Rais wa Marekani Donald Trump amewakosoa Viongozi wa Iran baada ya mazungumzo ya kidiplomasia kushindwa kuleta makubaliano kamili kuhusu suala la Nyuklia.
Kupitia ukurasa wake wa Truth Social, Trump amewataja Viongozi hao kuwa “Watu wasiotabirika, wagumu na wenye kubadilika badilika,” akisisitiza kuwa hawakuwa tayari kulegeza msimamo wao kwenye jambo muhimu zaidi la mpango wa Nyuklia.
Kauli hiyo ya Trump imekuja baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Makamu wa Rais JD Vance pamoja na Wajumbe Steve Witkoff na Jared Kushner waliokutana na Maafisa wa Iran Nchini Pakistan.
Licha ya Trump kueleza kuwa kulikuwa na mazingira ya heshima na urafiki kati ya pande hizo, amesema Viongozi wa Iran walibaki kuwa wagumu kubadilika katika msimamo wao, hasa kuhusu haki ya kurutubisha Madini ya Urani (Uranium), Trump amesisitiza kuwa Marekani haitaruhusu Iran kuwa na silaha za Nyuklia, akiongeza kuwa msimamo huo hauwezi kujadiliwa.