True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

uliponea kanisa gani mkuu
 
uliponea kanisa gani mkuu
Niwe mkweli dadangu, kiujumla niseme makanisa ya walokole. Ninasali kanisa la TAG kwasasa niko mkoani, lakini wakati wa dhiki yangu nimezunguka makanisa mengi sana ya kilokole. nimesali sana kwa mwingira pale mwenge, nimesali sana kwa gwajima, nimesali sana kwa katunzi, nimesali sana kwa makanisa mengi tu, ila sijawahi kwenda kwa lusekelo. hapo dsm makanisa karibia yote hayo makubwa nimesali. semina nyingi zikitangazwa nilikuwa nahudhuria, wakati mwingine sina nauli natembea kwa mguu. kuzunguka sana kulinisaidia kujua kanisa halisi ni lipi na la uongo ni lipi. huku kote nilikozungua i recomend uende ukitaka. watasema mengiii lakini mimi ninachojua ni kwamba nilipona....wanadamu ni wanadamu wana mapungufu yao lakini mponyaji ni Mungu. uwezo wa kutembea kwa mguu toka ubungo hadi mwenge, toka ubungo hadi posta, toka ubungo hadi kimara, ubungo hadi tabata vilikuwa vitu vya kawaida na joto lote la dar hilo. kwasasa siko dsm. sio kwamba nilikuwa napenda kutembea, sikuwa na nauli ya kulipa route moja ya daladala and yet moto wa kumtafuta Mungu unawaka ndani yangu.
 
sifa na utukufu ni kwa mwenyenzi Mungu pekee barikiwa
 
Hongera sana mkuu ubarikiwe sana!
 
Hongera sana mkuu ubarikiwe sana!
kwakweli naomba mnisaidie kumshukuru Mungu. na ukikutana na mtu mwenye shida kama hizo, mwambieni kila jambo lina wakati wake na mwisho wake. amwamini tu Mungu. historia kama hiyo kama nilivyoiandika imetokea kwenye maisha yangu na kamwe sitasahau.siwezi kusema mimi ni malaika kabisa sijatenda dhambi, lakini ukweli uko palepale nitaendelea kumtukuza Mungu na kusimulia ukuu wake kwani alinihurumia nisiyestahili wakati wa dhiki yangu, akanifunika aibu yangu na kunijaza utajiri nilioutafuta kwa miaka 5...utajiri wa watoto ambao haununuliwi kwa pesa..ni kwa neema yake.
 
mkuu pesa zipo saidie unifadhili masomo yangu plz ni pm nikupe a\c number yesu atakulipa mkuu
 
Asiye na wake ana MUNGU
hakika, wengine wametaja magari, wengine wametaja farasi, lakini sisi tutalitaja Jina la Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, amesema tuombe lolote kwa Jina la Yesu tutapokea. Hapana jina lingine chini ya Mbingu tulilipewa sisi wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo ila Jina la Yesu Kristo. Naye ameliinua sana jina hili kwani kwa Jina la Yesu kila goti litapigwa la vitu vilivyoko juu mbinguni, vilivyoko duniani na vilivyoko chini ya nchi. na kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Liitie Jina lake tu nawe utamwona Mungu Haleliyah.
 
Dah historia yako imenisisimua sana,kwa mtu ambaye hajayapiyia haya hawezi kuamini ila mitihani IPO,Mimi na mkewangu tulipitia haya tena kwa ujauzito kutoka namshukuru mungu sasa tuna mtoto wakike na maisha yanaendelea ,mungu yupo na unaweza jamani tusiache kumuomba iwe kwa shida au raha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…