True Story: You're advice might help

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,585
1,883
Hey guys wazima, Hopefully mko vizuri,

Well kuna kisa kimetokea ndani ya family yetu ni mambo ya kifamilia zaidi but kuna wakati it's better ukipata infinity thinking, ukipata ushauri kwa watu wenye kuona jambo flani tofauti kabisa na unavyofikiri au kutaka kulifanyia maamuzi.

Well katika uzazi wa mama yangu tumezaliwa wawili yani dada angu ameshaolewa na mimi tayari nimeoa infact kila mmoja ana mji wake ila mzee wetu alifariki muda kidogo.

Sasa mimi kama mtoto wa kiume ilikua ukiachilia shughuli zangu za mwajiri Nilikua na jukumu la kusimamia miradi yote ya familia sababu mama yangu umri umeenda sana so nikawa na total authority in everything so na play part kama baba mwenye nyumba mpaka Leo hii.


Miaka flani huyu jamaa ambae ni shemeji yangu(mume wa dada angu) alikua very good guy mwenye positive vibes na I felt proud kua nae.

Kama kukiwa na tatizo tulikua tunapeana ushauri na kutatua bila shida yoyote tuliishi hivyo tukitembeleana.

Sasa 2 yrs ago huyu shemeji yangu alinifata private akaniomba nimuazime some amount ni kubwa sana, binafsi nilistuka sana but kwa kua tumekua na taratibu za kusaidiana mara kwa mara (haikuwai kuwa money oriented) nilihoji kulikoni bwana shemeji mbona pesa nyingi hivi infact haikua easy but nilitoa nikijua simsaidii yeye tu bali na dada angu pia. Hiyo ikapitaa ikabaki kuwa kati yangu mimi na yeye nikiamini atazirudisha kwa heshima yangu kwake.

Sasa wakati tunaendelea na mvutano wa hapa na pale sikupenda kumfanya akose amani au ashindwe kutembelea kwangu sababu ni taratibu tuliojengea tangu day 1.

Nikiwa bado sijarudishiwa pesa yeyote nikasikia kua jamaa amekua promoted kazini alikua anatumia Gari ya kawaida tu Toyota Rav 4 L lakini sasa ameongeza gari nyingine mbili BMW X5 na discovery 3. Binafsi sikuongea lolote nilitoa ongera lakini moyoni sikua sawa sababu ever since nimpe such a big amount mpaka anunue hizo gari ni mwaka na miezi miwili.

Wakati maisha yanaendelea niliona siku niulize bwana shemeji vipi mbona kimya ule mzigo wetu?, akawa anadai mambo magumu lakini atajitahid baada ya mwezi anipatie atlist nusu amount nilikubali Japo Tayari nilikua nimekerwa Japo sikuonesha sikupenda kuvunja uhusiano wetu kama jamaa.

Muda umeshapita jamaa ananipiga chenga nyingi sana. Sasa miezi kama minne imepita tangu bomoabomoa ya Morogoro road ianzee na nyumba ya wazazi wake ikawa imebomolewa hiyo ndio ikawa kama pushing factor kibinadamu nikanyamaza sikusema lolote.

Sasa kilichonisukuma kuandika hapa ni hii mfarakano ambao upo ndani ya family yetu yani ni wazi huyu ndugu yangu anashikwa akili aje kuleta hoja za kipuuzi nyumbani naita za kipuuzi sababu mtu mwenye akili timamu hawezi leta hoja hizo.

Sasa ikawa sister amekuja kumfata Bi Mkubwa akamwambia kua wamekwama wanahitaji financial support waweze kulipa madeni wanadaiwa bank mambo yakienda vizuri watarudisha. Sasa bi mkubwa akaniita akawa anasema ndugu yako anahili na hili embu umskilize asije akaadhilika, mimi ikabidi nicheke nikasema tu sawa ngoja nione kwa kiasi gani naweza saidia ila wanipe muda kidogo, bi mkubwa akasisitiza sana akaenda mbali kua nisimdharau kwa kua she's a woman ila ni ndugu yangu pia.

Niliumizwa na maneno ya mama mzazi na sikutaka ajue kua tuna kitu kinaendelea kwa sisi watoto wakiume, sio hilo tu wakati mwengine napata feeling kua huyu dada angu hujui kinachoendelea but anatumika tu.

