Trump Vs Snoop

Trump Vs Snoop

Na ndo mana nikasema we are far miles away from them,may be miaka mingi ijayo tutakua katika level yao
Hapana, hiyo ingekuwa kweli tu kama tungekuwa tunalenga hatma zinazoshabahiana...bahati mbaya ni kwamba tunakoelekea ni kinyume na wao hivyo kufikia level moja hakuwezekani. Utofauti wetu utazidi kupanuka na hizi grafu haziwezi kukutana mpaka hapo tutakapobadilisha mwelekeo wetu.
 
Hapana, hiyo ingekuwa kweli tu kama tungekuwa tunalenga hatma zinazoshabahiana...bahati mbaya ni kwamba tunakoelekea ni kinyume na wao hivyo kufikia level moja hakuwezekani. Utofauti wetu utazidi kupanuka na hizi grafu haziwezi kukutana mpaka hapo tutakapobadilisha mwelekeo wetu.
Sahihi kabisa
 
Ni kwel ndugu yangu ujue sisi tunakosea watu weng hupend kuchukulia mfano marekani wakat hawajui mafankio yao yametoka.mbali na washapita marais weng sana 45 sasa...wakat sisi tuna marais 5 tu....wamepitia pengi had watu wao kuwa ivo had democrasia kuwa ivo kwao...hatuwez lingana na marekani hata kdgo....hata wananchi wao wanavoitumia mitandao ya kijamii tafaut na sisi kabisa....[emoji24]
Ndio maana kwetu rais ukimsema kidogo tu utaambiwa "umetoa kauli za kumuudhi rais" na hakika utafungwa. Labda tusubir tukifika rais wa 30 hivi tutaweza kuwa sawa.
Pia bado tukumbuke kwamba hupaswi kuanza walipoanzia waliokutangulia. Jaribu kuanzia pale walipo au hatua kama moja tu nyuma yao. Vinginevyo turudi zama za mawe màana hapo kati tulishapoteana.

Pia si ajab mkasikia ninatafutwa kwa kuandika raisi badala ya Raisi.
 
Namuona Trump akipewa makavu na TI .

Kweli wenzetu wako mbali sana kwenye uhuru wa kuongea .

Hapa hata ukiita mtu bwege .........

34b57ea2c71da739431db2be3b37f63b.jpg
Duuh hii ingishii ya troubleman sijaelewa ata moja. Naona chenga tuu
 
Ngoja kwanza.

Marekani wameanzisha nchi yao 1776, haki ya kusema imeingizwa kama rekebisho la kwanza la katiba, mwaka 1791, miaka 15 tu baada ya uhuru. Kwa hiyo toka mwaka 1791 ulikuwa unaruhusiwa kwenda njia panda hadharani kumchanana chana Rais.

Kwa nini sisi ituchukue miaka 200?

Lakini kingine, sisi tuna blueprint ya kuiga, au desa la kuigilizia kama ni mtihani, wao wamepitia mitihani hii bila mwalimu, bila tuition wala madesa ya kuibia.

Sisi tunatakiwa tuwe tumefika hapo tayari.
 
Back
Top Bottom