Trump awanyima Visa Maafisa wa kiserikali na wafanya biashara mashuhuri wa Afrika!

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Rais Trump katika kukaza kamba kuzuia watu kuingia nchini mwake ameamua kuwazuia wajumbe kutoka Afrika kuhudhuria mkutano wa kibiashara ulioandaliwa Marekani na Umoja wa Mataifa (UN)

Wajumbe hao ambao miongoni mwao ni maafisa wa Kiserikali wa nchi zao walikuwa waende Marekani katika mkutano uliohusu
KU PROMOTE
Bilateral foreign direct investiments,
International Trade,
Cultural Exchange na
UTALII.
Wajumbe hawa kutoka nchi 54 za Afrika walinyimwa Visa za kuingia Marekani. Siku chache kabla ya safari.Balozi mpaka sasa hazijatoa sababu zozote kutokana na katazo hilo.

Japokuwa wajumbe walikuwa wamekwishatuma maombi ya Visa WIKI KADHAA zilizopita. Lakini cha kushangaza waliitwa kwenda kufanya interview siku CHACHE kabla ya kusafiri na WOTE wakanyimwa.

Pigo hili limewaacha nje wajumbe 100 wa Kiafrika ambao wangeliwasilisha bara la Afrika katika mkutano huo.
Kitendo hiki kimewaudhi wajumbe wengi.

Miongoni mwa nchi ambazo wajumbe wake walinyimwa Visa ni
Ghana,
Sierra Leone,
Afrika ya Kusini,
Nigeria,
Guinea,
Ethiopia, miongoni mwa zingine.

Miongoni mwa watu walioathirika ni Msanii mashuhuri mtaalamu wa SPECIAL EFFECTS GRAPHIC ART, Prince Kojo Hilton wa Ghana ambaye alikuwa aongoze session ya Film Making katika mkutano huo.

Hali hii imeacha sintofahamu kwa Safari zijazo hasa baada ya Trump kutoa agizo la kuzuia nchi fulani kutoingia Marekani lilopingwa na Mahakama.
Chanzo:VOA
 
Back
Top Bottom