Rais wa Marekani Donald Trump amezungumzia hali ya mvutano na changamoto za kiusalama zinazohusisha Iran akisisitiza ugumu wa kuingia katika mifumo ya Nchi hiyo kutokana na uimara wake wa kijeshi na kiulinzi ambapo kauli hiyo imekuja katika muktadha wa tathmini yake kuhusu nguvu na uwezo wa Iran katika kukabiliana na Maadui zake.
Trump ameeleza hayo leo April 06, 2026, na kubainisha kuwa Iran imejijengea taswira ya Taifa lenye Wapiganaji hodari na Watu wenye msimamo mgumu hali inayofanya iwe vigumu kwa Mataifa mengine kuingilia au kushinda kirahisi.
Aidha, Rais amebainisha kuwa licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya nguvu kwa kipindi cha hivi karibuni bado Nchi hiyo inaendelea kuwa tishio lenye uzito.
"Kuingia himaya ya Mtu inahitaji mapambano na sidhani kuna Nchi ngumu kama Iran maana inahitaji mapambano sana, ni Wapiganaji wazuri sana ni Watu wagumu sana” amesema Trump.