Trump kushiriki maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Marekani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Trump kushiriki maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Marekani

Nov 14, 2020 07:21 UTC


Rais anayeondoka wa Marekani, Donald Trump amesema yumkini leo atajiunga na wafuasi wake katika maandamano ya mjini Washington, ya kupinga mchakato na matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita.

Katika ujumbe wa Twitter, Trump amesema anatiwa moyo na wimbi la maandamano yanayoshuhudiwa katika kona mbalimbali za nchi, kulalamikia matokeo ya uchaguzi huo, na kuongeza kwamba huenda leo Jumamosi ataungana na wafuasi wake watakaondamana katika mji mkuu, Washington DC.

Bila kutoa ushahidi wowote, Trump katika ujumbe huo ameendelea kusema kuwa kuna uchakachuaji na udanganyifu mkubwa wa kura kwa maslahi ya mshindani wake, Joe Biden.

Hii ni katika hali ambayo, uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni nchini humo uliofanywa na shirika la habari la Reuters na Taasisi ya Ipsos unaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wananchi hao wanaamini kwamba Trump anang'ang'ania madaraka bila sababu kwani ameshindwa katika uchaguzi huo wa Novemba 3.

Kadhalika taasisi zilizohusika na uendeshaji wa uchaguzi huo zimesema kuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuweko uchakachuaji au kupotea kura za uchaguzi huo.
 
Back
Top Bottom