Trump anashabikiwa kwa mambo ambayo hakuyasema

hukumundo

JF-Expert Member
Oct 8, 2011
849
435
Siwezi kuacha maneno yasiyo na busara yanayomsifia Trump yakapita bila kupingwa. Mmoja kamfananisha hata na Magufuli! Naona ni fedheha na matusi makubwa kumfananisha raisi wetu Magufuli na Trump. Na kabla ya yote jihadhari sana usipende kufanya ushabiki wa kisiasa kwa misingi ya jambo moja tu ulilolisikia tena bila kujiridhisha kwamba limesemwa hivyo. Mambo yanayodaiwa kayasema kuhusu Mugabe au Museveni na viongozi wengine wa Afrika hakuyasema. Yametoka kwenye magazeti ya tashtiti au kejeli. Si kweli jamani. Hebu tuangalie "ukweli" wa Trump na tuulinganishe na mwelekeo na matamshi ya JPM.

1. Trump anatamba kwamba yeye ni tajiri sana na ana akili sana ndiyo maana kafanikiwa sana katika biashara zake. Ni kweli yeye ni tajiri sana. Alipomaliza masomo yake alipata kianzio cha dola milioni na babake. Baada ya hapo amefanya biashara kadha kubwa. Nyingi sana alikuwa akitumia ujanja wa kuzifilisi na kuchukua mkwanja wake. Pia google “Trump University” upate habari za utapeli wake huku akiwa anafuata sheria. Je, JPM anafanya hivyo? Magufuli anachukia utapeli kabisa. Nafikiri Trump angalikuwa Bongo angalikuwa jipu kubwa la kutumbuliwa.

2. Trump anadai kwamba wahamiaji ndiyo wanaoleta matatizo huko Marekani. Kwamba Mexico ndiyo inaleta makusudi wabakaji, wezi na wahamiaji haramu. Sijapata kumsikia raisi wetu akitoa ufedhuli unaofanana na huo. Isitoshe, wazungu waliwanyang’anya nchi watu wa asili wa Marekani waliokuwa huko kabla ya kuja kwa wazungu. Leo hii wazungu ndiyo wanazuia kwamba nchi ni yao?

3. Alipata kutoa takwimu kwamba watu weupe wengi waliuawa na watu weusi. Of course, ni uwongo uliokusudiwa kuwatia kiwewe wazungu wabaguzi. Niongeze kuwa hao ndiyo wenye hamasa wanaompaisha mpaka sasa. Sililiza takwimu za Magufuli, hutaona upuuzi wa kujaribu ku-antagonize kundi fulani la watu.

4. Kuhusu ugaidi, amedai kwamba atazuia Waisilamu wasiingie Marekani ili kuzuia ugaidi. Lakini kwa Marekani, ugaidi namba moja hufanywa na watu weupe. Ukweli huu haujawahi kuzungumzwa na mnayemsema mkweli. Mauaji yaliyotokea 1995 Oklahoma City yalifanywa na kijana wa kizungu. Vijana waliwaua vijana wenzao huko Colorado miaka ya 90 walikuwa wazungu. Hivi karibuni, kijana aliyeingia kwenye kanisa la weusi na kuwaua alikuwa mzungu. Na jana nimesoma habari huko Michigan bwana mmoja mzungu amepita akaua watu 6. Na mengi tunayasikia kila mwaka. Kutozungumzia njia za kukomesha mambo hayo ni unafiki wa kupindukia na kielelezo cha ubaguzi wa rangi na dini. Tafadhali usimfananisha maaluni huyo na raisi wetu.

5. Trump anataka kabisa kuleta ubaguzi wa kidini na kupendelea Ukristo. Kichekesho ni kwamba alipokaribishwa kuhutubia katika chuo kimoja cha kidini, alionekana kupwaya na kutofahamu vizuri sana mambo ya dini na mafundisho ya Kristo. Isitoshe, kuna Waislamu wengi walio nchini Marekani wengine wako katika nyadhifa kubwa na wengine wanakufa vitani kwa jina la Marekani. Nakubaliana na Papa Francis kwamba mtu anayejenga kuta baina ya watu anafaa kutiliwa shaka Ukristo wake.

6. Trump ni mwepesi sana wa kutoa matamko ambayo ukiyatafakari utaona hakufikiri sana. Kwa mfano alilalamika kwamba Wachina, Wajapani na Wameksiko ndiyo wanafanya biashara kubwa ya kuuzia Marekani. Kwamba yeye atabadilisha hilo. Wazo zuri, lakini kwa namna gani? Hasa ukizingatia yeye mwenyewe ana biashara zake huko kama za utengenezaji wa nguo ambazo zinaenda kuuzwa kwa bei rahisi huko Marekani. Kama si unafiki nini? Sasa JPM hana unafiki wa namna hii na wala hakurupuki bila kufikiri kama hivyo.

7. Trump ana tabia mbaya ya kuwatukana watu hata matusi ya nguoni iwapo hakufurahia walichosema au wakimpinga. Kwa mfano alipata kumwelezea mtangazaji mmoja wa kike, Megyn nafikiri, kwamba si mzuri na kwamba alikuwa akisumbuliwa na hedhi ndiyo maana alimuuliza Trump maswali magumu. Alipata kumwelezea Hillary Clinton kwamba “she got schlonged”, tusi la nguoni la kingono. Schlong ni neno la Kiyidish lenye maana ya uume. Kiongozi wa nchi lazima uwe na lugha ya staha. Ni aibu na mtu ambaye ni wazi hafai kuongoza nchi. Je, niambie kama Magufuli ni mtu wa namna hii.

