Trump ashinda majimbo muhimu Marekani

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
16,456
30,882
160316020024_trump_624x351_getty_nocredit.jpg

Mshindi chama cha Republican Florida na Ohio hukabidhiwa wajumbe wote
Donald Trump amepiga hatua katika kukaribia kutwaa tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani baada ya kushinda mchujo majimbo matatu makubwa, likiwemo jimbo la Florida.

Bilionea huyo kutoka New York ameshinda majimbo ya Illinois na North Carolina.

Hata hivyo ameshindwa na John Kasich jimbo la Ohio.

Mgombea anayeongoza chama cha Democratic Hillary Clinton naye amepanua uongozi wake kwa kupata ushindi majimbo ya Florida, Ohio, Illinois na North Carolina.

Marco Rubio, mmoja wa waliotarajiwa kutoa ushindani kwa Trump katika chama cha Republican amejiondoa baada ya kushindwa na Trump katika jimbo lake la nyumbani la Florida.

Majimbo matano makubwa, Florida, Missouri, North Carolina, Ohio, Missouri na Illinois, yalifanya mchujo Jumanne.

Image caption Trump amemsifu Rubio
"Lazima tuunganishe chama,” amesema Bw Trump akihutubu Palm Beach, Florida, baada ya kupata ushindi.

Anatumai kwamba ushindi huo utamfungulia njia ya kupeperusha bendera ya chama cha Republican.

John Kasich hata hivyo ameshinda jimbo lake la kwanza tangu mchujo kuanza, jimbo la Ohio ambako yeye ndiye gavana.

Akihutubu baada ya ushindi, Bw Kasich amesema anataka kuweka “mazingira ya kubuni nafasi” kwa vizazi vijavyo na pia akampongeza Bw Rubio kwa kampeni yake.

Bw Rubio ametangaza kujiondoa kwake kwenye kinyang’anyiro katika mkutano wa kampeni mjini Miami baada ya kushindwa Florida.

Amesema Marekani imo kwenye dhoruba ya kisiasa na kwamba wapiga kura wamekasirika na kutamauka.

Image copyright Reuters
Image caption Clinton amemshutumu Trump akisema anawagawanya Wamarekani
Katika jiji hilo, Bi Clinton ametoa hotuba yake akifurahia ushindi ambapo amemshutumu Bw Trump na kusema „Wamarekani wana hamu ya kupata suluhu (kwa changamoto zinazowakabili)”.

Mpinzani wake, seneta wa Vermont Bernie Sanders, amewahakikishia wafuasi wake Phoenix, Arizona, kwamba atasalia kwenye kinyang’anyiro na kusema tayari kampeni yake imezidi matarajio ya wengi.

Majimbo ya Florida na Ohio huwa muhimu sana kwa chama cha Republican kwani mshindi hukabidhiwa wajumbe wote.

Florida huwa na wajumbe 99 na Ohio wajumbe 66.


Chanzo: BBC SWAHILI
 
Trump atashinda hizi primaries ila urais atausikia tu cnn.
Hata mi ningependa iwe hivo ila kwa kweli Hillary Clinton hataweza kupambana na Trump mbavu kwa mbavu. rais wa marekani atakuwa Trump. Watu wengi wanadhani eti kwa sababu Trump ni racist hivo hawezi kushinda urais ila ki ukweli majority ya wamarekani wengi weupe ni racist in nature na ndio maana unaona Trump anazidi kunyakuwa majimbo kwa ushindi siku hadi siku.
 
Hiyo siyo wall ya Trump..huwa hampo makini kuchunguza mnapotoa hizo taarifa. Ndiyo maana Nyani Ngabu amejuwa busy kuwakatalieni kuhusu hayo matamko fake ya Trump mnayo sambaza.

Posy Trump kwenye wall yake, j ust in three minutes tayari ina more 30k likes..na other Ks of post. Sasa hiyo yako 26 minutes ina post 250. Yaani anazidiwa hata na comments anazopata mshana jr japa JF!
 
Rep wakitaka kumshnda clinton basi wamwekee Trump,vingnevyo clinton atashnda asubuh na mapema.
 
Trump is about to win. Let's wait and see. All the best Mkuu.

Hiyo "all the best mkuu" yakk unampa Trump??! :eek::eek:

Acha kujitoa ufahamu, you are black for godsake, au umesahau?! Trump is no a mkuu to any black dickhead nigga:mad::mad:

Afu sio kila comment lazima uandike mkuu, au ndo kuonyesha usomi wa chuo kikuu:rolleyes::rolleyes:
 
Hiyo "all the best mkuu" yakk unampa Trump??! :eek::eek:

Acha kujitoa ufahamu, you are black for godsake, au umesahau?! Trump is no a mkuu to any black dickhead nigga:mad::mad:

Afu sio kila comment lazima uandike mkuu, au ndo kuonyesha usomi wa chuo kikuu:rolleyes::rolleyes:

!
!
Aisee hata mimi nadhani na natamani Trump ashinde urais
 
Back
Top Bottom