Trump Ataka Kupitishwa kwa “Save America Act” Ili Kulinda Mfumo wa Uchaguzi na Sera za Kijamii

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Kumekuwa na mjadala mkubwa nchini United States kufuatia wito wa kupitishwa kwa sheria mpya inayojulikana kama “Save America Act.” Sheria hii inapendekezwa na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambaye amesisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha uadilifu wa uchaguzi pamoja na kulinda maadili ya kijamii nchini humo.

Kupitia ujumbe uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii unaohusishwa na akaunti za Ikulu ya Marekani (White House) na akaunti ya rais huyo wa sasa wa Marekani (inayojulikana kama POTUS) katika mitandao ya kijamii ikiwemo instagram, Trump ametoa mapendekezo kadhaa ambayo angependa yaingizwe kwenye sheria hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyochapishwa, kipengele cha kwanza kinapendekeza kuwa kila mpiga kura atalazimika kuonyesha kitambulisho cha mpiga kura (Voter ID) kabla ya kuruhusiwa kupiga kura. Lengo la pendekezo hili ni kuzuia udanganyifu katika uchaguzi na kuhakikisha kuwa watu wanaoshiriki kupiga kura wanatambulika rasmi.

Pili, pendekezo hilo linataka kila mpiga kura atoe uthibitisho wa uraia wa Marekani kabla ya kupiga kura. Wanaounga mkono hoja hii wanaamini kuwa hatua hiyo itahakikisha kuwa ni raia halali pekee wanaoshiriki katika mchakato wa kidemokrasia wa kuchagua viongozi na sio raia wavamizi.

Pendekezo la tatu linahusu kupunguza au kuzuia kabisa matumizi ya kura za sanduku la posta (mail-in ballots), ambapo wapiga kura utumiwa vifurushi vyenye karatasi za kupigia kura wakiwa walipo kisha wakimaliza kupiga kura wanazituma tena kwenye sanduku la posta. Kulingana na mpango huo, kura za aina hii zitaruhusiwa tu katika mazingira maalum kama vile ugonjwa, ulemavu, wanajeshi walioko kazini, au mtu anayesafiri na hawezi kufika kituoni kupiga kura. Wafuasi wa pendekezo hili wanasema linasaidia kudhibiti udanganyifu, ingawa wakosoaji wanasema linaweza kupunguza ushiriki wa wapiga kura.

Aidha, pendekezo lingine linalozua mjadala ni lile linalotaka wanaume wasiruhusiwe kushiriki katika michezo ya wanawake, hoja ambayo imeibua mjadala mpana kuhusu haki za wanariadha na masuala ya jinsia katika michezo. Kama mnavyofahamu kulikuwa na Mjadala wanaume wanaobadilisha jinsia na kuwa wanawake walikuwa wakishiriki michezo ya wanawake. Kibaiolojia bado wanabaki wanaume licha ya Kubadilisha maumbile.

Kipengele cha tano kinahusu upasuaji wa kubadilisha jinsia kwa watoto, ambapo pendekezo linaeleza kuwa taratibu hizo hazipaswi kufanyika kwa watoto bila idhini ya maandishi kutoka kwa wazazi au walezi wao.

Mapendekezo haya yameibua mijadala mikali katika siasa za Marekani, huku baadhi ya wanasiasa na wananchi wakiyaunga mkono wakisema yanalenga kulinda mfumo wa uchaguzi na maadili ya jamii. Hata hivyo, wengine wamekosoa mapendekezo hayo wakidai yanaweza kuathiri haki za kiraia na uhuru wa baadhi ya makundi ya watu.

Mjadala kuhusu Save America Act unaendelea ndani ya vyombo vya kisiasa na kijamii nchini Marekani, huku wachambuzi wakisema kuwa iwapo mapendekezo hayo yatawasilishwa rasmi bungeni, yanaweza kuchochea mjadala mkubwa katika siasa za taifa hilo.

550c7811f20745ddaa71eb9957be9a74.jpg
 
View attachment 3553151
Trump alizaliwa Marekani kimakosa. Kwa jinsi alivyo, alipaswa kuzaliwa Africa ambako mambo yetu tunayaendesha kwa kuchezwa na machale na imani kwamba kuna mkono wa mtu kwenye kila unfavorable outcome!
 
yupo sahihi kabisa

vitambulisho vinahitajika kupiga kura kama vinavyotumika kuendesha gari, kukata tiketi ya ndege , kulipa bima, kuomba ajira, udahili wa vyuoni, ndoa, kufungua account ya bank, kusajili line, kwenda mahakamani, n.k.

Chama cha kina Obama, Bidden, Kamala Harris ni vinara wa kuiba kura Marekani, hawataki vitambulisho.
 
That’s utter nonsense. Hakuna illegal immigrant mwenye ujasiri wa kujisajili kuwa mpigakura. If anything, illegal immigrant hapendi kabisa unnecessary interactions na Serikali.

Hata mwenye green card naye hataki kuhatarisha uwezekano wa yeye kupata uraia!
 
Trump alizaliwa Marekani kimakosa. Kwa jinsi alivyo, alipaswa kuzaliwa Africa ambako mambo yetu tunayaendesha kwa kuchezwa na machale na imani kwamba kuna mkono wa mtu kwenye kila unfavorable outcome!
Yeah true
 
Hiyo mijadala ya jinsia ni kama vile wanatumia akili mnemba ama unde...😅
 
Kumekuwa na mjadala mkubwa nchini United States kufuatia wito wa kupitishwa kwa sheria mpya inayojulikana kama “Save America Act.” Sheria hii inapendekezwa na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump,

Mzee nii ni habari ya zamani umenakili mahali au ni makosa ya kiuandishi?
 
Anajisumbua tu hakuna kura 60 za seneti kupitisha huo ujinga wake.
 
Kuna mengi katika chaguzi za Marekani ni kama Africa tofauti ni mapokeo tu ya watu wa Africa kuhusu chaguzi za Marekani.

Hivi kuna mpinzani nchi hii anaweza kuunga mkono uchaguzi wa Tanzania ufanyike na mpiga kura asioneshe kitambulisho chake.

Sasa ukitaka kujua akili za Watz/Waafrica ni katika mambo ya namna hii.

Hapa kuna mtu anaona sawa mpiga kura asioneshe ID voter katika uchaguzi wa Marekani lakini aoneshe katika uchaguzi wa Tz.

Tunasafari ndefu sana.
 
Watu kuhitajika kuonyesha kitambulisho cha mpiga kura tu bado uchaguzi wa Tanzania ni wizi na udanganyifu mtupu. Hata hivyo bado ni sheria ya hovyo kunyima watu wenye passport na leseni za udereva kupiga kura.

Marekani pamoja na kutokuwa na sheria za kuhitaji raia kuwa na vitambulisho vyovyote kupiga kura bado hakujawahi kuwa na matatizo ya uchaguzi katika kura mpaka alipokuja mwendawazimu Trump kwenye siasa zao. Hata hivyo kabla ya kupiga kura Marekani lazima ujiandikishe na uthibitishe kuwa ni raia na mkazi wa Marekani katika Jimbo lake.
 
Back
Top Bottom