Trump awashtua wamarekani na kutoa FUNZO

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Katika tukio ambalo si la kawaida kando la wakati wa rais Kennedy alipomteua ndugu yake kuwa waziri..
Trump naye ameingia na lake jipya kwa amemteua MKWEWE/Son in law
Jared Kushner kuwa ndo MSHAHURI mkuu wake wa Ikulu ya White House/White House senior adviser.
Na amesema HATACHUKUWA mshahara wa serikali.

Jared ambaye hana UZOEFU wa kisiasa umewaacha Wamarekani wakiuma vidole kwa mshangao.
Jared ni mfanya biashara ambaye Forbes inakadiria mali yake ni dollar za kimarekani 1.8 billion.

Swali Wana JF kama ni kwetu Tanzania?
Magufuli akifanya hivyo je kuna UBAYA wowote jamani?
Maana nchi yenye demokrasia kubwa imetuonyesha MFANO.
Maana kila mtu hutaka mtu wake wa KARIBU!
 
Katika tukio ambalo si la kawaida kando la wakati wa rais Kennedy alipomteua ndugu yake kuwa waziri..
Trump naye ameingia na lake jipya kwa amemteua MME wa binti yake/Son in law
Jared Kushner kuwa ndo MSHAHURI mkuu wake wa Ikulu ya White House/White House senior adviser.
Na amesema HATACHUKUWA mshahara wa serikali.

Jared ambaye hana UZOEFU wa kisiasa umewaacha Wamarekani wakiuma vidole kwa mshangao.
Jared ni mfanya biashara ambaye Forbes inakadiria mali yake ni dollar za kimarekani 1.8 billion.

Swali Wana JF kama ni kwetu Tanzania Magufuli akifanya hivyo je kuna UBAYA wowote?
Maana nchi yenye demokrasia kubwa imetuonyesha MFANO.
Maana kila mtu hutaka mtu wake wa KARIBU!
Hata mkulu anao sema hajaweka hadharani
 
Tatizo kwa Afrika hizi teuzi za undugu huwa ni namna ya kulifisidi taifa na kulindana. Nadhani, umeona tofauti ya Trump na Afrika - hatachukua mshahara wa Serikali; kwa Afrika thubutu! Hao "ndugu" ndani ya muda mfupi wanageuka mabilionea na miungu watu wasiohojiwa na chombo chochote na mifano ipo ya kutosha kabisa. Yule wa Marekani sio tu tayari ni bilionea (tena ubilionea wa jasho la ukweli) bali ni kichwa balaa - pita CV yake ujionee.
 
Kuna kitu nyuma ya pazia Jared ni Mmarekani mwenye nasaba ya Myahud na mpango wa Trump nikuendelea kuilinda Israel pia Jared Kushner ndio atakuwa mshahuri pia wa mambo ya Masharik ya kat,Kwa mazingira hayo Iran ijiandae
 
Yawezekana sana.
Unajua shirika la Ujasusi la Israel Mossad hutumia sana RAIA wake WAISHIO nchi za KIGENI katika kuwasaidia kupata duru za KIJASUSI.

Watu hawa ambao wana damu ya Kiyahudi na niwaenda Masinagogi, hujulikana kama SAYANIM-Ama SAYAN.
Maanake WASADIZI.
Huwa ni watu wa kawaida sana tu, Wafanya Biashara, Wafanya kazi na watu wenye utaalamu mbali mabali hivyo Mossad huwatumia sana.
SAYAN hawa Si waajiriwa rasmi wa Mossad bali hujitolea kwa ajili ya UPENDO wa TAIFA lao.

SITASHANGAA kuona SERA za Marekani kuhusu Mashariki ya Kati ZIKIBADILIKA sana.!
 
Back
Top Bottom