True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

hahaha, unafika mahali unaanza kuita Mungu, na shetan anachofanya ni kukuletea mawazo kuwa Mungu hakujali na pengine hayupo, kama yupo na anakujali si angeshakujibu...ukivumilia hivyohivyo inafika kipindi rohoni Mungu anakutia moyo na kuhisi yupo, unasonga mbele. wakati mwingine unaona kabisa Roho wa Mungu anakushuhudia moyoni kwamba wewe ni mtoto wa Mungu,....then shetan analeta mawazo, kama mtoto wa Mungu, kwanini matatizo haya yanakupata, ina maana Mungu hayaoni au hakujali....lakini hata kwa udhaifu, atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka. wale wanaoishia njiani na kwenda kuhitaji msaada kwa mashetani, ni chukizo kwa Mungu wetu.
 
Amen Mungu wetu ni mwaminifu ukimwamini hawezi kukuacha uaibike..
Hongera sana.
 
Amina mkuu kweli Mungu ameondoa huzuni yako na kukupa furaha
 
Amen LadyRed Mungu huwa anajibu kwa wakati wake naamini wakati wako umekaribia. Mungu akupe hitaji lakobla moyo.
 
Mungu ni mwema sana......bora wewe ilikuwa 5yrs......imagine nilipitisha 7yrs,,,, but sikuwahi kugeuza moyo wangu kwa Yesu......wala kumkashifu mama watoto......niliamini kuwa anaweza......na yalitimia......Amen
 
Mungu wangu, wasaidie wengine ambao wanapitia katika jaribu hili. asante kunitoa kule, sifa na utukufu ni kwako.
 
Aione bashite wa kolomije
HAHAHA, Bashite,..hahaha. nikisema toka moyoni, nikifikiria kuwa Bashite anapitia njia kama hii, mengine yote nayasahau namwomba Mungu amsaidie ampe watoto. Mungu amkumbuke yule dada (mkewe) akampe watoto. halafu unajua Mungu ni Mungu wa huruma na rehema sana, hahukumu kama sisi wanadamu tunavyohukumu, hafikirii kama sisi tunavyofikiria, hapendi kama sisi tunavyopenda. unaweza kuona Bashite anachukiwa na watu lakini Mungu kwa hili akamponya akapata watoto tena mapasha wa kutosha. Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kama angelihesabu maovu, ninani angesimama mbele zake, sisi sote tu wadhaifu mno na ni kwasababu tu Mungu ametusitiri, kila mtu akianika maisha yake yalivyo, kuna sehemu moja au mbili lazima ulishawahi kuteleza na kufanya jambo la aibu ambalo kama likiwekwa wazi litakusumbua maisha yote. tumseme Bashite kwa mambo yote, lakini tusimseme kuhusu watoto, wala kumsema kuhusu mkewe. Mungu amsaidie.

however, ningependa kumshauri Bashite kitu kimoja, hiki nitakisema toka moyoni kabisa na kama akisikia naomba akifuate. MUNGU NI MUNGU MWENYE WIVU SANA, na huwa hapendi kushare utukufu wake. simhukumu lakini, kwa jinsi anavyotangatanga mara kwa mabohora wanamuombea, mara kwa mashehe wanamuombea, mara kwa wachungaji wa kila aina etc, kuna michanganyo fulani, hivi akipata chochote toka kwa Mungu, tutajua ni Mungu yupi aliyemsaidia sasa. huwezi kunaimbia mimi ninamwabufu Mungu sawa na yule wa mabohora, au yule wa mashehe (tuwe wakweli, ndio maana hatusali pamoja), kuna wengine wanaamini Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu wengine hawaamini, na ni kwa Jina la Yesu tunaomba na tunatakiwa kuomba, sasa ukienda sehemu hawasali kwa Jina la Yesu ambaye ndiye njia kweli na uzima, mtu haendi kwa baba bila kupitia kwake....tusemeje sasa? mara unaombewa kwa Jina la Yesu, mara kwa mabohora, mara kwa mashehe wanaosema Yesu sio Mungu etc. kwamfano ukibarikiwa sasaivi, tutajua baraka zimetoka wapi? kwa mabohora, kwa mashehe, au kwa Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo?...naongea hivi kwasababu Bashite namfahamu alikuwa mhubiri mzuri wa injili, anajua kila kitu. Utukufu wa Mungu utaugawa kwa nani? watu watamwona Mungu yupi aliyekusaidia? ni Mungu gani unamwabudu kwasasa?

Namshauri arudi haraka kwa Mungu, jua lolote unalolifanya kama lina effect yeyote katika mambo ya Kimungu, unapambana na Mungu. wewe mtu wa injili ukienda kuombewa kwa mashehe uliokuwa unawasema hawana Mungu una maana unaunga mkono wao kutotumia Jina la Yesu? au kwa mabohora etc. RUDI KWA MUNGU ULIYEMWACHA, yeye ni wa rehema, dhambi zetu zijapokuwa nyekundu zitakuwa nyeupe kama theluji. unaweza kushangaa matendo yako kama haya ndiyo yanachelewesha muujiza wako na hiyo inamtesa sana binti wa watu (mkeo). Mungu amsaidie yule mwanamke kwakweli.
 
Mungu ashukuriwe!

Hongera sana kwa kuyashinda majaribu. Mungu azidi kuwabariki.

Binafsi nimebarikiwa sana na ushuhuda huu!!! Na najiunngamanisha nao.
 
Je,, haikuandikwa tafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na mengine yote mtazidishiwa? Ulianza na wrong footing,,,, Mungu akarekebisha hatua zako ulipojitambua na akajionesha kwako kuwa ni mwenye uweza. Mungu akubariki sana
 
fanya yoote lakini omba Mungu msalaba wa kukosa watoto usikukute maishani mwako. ni mzigo mzito sana hasa kwa watu ambao kabla walikuwa hawajawahi kuzaa kabisa. either parties unaishi haujui kama utakuwa productive au la, kama ni mwanaume haujijui kama wewe ni mwanaume au la....ila, hakuna aliyemkimbilia Mungu akaaibika. watumainio yeye, wamwaminiye yeye, wamkimbiliao Bwana hawatatahayarika/hawataaibika. na Mungu huwa anaacha tu, uhangaike kwa akili zako wee (kama amekuona unategemea wanadamu na akili zako), siku ukifika mwisho ukasema hapa sina uwezo wowote ni Mungu tu amebaki kama last option, ndipo Mungu anatokea na kujitwalia utukufu. wakati mwingine inatokea kwasababu ni mapenzi ya Mungu, ila wakati mwingine ni kwasababu mtu amefuata njia mbaya akaenda sehemu ambako hakuna Mungu, sasa atakutanaje na Mungu wakati amefuata njia isiyoelekea kwa Mungu. Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…