Trump: Ninakosa maisha yangu ya zamani.

fakalava

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
4,459
6,027
Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akizungumza kuhusu maisha ya awali kabla ya kuwa rais na kueleza jinsi wajibu wake huo mpya katika Ikulu ya White House ni ngumu.

Trump alisema aliyapenda maisha yake ya zamani kwa sababu ni mengi yalikuwa yakifanyika, alipozungumza na shirika la habari la Reuters akiwa White House.

"Hii ni kazi nyingi zaidi kuliko ya maisha yangu ya awali, alisema. "Nilifikiri itakuwa rahisi."

Huyu jamaa alidhani Urais ni mchezo mchezo, ndiyo maana Urais unatakiwa uwe na backgrounds za siasa.

Trump: Ninakosa maisha yangu ya zamani - BBC Swahili
 
Kama kazi imekuwa ngumu kuliko ulivyotegemea si uombe kustaafu?Uraisi sio kazi ya kukimbilia ni kazi ya kumtanguliza Mungu mbele na kuomba hekima kuliko tunavyofikiri.Utazeeka mapema sasa
 
Na mnyoa kiduku anavyojiamni atampelekesha mpaka akome kuringa wamwambie avue hilo wigi la sivyo kuna siku ataomba kuachia ngazi yeye alifikiri urais ni kuamka tua unaanza kutoa matamko
 
Mkuu mleta uzi umetafsiri neno kwa neno; miss = kosa. Kiswahili hakiendi hivyo mheshimiwa, hata kama umeichukua toka BBC ulistahili kuboresha.
 
Mkuu mleta uzi umetafsiri neno kwa neno; miss = kosa. Kiswahili hakiendi hivyo mheshimiwa, hata kama umeichukua toka BBC ulistahili kuboresha.
Shukrani sana, ila sina kumbukumbu kama nimeandika neno "miss".
 
Back
Top Bottom