True Story: You're advice might help

Mkuu pole sana!

Me nahisi kwanza ulikosea from the very beginning kumpa msela pesa ndefu hiyo bila kutaka ushauri kutoka kwa sista, pengine hilo tatizo alilokuelezea huko nyuma hata hakuwa nalo na kama kuna upendo wa dhati kati yako na sista wako basi ungemshirikisha mchezo ungeishia huko huko.

Sasa the way forward me nahisi lazima kwanza umuite sista, tena ikiwezekana sista alone bi mkubwa wala usihangaike nae, jua uhalisia wa kile shemeji yako anachokiomba kwa sasa na tena jua uhalisia huo kutoka kwa dada yako. Taka kujua repayment schedule yao (sista na shemeji yako), kama ukiona hawajajipanga njema hebu washauri vizuri na uangalie namna njema ya kutatua hiyo shida yao. Ikishindikana ndio umshirikishe bi mkubwa.

Kama mtakubaliana huyo jamaa apewe hizo pesa basi hakikisha maandishi yanakuwepo maana usishangae baadae ukaja ukaambiwa mirathi igaiwe.
 
Mie nikimpaga ndugu hela, nahesabu nimetoa sadaka. maana hazirudigi.

Pole mkuu, ila ili muende mbele hili lazima liishe lasivo ataendelea kukusumbua zaidi. Kaa chini na sister umueleze, ila umtahadharishe nia sio kumnyima hela ila nia ni kweka jambo sawa kwanza. kwa sababu ni sister yako atakuelewa na mtayajenga kama ndugu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom