Trump atashinda Uchaguzi USA

Bolshevick

JF-Expert Member
Sep 2, 2013
355
247
YANAYOENDELEA REPUBLICAN BAADA YA TRUMP KUKOSA WA KUMZUIA.(JAMAA WANADHIHIRISHA DEMOCRACY HAPA TZ WANAKUKATA JUU KWA KWAJU NA KUMUWEKA WAO)
Na:Joseph Mshinga.

1.Wapinzani wa Donald Trump wamejitoa wote baada ya matumaini yao kumzuia kushindikana.

2.Hakuna namna tena ya kumzuia billionea Donald Trump kuwa mgombea urais wa Republican.

3.Chama cha Republican kinashuhudia mgawanyiko na mpasuko mkuwa kabisa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote.

3.Wanachama wa Republican wameonekana kuchoma moto kadi zao za uachama kama hasra zao kwa mgombea ambaye hawamtaki.

4.Wapo wanaosema hawatashiriki kabisa kupiga kura uchaguzi mkuu kwa kuwa Donald Trump hawamtaki na hawawezi kumpigia kura Hillary Clinton.Wapo ambao wanajiondoa katika chama.

5.Wapo wanaosema watalazimika kumchagua Hillary Clinton maana hawako tayari kuona Donald Trump anakuwa Rais wa Marekani.

6.Wapo wanaoona ni bora tu wakubaliane na hali na kumuunga mkono mtu ambaye hawamtaki kwa manufaa ya chama.

7.Aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W Bush mwenye umri wa miaka 91 amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hana mpango wa kumuunga mkono Donald Trump.
Hii ni mara ya kwanza kwa George H.W Bush kutomuunga mkono mgombea wa chama chake cha Republican katika chaguzi zote.

8.Aliyekuwa rais wa 43 wa Marekani George W Bush(Junior ) naye amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hatamuunga mkono Donald Trump.
NB:Marais wastaafu wa Republican walio hai ni hawa Bush wawili kwa maana ya baba na mwana.

9.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2012 Mitty Romney amesema hatamuunga mkono Donald Trump na ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa hata kwenye mkutano mkuu wa kumtanganza mgombea pale Cleveland hatashiriki.

10.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2008 John McCain naye yupo mbioni kutoa taarifa rasmi.Taarifa za awali zinadokeza kuwa naye atachukua msimamo wa kutomuunga mkono Donald Trump na atajiweka kando katika uchaguzi huu.

11.Matajiri wapenzi wa chama nao wamegawanyika kama ilivyo hapo juu kwa makundi mengine wapo ambao wameonekana tayari kumuunga mkono Hillary Clinton kwa kuandika hadharani kauli mbiu ya Hillary Clinton I AM WITH HER (wakimaanisha wanamuunga mkono Hillary Clinton na si mgombea wa chama chao).
 
Hahaha ....bora huko wana akili ....huku kwetu gia zilibadilishiwa angani na watu wakakubali kuzungurusha mikono ...wengine na barabara wakadeki ....kweli elimu, elimu, elimu ....
hahaha. ..wewe naweee...uchaguzi ulishaisha wewe bado unaugua...
 
Huyo jamaa mimi namkubali kinoma yaani kwa maana ni style ya Magufuli wetu, hivyo kama akipita itakuwa poa sana ingawaje ni ngumu sana kuamini kama kweli wanweza kumpa!
Kumpa wanaweza sana, maana Hilary inaonekana naye ni warmonger kama huyu tu, na tatizo jingine la Republicans ni wahafidhina sana.
 
Huwezi kuchukua nchi ikiwa wengi ndani ya chama chako wanakupinga wazi wazi tena hadharani. Hillary akijipanga vizuri kwenye hizi kampeni kuwatumia akina Michelle, Barack, African American, white na Latino celebrities wanaomuunga mkono na kuhakikisha wote wanaomuunga mkono kujitokeza kwa wingi kupiga kura, basi ataichuikua nchi kiulaini na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais USA.
 
Huwezi kuchukua nchi ikiwa wengi ndani ya chama chako wanakupinga wazi wazi tena hadharani. Hillary akijipanga vizuri kwenye hizi kampeni kuwatumia akina Michelle, Barack, African American, white na Latino celebrities wanaomuunga mkono na kuhakikisha wote wanaomuunga mkono kujitokeza kwa wingi kupiga kura, basi ataichuikua nchi kiulaini na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais USA.
Mama Clinton ana tamaa hatosheki : first lady ,gavana, mtangaza nia 2008, secretary of state. Leo tena anataka Urais mumewe awe first gentleman! Nashauri apumzike alee wajukuu. Maybe for the first time big nation kama USA watapata Rais Grandma.
 
Trump ana mbwembwe sana juz ana mwambia hirary clinton kuwa ashukuru yeye ni mwanamke hivyo atapatapata kura kidogo ila angekuwa mwanaume hata kura kidogo hata pata sabab atampiga knock out bila shika
 
Je Seneta John McCain naye ametoa msimamo gani mpaka sasa juu ya Trump?
 
Back
Top Bottom