Sasa emb waungwana naombeni ushauri wenu tafadhali nifanyaje niweke mambo adharani? Nigome kusaidia au nimuite huyu jamaa shemeji yangu? Well nifanyaje maana naona kama dada angu anatumika wakati mwingine.

Please positive vibes thanks!
 
Pole mkuu.. Nadhani usiende kwa mother kwanza muite sister kando umwambie ukweli.. (She's ur blood) mpo wewe mama na yeye huyo shemej labda anampango kando. Then outcome ya mazungumzo yenu yatawapelekea kumshirikisha mom. (If possible)
 
"Money and blood don't mix.." Haka kamsemo ka marehemu BIG kananisaidia sana hasa katika hali kama yako bro!.

Haya nikushauri, kwanza pole na hongera kwa kuwa na utu na busara, ila kama ulivyoambiwa apo juu na Urban Monkey, 'huruma itakuponza' ni kweli wala si utani itakuponza bro.

Kuwa serious kidogo huyu shemeji ako ajue uko na authority kwanza kama kaka wa mke wake na muangalizi mkuu wa familia, asitake kukuchezea 'upuuzi' kuwa mkali na mwenye msimamo. Mwambie auze izo magari aache upuuzi wake.

Kama akikubali ziuza usisite ni PM madalali tupo bro!.
 
Ukweli unaweka Huru
usipindishe Weka mambo hadharani kipi hasa kinachokutia ugumu ili wafahamu....
Hali ikizidi kuwa Ngumu wauze Bmw
 
Pole mkuu uyo shemeji yako muda si mrefu atafanikiwa kuharibu family yenu na kutengeneza chuki kwa watoto wenu. Simama imara uchague moja uwe mpole upotezee na ufanye kama anavyoitaji kwa kumtumia dada yako au uwe mkali mkosane kwa muda lakini mbele ya safari mama yako na dada yako wakushukuru au wakuchukie mazima
 
Kaka kwanza nikupe hongera kwa uvumilivu coz siyo wote wenye moyo kama huo when it comes to money.
Wadau wametoa mawazo mengi lakini from my point of view naona cha kwanza jaribu kumwambia dada ako
coz kwa inavyoonekana hata yeye hajui,So mwambie kwanza then muangalie mnafanyaje,Coz ukichukua maamuzi ya kwenda kwa mazaah direct uwezi jua mazaah hata react vipi na Dada ako atareact vp,ko usipo angalie unaweza kuleta mtafaruko................LAKINI JUA KUWA WEWE NDO KICHWA CHA FAMILY KO FANYA MAAMUZI AMBAYO MWISHO YATAFANYA FAMILIA KUWA PAMOJA SIYO KUTENGANA........
 
Mara nyingi ndugu au rafiki yako anapokuomba umkopeshe pesa wazo la kwanza ni kutaka kumsaidia. Lakini watu wengine wamejifunza in the hard way undugu/urafiki na pesa haviji-mix vizuri. Kwa hiyo, kabla ya kukukabali kumkopesha ndugu/rafiki kuwa smart na zingatia yafuatayo:

  • Jadiliana nae njia nyingine ambazo unaweza kumsadia. Kuna wakati pesa inaonekana kama ndiyo solution ya tatizo wakati kuna njia kuna njia nyingine za kukabiliana na tatizo.
  • Kopesha kiasi cha pesa ambacho you can afford to lose. Kuna uwezekano hutaiona hiyo pesa tena. Akirudisha ni bonus, asiporudisha sawa vile vile kwa sababu ulikuwa umeshajiandaa kuipoteza hiyo pesa anyway. Ila uaminifu wako kwake utapungua. Kwa hiyo, kabla ya kumkopesha make sure you can take care of yourself.
  • Kuwa clear na matarajio yako. Ikiwezekana mkubaliane a payment schedule. Mkubaliane nini kitatokea kama akishindwa kulipa kama mlivyokubaliana.
  • Kama ni hela ndefu weka kila kitu kwenye maandishi. Kama hataki then ni sign kuwa hana mpango wa kukurudishia.
  • Tatua matatizo haraka bila kupoteza muda. You may feel like a nice person, lakini kama hutamshtua ndugu/jamaa mapema kuwa muda mliokubaliana kuwa atalipa umefika then you are just setting yourself up for trouble.
 
