True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

.....21
Jamani mimi ni mkubwa kwako bwana, alisema yunge!
Mimi: labda kama unatafta njia ya kunikataa tu, maana naona hunipendi na hujaridhika mimi kuwa mchumba wako, najua siwezi kulazimisha mambo! Tulale tu wala sikufanyi chochote, miaka hii 19 sijawahi kufanya leo hii nikubake mtoto wa watu? Siwezi bwana, nilipama kina cha maji!
Yunge: umechukia?
Mimi: kwani nmefoka?
Yunge: haya tulale usiku mkubwa huu
Mimi: poa,
Nikazima radio nakujigubika ghubighubi! Tulipitiwa usingizi mpaka yunge aliponistua kwamba kumekucha na anataka ondoke! Basi saa 11 na dakika 37 ile nikamsindikiza mpaka karibia na nyumbani kwao, kabla sijaanza kurudi akasema, mhh! Nmeamini wewe ni mchumba wangu kweli! Naomba usirudi nyumbani kwenu leo, baki nitakurinda na mafisi na hao wachawi wachawi! Alisema,
Pia ukibaki ntaamini unanipenda kweli, usiku ntakuletea zawadi ambayo hutoisahau! Sawa nzehe? Aliuliza! Sawa ntaona!
So kuona baki bwana!
Dah ! Umezingua mwamba umemuacha mtoto yunge bila kumtia umeyeyusha
 
....22
Basi nirejea nyumbani ikiwa bado kigizagiza saa 12 ile na kulikuwa na ukungu siku hiyo!
Amesema atanipa zawadi nisipo ondoka? Pia ameshamwambia mama yake majaruba ma3 yaliyo baki wanipe mimi nipande na amekubaliwa? Nilijiona nakwenda kuuwa ndege wengi kwa jiwe moja,
Nilifija nyumbani pale nikamkuta babu anakoka moto pale nje (shikome) nilimsalimia babu kwa uchangamfu, nae akanijibu salamu ile kwa basha na utaniutani kama kawaida yake, aise babu alikua mjanja mjanja sana, yaani kama unaongea na kijana mwenzio! Nilianza kumzoea kutokana na vijimaneno vyake vya utani!
Babu: kinehe nyanda wanekela ung'wanike aje getumo wizelile? (imekuaje dogo umemwachia binti aondoke kama alivyokuja?)
Mimi: mhh! Binti yupi huyo babu?
Babu: hahaa! Usinifiche mdogo wangu, yaani kwa binti yule japo anakuzidi miaka 2, lakn ndo msichana pekee unaweza anzisha urafiki nae tofauti na mabinti wengine, alsemema bab
Kwanza nilishangaa, huyu mzee inamaana alituona wakti tunatoka Niliwaza!
Babu: hakuna ki2 kitafanyika hapa nisijue.
 
....23
Najua kila kitu mdogo wangu! Kwa maisha ya hapa kijijini inakua hatari sana yanapofanyika mambo ndani ya mji wako bila wewe kujua, hivyo usiwaze sana,
Alisema babu!
Haya chukua madumu mawili jikoni (pembe nne) umsaidie bibi yako kufata maji pale bombani, alishindwa kukinga maji ya mvua usiku, alsema babu,
Nilinyanyuka nikaelekea jikoni kuchukua madumu' nikamuaga babu, akasema chukua baiskeli wewe, utayabeba kichwani hayo yote?
Hapana babu naweza yapakata mkononi tu, kwani kisimani ni mbali sana? Niliuliza!
Ebu njoo hapa kwanza, aliamrisha babu, nikayatua chini madumu yale kisha nikamsogelea babu,
Ebu chuchumaa,
Alitema kimbegu flani hivi kisha akakisogeza karibia na moto kwa dakika nzima, alichukua na kuniamru nivue shati kisha ninyoshe mkono wa kushoto juu, nilitii maagizo,
Alikibana kimbegu kile kwenye mkono wangu wa kushoto kwandani chini kidogo ya kwapa! Nilishangaa kimeishilia chote mwilini pasi na kubaki!
Masalaale! Nilisisimkwa mwili wote mpaka nikahisi wadudu wanatembea mwilini!
Nenda sasa.
 
...24
Niliondoka kuelekea kisimani kuchota maji kukiwa kumeanza kupambazuka sasa na ukungu unaelekea kuisha! Nmetembea kama dakika 4 hivi, nikaona waschana wawili kwambele wanatoka kisimani wamebeba ndoo vichwani! Wanaelekea niliko mimi yaani uso kwa uso nakutana nao!
Ng'wangaluka yunge (habari ya asbuhi yunge) nilimsalimia yunge mdogo ambae alisimama ghafla na kunikata jicho, umelijuaje jina langu? Usinizoee sawa? Alinikoromea yunge mdogo huku akizichapa hatua na kuondoka, nilimtizama kwa nyuma, dah! Kweli nilikiri yale aloniambia yunge mkubwa, niyule binti alie nikamatia jogoo ndani mwao, ambae nilimkuta amepauka anaanua maharagwe, leo namwona asbuhi hii akiwa safi kabisa! Kweli alikua msichana mzuri sana ika aliniudhi kwa dharau alonionesha, nikawaza ntakuonesha pimbi wewe! Nilienda kuchota maji pale kisimani ambapo kulikuwa na kina mama na wasichana kadhaa waliokuwa wamepanga foreni kungoja zamu ya kukinga maji kwenye bomba lile, nikawasalimia kwa heshma na wakaniitikia freshi tu, mama mmoja aliniuliza!
 
Back
Top Bottom