kwinyo
JF-Expert Member
- May 2, 2017
- 281
- 230
Pakistan yaionya Marekani, yaiambia Afghanistan inaelekea kuwa Vietnam ya pili
Waziri Mkuu wa Pakistan ameionya Marekani kwamba hivi sasa Afghanistan inaelekea kuwa Vietnam ya pili kwa Washington.
Shahid Khaqan Abbasi amesema kuwa matatizo yote ya Afghanistan yanatakiwa yatatuliwe kwa njia ya mazungumzo na kwamba kinyume na hivyo taifa hilo la Asia litageuka na kuwa Vietnam ya pili dhidi kwa Marekani. Kadhalika Waziri Mkuu wa Pakistan amezungumzia kadhia ya kupambana na ugaidi na kuongeza kuwa Islamabad ipo tayari kushirikiana na upande wowote kwa ajili ya kupambana na ugaidi.
Amesema katika kuonyesha azma yake, serikali imesambaratisha maficho yote ya makundi ya kigaidi ndani ya ardhi ya Pakistan, huku akisisitiza kwamba kukatwa misaada ya kifedha ya Marekani kwa nchi yake hakutakuwa na taathira yoyote kwa Pakistan, kwani misaada hiyo haikuwa na mchango wowote katika kuboresha maisha ya raia wa Pakistan.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Khaqan Abbasi, alinukuliwa akisema kuwa Islamabad haichukulii jumbe za kutatanisha za mtandao wa kijamii wa Twitter za Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Pakistan, kuwa ni msimamo rasmi wa Washington, huku akifafanuwa kwamba siasa rasmi haziwezi kutangazwa kupitia jumbe zinazoandikwa katika mtandao huo, bali zinatangazwa kupitia nyaraka maalumu au vikao rasmi vya pande husika.
Uhusiano kati ya Marekani na Pakistan uliharibika baada ya Rais Donald Trump kuituhumu serikali ya nchi hiyo kwamba inawapa hifadhi magaidi wanaokimbia kutoka Afghanistan.