Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,565
- 4,009
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuahirisha mkutano wake wa kwanza mkubwa wa kampeni baada ya kuandamwa na ukosoaji kwa kuandaa mkutano huo katika siku ya kukumbuka kukomeshwa kwa utumwa nchini Marekani
Trump amesema uamuzi wa kusogeza mbele mkutano huo umefikiwa baada ya mazungumzo na wafuasi wake kutoka jamii ya wamarekani weusi waliopendekeza kubadilishwa tarehe kwa lengo la kutoa heshima kwa Juni 19 inayotambulika kuwa siku ya maadhimisho ya kumalizika utumwa
Uamuzi wa Trump wa kuandaa mkutano hasa katika eneo la Tulsa mjini Oklahoma ulisababisha ghadhabu miongoni mwa wakosoaji wake waliosema ilikuwa ni tusi kwa kumbukumbu ya George Floyd , mmarekani mweusi aliyeuliwa wiki chache zilizopita kutokana na ukatili wa polisi
Makundi ya wamarekani weupe yaliwauwa mamia ya wamarekani weusi katika kitongoji cha Tulsa wakati wa vurugu za mwaka 1921 na mipango ya Trump kufanya mkutano kwenye eneo hilo imetafsiriwa kuwa tendo la kuenzi ukatili wa mabeberu wa kizungu.