ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,476
- 9,654
Siku ya jumanne(Leo) utawala wa bwana Trump umetangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Iran, kuhusiana na mpango wake wa silaha za nyuklia, mpango wake wa makombora na pia kuunga mkono ugaidi.
Hatua hiyo imekuja baada ya utawala wa Trump kuithibitishia Congress kwamba Iran imekua ikikiuka makubaliano ya mkataba wa nyuklia.
Taarifa hiyo pia ilikosoa hatua ya Iran kuunga mkono serikali ya Syria na makundi kama Hezbollah na Hamas.
Marekani ina wasiwasi kuhusu shughuli za Iran mashariki ya kati, zinazovuruga utulivu eneo hilo.
Pia iliilaumu Iran kwa kuendeleza mzozo ulio nchini Yemen kwa kuunga mkono waasi wa Houthi. Pia mpango wake wa makombora nao umekosolewa vikali.
Iran bado haijatamka lolote kufuatia hatua hizo za hivi punde.