Trump ataka shule za umma kufunguliwa

Trump ataka shule za umma kufunguliwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali za majimbo nchini humo zinapaswa kufikiria kufungua shule za umma licha ya hofu ya usalama wa kiafya inayowakodolea macho wanafunzi kutokana na janga la virusi vya corona.

Rais Trump alitoa kauli hiyo katika mkutano wa njia ya simu kwa magavana waliokuwa wakijadili jinsi ya kuruhusu tena shughuli za kiuchumi kuendelea miongoni mwa masuala mengine.

Amesema "Tunapendekeza wafungue shule haraka iwezekanavyo lakini kwa tahadhari na kuzingatia usalama. Tunataka kila mtu awe salama, nadhani mutaliona hilo. Magavana wengi wanafikiria kuhusu mifumo ya shule zao, si mbali shule zitafunguliwa tena hata kama ni kwa muda mchache. Nafikiria huenda likawa jambo zuri."

Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, hakuna gavana yoyote aliyeridhia pendekezo hilo la kufungua shule. Maafisa wengi wa elimu wana wasiwasi kuwa huenda kukawa na hasara kubwa hata kuliko faida iwapo shule zitafunguliwa.

Shule kote nchini Marekani zimefungwa kutokana na janga la virusi vya Corona.

Chanzo: DW Swahili
 
Hili jitu jinga kabisa ndiyo maana linapendekeza watu wadungwe sanitisers na kuwasubject watu kwenye UV light kuua coronavirus
 
Naskia wanafanana akili na jamaa mmoja hivi kwa kupambana na janga hili na watu wake wanamsifia kila siku kwa kumfananisha na huyu jamaa...!
 
Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali za majimbo nchini humo zinapaswa kufikiria kufungua shule za umma licha ya hofu ya usalama wa kiafya inayowakodolea macho wanafunzi kutokana na janga la virusi vya corona.

Rais Trump alitoa kauli hiyo katika mkutano wa njia ya simu kwa magavana waliokuwa wakijadili jinsi ya kuruhusu tena shughuli za kiuchumi kuendelea miongoni mwa masuala mengine.

Amesema "Tunapendekeza wafungue shule haraka iwezekanavyo lakini kwa tahadhari na kuzingatia usalama. Tunataka kila mtu awe salama, nadhani mutaliona hilo. Magavana wengi wanafikiria kuhusu mifumo ya shule zao, si mbali shule zitafunguliwa tena hata kama ni kwa muda mchache. Nafikiria huenda likawa jambo zuri."

Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, hakuna gavana yoyote aliyeridhia pendekezo hilo la kufungua shule. Maafisa wengi wa elimu wana wasiwasi kuwa huenda kukawa na hasara kubwa hata kuliko faida iwapo shule zitafunguliwa.

Shule kote nchini Marekani zimefungwa kutokana na janga la virusi vya Corona.

Chanzo: DW Swahili
USA Wanazingua itakuwa wanapika data za vifo siyo uhalisia.
Vifo vyote hata makaburi ya pamoja hayaonekani kwenye videos.
Trump anajua what is going on ndo maana analazimisha shughuli zifunguliwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_20200430-081835.png
 
Back
Top Bottom