Trump aionya tena Korea Kaskazini

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Posts
392
Reaction score
954
Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametoa onyo dhidi ya Korea Kaskazini kupitia mtandao wa twitter, akisema kuwa Pyongyang inatafuta matatizo.

Pia aliitaka China ambayo ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kujaribu kukabiliana na jirani wake huyo.

Bwana Trump alipendekeza kuwa China itapata makubaliano bora ya kibiashara ikiwa itafanya hivyo, lakini akaongeza kuwa Marekani haitaogopa kutatua tatizo la Korea Kaskazini bila ya Uchina.

Bwana Trump alitoa matamshi kama hayo wiki moja iliyopita lakini tangu wakati huo msukosuko umekuwa mkubwa.

Marekani imetuma meli za kivita kuenda kwa maji ya rasi ya Korea hatua ambayo imeighadhabisha Korea Kaskazini.
 
yule dogo sio wakuonya kama anaubavu aende akamtandike kama hana aufyate kimyakimya we kila siku unaonya tu dogo anawaimiza kichwa sana ingia kichwa kichwa uone mchina mwenyewe anajua awezi kukubali auziwe kesikirahisi hivyo zigo lako hilo komaa nalo tu mwenyewe
 
marekani anatumia inchi za wengine kuweka kambi za kijeshi alafu kwake pako safi sasahivi kaweka korea kusin kikinuka mabom yote yanadondoka korea kusin huku marekani poko safi
 
Q
JF ina raha yake kwamba akomae na zigo lake.
 
Wametukaririsha kuwa marekani ni taifa kubwa
Wametukaririsha kuwa marekani ni taifa kubwa
 
Natamani kinuke huyu trump sijui mawigi anatikisa kibritiii
 
Tatizo uzi huu wa Marekani na Korea tunashindwa kujua uhalisia kwa kuwa wachangiaji wengi wanatoa maoni kishabiki
 
Kila Rais wa marekani anataka akiingia tu
apigani vita
hakuna sababu wala nini
 
Nikifikiria tu zile movie zao za mapanga nawaza tu jinsi wamarekani watavyochinjwa kama kuku. Refer to "Jumong" "Emperor of the Sea" ha ha ha
 
Marekani ngoja ikutane na kipigo kikali na ndoo utakuwa mwisho Wa ubabe na itabaki kuwa kama ujerumani,itasambalatika na uchumi utayumba,na mchina atachukua nafasi yake,trump atakuwa amesha ambiwa na makamanda wake kwamba hapa tunaenda kutiwa aibu,ndio maana amebaki anatoa vitisho
 
Sasa kama anajua ana uwezo wa kuipiga mbona anaihusisha China si aingie moja kwa moja.

Ndo wale wale "Nishikeni nitamuuawa Nishikeni nitamuuawa"
[emoji12] [emoji12] [emoji12] umeona eh hapo anapiga bit aone uwezo tuu was dogo ili aongeze idadi ya wababe wake kwenye diary wamefika wangapi. Hana lolote pale ameukwaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…