki.

Viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi vijengo hukohuko ili vijana wa barabarani mijini wakose machungwa, maembe, maparachichi, ndizi za kutandaza chini.

Kama kilimo kitapewa maji ya kumwagilia mwaka mzima, matrekta, mbegu bora, pembejeo, tecnlojia na masoko ya uhakika vijana watafutika mijini na wale wa vijijini watabakia hukohuko mashambani kwenye mashamba ya mkonge, mpira, machungwa, malimao, pamba na viwanda vya kusindika mazao yao.
 
Kwanini tz kilimo kinaonekana kama bahati
Nasibu,wakati huku wenzetu mkulima ana thaminiwa,yaani ukisikia mtu anaitwa mkulima mpaka jamii inamuogopa
Serikali ingekuwa serious haya yote yangewezekana

Ila naona serikali inawataka vijana wawe ma content creator tu+wakata mauno

Ova
Wanajiandalia mabomu yanayosubiri muda ufike yawalipukie. Wanadhani kuwaacha vijana wawe barabarani ni kuwasaidia. Siku hizo barabara zikijaa n vijana wakakosa nafasi watagundua makosa yao na kutafuta nani kawashawishi.
 
Wanataka vijana wengi wawe bodaboda na content creator

Ova
 
Una uhakika waliopo kwenye kilimo wana maisha kuliko walioko barabarani?

Kilimo cha Tanzania ni another scam project.
Ningekuwa mimi hizo bil 200 zote ningezipeleka kwenye ardhi ya kilimo vijijini. Vijana wa vijijini wawe na fursa pia za uhakika kuliko wa mijini ili iwe sumaku ya kuwatoa vijana wanaozurura mijini. Maisha ya mijini duniani kote hata nchi zilizoendelea yamefanywa yawe magumu sana kwa vijana wasiokuwa na kazi, lakini hapa kwetu ni kinyume chake.
 
Wanataka vijana wengi wawe bodaboda na content creator

Ova
Hapa wanakosea sana. Lazima taifa lifanye mapinduzi kwenye jambo moja kwanza kabla ya kwingine. Sekta ambayo inabeba vijana wengi ni kilimo, na bahati nzuri ardhi kubwa ya kilimo tunayo na masoko ya ndani na nje yapo. Hata hela ya goli la mama ilipaswa kuelekezwa kwa kijana yupi amezalisha mazao yenye ubora wa masoko.

Mkakati lazima uwe Kilimo-maji-Umeme vijijini - barabara- maghala- masoko badala ya kutafuta wapi tutawasogeza vijana mijini wakati vijana wanahamia mijini kila siku kutoka mashambani.
 
Mfumo hautaki kuwakwama vijana kwa asilimia angalau 60 wawe na kipato,mazingira mazuri ya kuishi nk

Ova
 
Walete hizo pesa kwa vijana wanywee double kik na kvant
vijana wenyewe hawa wa akili za kubeti na kushinda mitandaoni? Wasiokuwa na maarifa na ujuzi wa kulima na kufuga
 
Back
Top Bottom