Donald Trump atangaza kusimamisha vita na Iran kwa siku 5 kuanzia leo

Sir John Deere

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
14,162
Reaction score
27,197
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kusitisha kwa muda wa siku tano mipango yote ya kijeshi ya kushambulia miundombinu ya nishati ya Iran, kufuatia kile alichokielezea kama mazungumzo "mazuri sana na yenye tija" yaliyofanyika ndani ya siku mbili zilizopita kati ya mataifa hayo mawili.

Kupitia ujumbe wake (kwa herufi kubwa) alioutoa leo, Trump amebainisha kuwa sauti ya mazungumzo hayo ya kina yanamfanya aamini kuwa kuna uwezekano wa kufikia suluhu ya kudumu ya uhasama uliopo Mashariki ya Kati.

Rais Trump ameiagiza wizara yake ya ulinzi kusitisha mashambulizi yaliyokuwa yamepangwa dhidi ya vinu vya umeme na miundombinu ya mafuta ya Iran, ili kutoa nafasi kwa timu za majadiliano kuendelea na kazi hiyo wiki nzima.

"Nimefurahi kuripoti kuwa Marekani na nchi ya Iran zimekuwa na mazungumzo yenye tija kuelekea suluhu ya jumla ya uhasama wetu. Kufuatia mazungumzo haya ya kina na ya kujenga, nimeelekeza kuahirisha mashambulizi yoyote ya kijeshi kwa kipindi cha siku tano," ameandika Rais Trump.

Tangazo hili limekuja wakati saa 48 za sharti la awali la Trump zikikaribia kuyoyoma. Kusitishwa huku kwa mashambulizi kunatarajiwa kupunguza taharuki katika Mlango-Bahari wa Hormuz na kunaweza kusaidia kushusha bei ya mafuta ambayo ilikuwa imeanza kupaa kutokana na hofu ya vita vya jumla.

20260323_144805.jpg
 
Rais Donald Trump kupitia mtandao wake wa truth social ametangaza kusimamisha mashambulizi ya kijeshi kwa siku 5 kuanzia Leo ili kupisha mazungimzo na Iran ya kumaliza vita.
Naona malengo ya marekani na Israel yemegonga mwamba. Wameanza kula Kona.
View attachment 3561684
Kama Trump hawezi kuandika proper English, watanzania wote wanaopuyanga hii lugha wasamehewe bure.
 
Subirini atakachokifanya kabla ya hizo siku tano kuisha. Hiyo ni war stratergy yake ya shambulizi la kushitukiza. Siku hizo anazuga kwamba ana negotiation ila anachukuza makombora ya iran yanarushwa kutoka sehemu gani ili apalipue bado haamini kuwa iran anaendelea kuwa na nguvu kiasi hicho na yeye ni mpenda sifa asiyetaka kushindwa
 
Rais Donald Trump kupitia mtandao wake wa truth social ametangaza kusimamisha mashambulizi ya kijeshi kwa siku 5 kuanzia Leo ili kupisha mazungimzo na Iran ya kumaliza vita.
Naona malengo ya marekani na Israel yemegonga mwamba. Wameanza kula Kona.
View attachment 3561684
Baada ya vita kumalizika Iran atakuwa muuzaji Mkuu wa silaha Duniani.

Mwisho Tulikubaliana hakuna wa kuzungumza nao wote wameuwawa 😂😂
 
Hayo mazungumzo si yalikuwepo toka mwanzo? Kilichofanya waiattack Iran ni kipi? Na kipi kinawafanya warudi tena kwenye mazungumzo?

FUNZO,

Hapa Duniani,usikubali kabisa kuonewa hata siku moja,tumia akili zako zote na nyenzo zako katika kujitetea na kujilinda na kurudisha mapigo kwa adui,
Dunia ya kutia huruma au kutafuta huruma haipo tena,

Bravo IRAN.
 
Subirini atakachokifanya kabla ya hizo siku tano kuisha. Hiyo ni war stratergy yake ya shambulizi la kushitukiza. Siku hizo anazuga kwamba ana negotiation ila anachukuza makombora ya iran yanarushwa kutoka sehemu gani ili apalipue bado haamini kuwa iran anaendelea kuwa na nguvu kiasi hicho na yeye ni mpenda sifa asiyetaka kushindwa
Umecomment kama vile US anapigana na Wilaya ya Urambo,

Iran wapo makini sana toka yale mazungumzo ya mwanzo waliositisha na kuiattack Iran,usifikiri unachokihisi wewe basi wao Iran hawakijui,masaa aliyotoa Trump wafungue Hormuz yameishia wapi?
 
Hauwezi jua nini kiko nyuma ya pazia. Lazima wana benefits za gharama za vita. Remember America First!!!

IRANI HAITAKI MAZUNGUMZO NA WANAFIKI.....
WAKATI IRANI INAPIGWA NA KIBARAKA WA MAREKANI (ISRAEL) WALIKUA KWENYE KIKAO CHA MAZUNGUMZO.
SASA KUNA UHAKIKA GANI, KAMA MAREKANI & ISRAEL WANAMAANISHA AU WANATAFUTA NAMNA YA KUOKOA SOKO LA HISA LILILOPOROMOKA KULE NEWYORK KWA SABABU YA VITA???
Sishabikii vita ILA sijui kwa nini Israel na Marekani walishambulia Irani wakati wapo katikati ya mazungumzo!
 
Back
Top Bottom