Trump anahofia kuungana Saudi Arabia, Iran, China na Russia

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,568
Trump atiwa hofu na wasiwasi na muungano wa Iran, Saudia, China na Russia

Trump atiwa hofu na wasiwasi na muungano wa Iran, Saudia, China na Russia
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameeleza hofu na wasi wasi alionao juu ya muungano unaoweza kuanzishwa kati ya Iran, Saudi Arabia, China na Russia.

Kwa mujibu wa IRNA, Trump, ameelezea hofu na wasi wasi alionao kuhusu muungano unaoweza kuasisiwa kati ya Iran, Saudi Arabia, China na Russia na kwa mara nyingine amekosoa sera za utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani na kudai kwamba kama angekuwa rais isingewezekana kuaanzishwa muungano kama huo.
Hii ni katika hali ambayo, baada ya mazungumzo yao waliyofanya Jumanne iliyopita mjini Moscow, marais Vladimir Putin wa Russia na Xi Jinping wa China walitangaza katika taarifa ya pamoja kwamba Moscow na Beijing zinaunga mkono kurejeshwa uhusiano kati ya Saudi Arabia na Iran.
Wakati wa mazungumzo kati ya Iran na Saudi Arabia yaliyofanyika mjini Beijing, nchi hizo mbili zilikubaliana Ijumaa Machi 10, kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia baada ya miaka saba.

Wawakilishi wa Iran na Saudi Arabia walipokutana Beijing kwa upatanishi wa China
Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na nchi mbili, mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Saudi Arabia watakutana ndani ya muda usiozidi miezi miwili, ili kuandaa mazingira ya utekelezaji wa mchakato wa kubadilishana mabalozi na kufungua tena balozi zao, pamoja na kukamilisha taratibu zingine za kuanzisha upya uhusiano kati ya nchi mbili.

Tangazo la makubaliano ya kurejeshwa uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia kwa upatanishi wa China, limeakisiwa sana kuanzia kwa kuungwa mkono na kukaribishwa na nchi za ukanda huu, mpaka kwa matamshi ya hofu na wasiwasi ya viongozi wa utawala wa Kizayuni, na tamko la serikali ya Marekani la kueleza matumaini iliyonayo juu ya taathira chanya za makubaliano hayo katika kupunguza mivutano katika eneo la Asia Magharibi na kuhitimishwa vita nchini Yemen.../
4c3jaa3dbfbe8129asz_800C450.jpg
 
Kuna nchi nyingine kweli zinamuwakikisha shetani.
Hivi kweli mapatano baina ya nchi mbili ndio inakua maumivu kwa nchi nyingine?
Au mgogoro wa nchi mbili jirani ndio furaha ya nchi nyingine?
Aisee.!!
Utasikia Kila siku Marekani inaisema Urusi ijifunze kuishi vizuri na majirani zake,
Mara Urusi isizichagulie marafiki nchi jirani zake.
Kumbe yeye hapendi majirani wapatane,na pia hupenda kuchagulia majirani marafiki.yaani Saudi Arabia isipatane na irani.au Urusi isipatane na jirani zake.
 
IRNA hao si walisema watamuua sasa walikuwa naye wapi hadi wakapiga naye stori?? Yaani wewe naye ni makyembe tu ovyo kabisa bwashee
 
Muungano huu huenda utasaidia kumaliza vita Yemen ambavyo vimesababisha Saudia na Iran kupigana ndani ya Yemen kwa maslahi ya US na nchi za magharibi.
Watu wa Yemen wanapitia katika dhiki na taabu kwa sababu ya maslahi ya US na vibaraka wake.
 
Back
Top Bottom