8. Kwa muda mrefu sana, Trump amekuwa akimpinga Obama kwa madai kwamba hakuzaliwa Marekani. Nilikuwa Marekani siku ambapo Obama na ikulu ya Marekani ilipotoa cheti cha kuzaliwa cha Obama hadharani. Huo ulikuwa ushahidi wa kutosha kwamba Obama alizaliwa Hawai’i, na si nchini Kenya alivyodai Trump na “birthers”. Trump alipoambiwa aangalie cheti kujiridhisha kwamba Obama ni mzaliwa wa Marekani, alikataa kukiangalia cheti na kusema hajali nini kinasemwa. Ndiyo kusema hana sababu ya msingi ila ubaguzi tu. Nidhihirishie kwamba Magufuli ni mtu wa namna hii.

9. Imedhihirika mara nyingi kwamba Trump pamoja na tough talk yake hajui mambo mengi na watu ambao wanahusika katika migogoro duniani. Utatuzi wake yeye ni kwamba atawalipua tu watu. Anadai mambo yote atajifunza huko kazini. Hiyo ni hatari ya kurudia tena mambo ya enzi za GW Bush za kuzua tu vita mahali ili kujipatia raslimali zao bila kujali watawaua watu wangapi. Na pia inadhihirisha kwamba ni mtu ambaye hajajifunza kutokana na makosa ya huko nyuma. Matokeo ya sera za uvamizi na vita si usalama duniani bali ugaidi zaidi na kukosekana kwa usalama.

Nawasihi Watanzania wenzangu kuwa makini na kuyajua mambo vizuri. Tusipende kurukiarukia habari za vijiweni. Kutokuwa makini kunapelekea taifa letu kuwa namba moja katika ushirikina. Hii ni kwa sababu hatuko critical. Habari zinazoshabikiwa sana kwamba Trump kasema hivi au vile kuhusu Afrika TRUMP HAKUSEMA. Ni magazeti ya porojo ndiyo yaliyosema mambo hayo. MNAMSHABIKIA HUYO MTU BURE, BILA KUJUA ANACHOPIGANIA WALA ANACHOSEMA. MITANDAO IPO SIKU HIZI, TAFUTENI HABARI ZA KWELI.

Tena, tusipende kumshabikia kwa sababu tu inadaiwa kasema kitu fulani au tu kapatia jambo fulani. Wamarekani wengi bado wanajutia kumchagua G.W. Bush kwa sababu tu alikuwa anapinga utoaji wa mimba na ushoga. Lakini je, aliipeleka wapi nchi? Matokea mpaka alipokuja Jaluo ndiyo ikabidi arekebishe mambo. Jambo moja au tamko moja siyo ushahidi wa uthabiti au ubora wa mtu. Hata kama Trump angekuwa amesema kwamba viongozi wa Afrika wanastahili kushughulikiwa, si kigezo cha kufaa kwa Trump. Naona watu wanajitoa ufahamu kabisa katika ushabiki huu na kudai kumwombea au kudai ni chaguo la Mungu. Ni mtu ambaye ana majivuno, ana dharau za kupindukia, mbaguzi, tapeli lililokuhu, na wanaomshabikia na kumpandisha chati ni mambumbumbu wasio na elimu. Mnakuwa kambi moja na watu wanaowasema nyie sio watu, nanyi mnashabikia tu!!!
 
Shida yako ni nini, Magufuli ni nani hapa? Hauna akili mzee, au ndo matatizo ya uzee..... Sisi tumpinge, tumponde au tumtukane Donald hatupigi kura zake, hatuongezi au kupunguza kitu kwake...... Back to your sense mzee
 
acha kulialia asee, shen hajatajwa katika orodha watakaonigwa na trump
Exactly my point. Trump hajamtaja mtu yeyote hapa Afrika ila Wabongo wanajilengeshalengesha kwake. Mambo wanayosema aliyasema hakuyasema.
 
Shida yako ni nini, Magufuli ni nani hapa? Hauna akili mzee, au ndo matatizo ya uzee..... Sisi tumpinge, tumponde au tumtukane Donald hatupigi kura zake, hatuongezi au kupunguza kitu kwake...... Back to your sense mzee
That is exactly my point. Trump hatuhusu kabisa na watu wanamshabikia kama vile atakuta kutuondelea madikteta wetu huku. Hana interest na sisi, na wala hatuhusiki katika kumpigia kura.
 
Sasa Magufuli leo amekuwa mtakatifu au Mungu?Muulize magufuli ile meli ya mv Dar es Salaam aliyoinunua kwa bei ya kifisadi iko wapi?
 
Sasa Magufuli leo amekuwa mtakatifu au Mungu?Muulize magufuli ile meli ya mv Dar es Salaam aliyoinunua kwa bei ya kifisadi iko wapi?
Hoja ilikuwa Trump hafanani kabisa na Magufuli. Hata pahali pamoja sijawahi kutamka kwamba Magufuli ni mtakatifu. Hilo la utakatifu unalitoa wewe. If you are not like Trump it does not mean you are a saint. Don't bring your ridiculously distorted illogical thinking to the discussion. If you don't have an argument, staying quiet would be more reasonable and desirable.
 
Trump songa mbele baba mti wenye matunda ndo hupondwa mawe, jiulize mleta mada na story yako ndeeeeefu je watanzania wanapiga kura?
Hata tuseme hatumtaki Trump au tunamtaka inatusaidia nini sisi watanzania?
Waachie wamarekani waamue Nani wanaemtaka aongoze Taifa Lao.
Tuache vihelehele ya kwetu yametushinda
 
naona leo kila ukisikia jina la Trump upo, sasa kama huyo Trump hawahusu hao unaosema wanamshabikia, sasa wewe anakuhusu nini mpaka kuandika gazeti lote hili kuhusu yeye? usichopenda kukijua ni kuwa Anaonekana ameteka hisia za waMarekani
 
Back
Top Bottom