Mambo.haya kwakwel we use both heart and brain tuliyopewa na Mungu,itisha kikao cha kwako, mama.na.dada yako, ikiwezekana na shemeji yako..useme kila kitu ina a very calm way...lakini tegemea hiki anaweza kukuruka shemeji yako ..just be prepared tu kwa lolote friend. Hio itakuweka huru, na pia mama yako na dada yako watajua ukweli wasije kudhani unamnyima msaada shemej yako,
Ila.watu.wengine manunda kweli unapata hela unanunua magari bora hata angefanya investment ya maana
 
Ushauri wangu Weka kikao na dada na mama yako tu mkae ili wote wasikie kwa wakati mmoja. Na uwaambie kuanzia mwanzo alipokopa mpaka akapata hio promotion na kununua gari kuwa ulishamkopesha hio hela. Halafu mwambie sis wako asimwambie kitu mumewe ili uweke kikao chengine na sis,mama na huyo shemegi yako. Na ueleze tena kuhusu huo mkopo uliompatia, akikubali kuwa umemkopesha hao ndio watakuwa mashahidi wako.
Sababu ya kukupa ushauri huo inaonesha huyo shemegi yako hachukulii kama ulikuwa mkopo bali ni sehemu ya urithi wa mkewe. Na kama huamini haipo mbali utamuona sis wako anakuja kudai urithi wake karibuni haya yameshatokea kwetu nilipokuwa mdogo. Baadhi ya mashemegi hawafai sababu huwajui mioyoni mwao kama Chui ukidhania Kondoo.
 
itisha kikao na dada yako na mama na wazee wa karibu wa familia yenu eleza kila kitu ikibidi shemeji yako aseme atarudisha lini hela unazomdai.
 
Pole sana Mkuu!

Tafuta muda ukae wewe, dada na mama, then waeleze kuhusu mkopo mkubwa uliompatia shemela na namna anavyozingua. Ukiwaambia utaona reaction zao, mf sister anaweza kusema hajui chochote ama akasema anajua. Mama naye atatoa maoni yake. Then utaona wanasemaje.

Ukihisi sister anajua mkopo huo wote na bado anaendelea kutaka mkopo zaidi na zaidi basi usione haya kutoa hoja mfanye mgao wa mali. Kila mtu awe na chake.

Iwapo ukiamua kumkopesha tena hakikisha unaweka records na wanasaini. Haya mambo ya urithi ni mwiba kwa familia nyingi. Mnaweza kuwa mnapendana mkaja kutoana roho yarabiiiii kwa mali alizoziacha baba...

Usiache kuleta mrejesho...
 
Mara nyingi ndugu au rafiki yako anapokuomba umkopeshe pesa wazo la kwanza ni kutaka kumsaidia. Lakini watu wengine wamejifunza in the hard way undugu/urafiki na pesa haviji-mix vizuri. Kwa hiyo, kabla ya kukukabali kumkopesha ndugu/rafiki kuwa smart na zingatia yafuatayo:

  • Jadiliana nae njia nyingine ambazo unaweza kumsadia. Kuna wakati pesa inaonekana kama ndiyo solution ya tatizo wakati kuna njia kuna njia nyingine za kukabiliana na tatizo.
  • Kopesha kiasi cha pesa ambacho you can afford to lose. Kuna uwezekano hutaiona hiyo pesa tena. Akirudisha ni bonus, asiporudisha sawa vile vile kwa sababu ulikuwa umeshajiandaa kuipoteza hiyo pesa anyway. Ila uaminifu wako kwake utapungua. Kwa hiyo, kabla ya kumkopesha make sure you can take care of yourself.
  • Kuwa clear na matarajio yako. Ikiwezekana mkubaliane a payment schedule. Mkubaliane nini kitatokea kama akishindwa kulipa kama mlivyokubaliana.
  • Kama ni hela ndefu weka kila kitu kwenye maandishi. Kama hataki then ni sign kuwa hana mpango wa kukurudishia.
  • Tatua matatizo haraka bila kupoteza muda. You may feel like a nice person, lakini kama hutamshtua ndugu/jamaa mapema kuwa muda mliokubaliana kuwa atalipa umefika then you are just setting yourself up for trouble.
Exactly what I wanted to say, pesa ni pesa, na binadamu tutabaki kuwa binadamu (haijalishi ni ndugu yako au rafiki). Ikija kwenye suala la pesa tena pesa ndefu ni bora muandikishane na kila mmoja awe na mwanasheria wake au shahidi wa makabidhiano hayo, kama anayepewa pesa atakataa hilo jambo basi utapata shida kwenye kudai pesa zako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom