TRL-Sikio la kufa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRL-Sikio la kufa??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, Dec 2, 2009.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimeshangazwa na habari za mgogoro wa kampuni ya reli (TRL) na wafanya kazi wake waliotishia kutoruhusu treni ya kwenda bara mpaka walipwe mishahara yao ya mwezi Novemba. Hivi serikali hili jambo wameshindwa kulitafutia ufumbuzi?? Kwa nini serikali haitoi maamuzi ya mara moja kumalizana na huyo muwekezaji??? au mkuu wa kaya na vijana wake wametia pamba kwenye masikio yao?
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  vitu vingine jamani ni matatizo maisha yalivyo magumu watu wana familia unaondoka asubuhi kwenda kazini na kurudi jioni huna kipato kingine mwisho wa siku hupewi mshahara wako inakuja kweli ...?
  boring news
   
 3. kilema

  kilema Member

  #3
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hii ndio serikali sikivu ya ccm
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  1st Lady, hilo suala lilifanya roho iniume sana as if hawa wenzetu hawako katika nchi yao yenye viongozi wenye akili timamu. Kuna mfanyakazi mmoja alikuwa anahojiwa na BBC anasema landlord wake anatishia kumtimua kama hatolipa kodi na ametoka nyumbani hajua familia yake watakula nini? Haya mambo kuna siku yatasababisha mtu kutandikwa makofi hadharani unajua inafika mahali uvumilivu unafikia kikomo...Inasikitisha sana..
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  Hayo yote tumeyataka wenyewe, viongozi wetu tuliowachagua kwa hiari yetu wenyewe ndio wameingia mkataba mbovu kati ya serikali na hao wahindi, viongozi hao hao ndio wasiotaka kuondoa hao wahindi, pamoja na kuonyesha kuwa wameshindwa. Pamoja na matatizo ya wenzetu sisi ndo wa kulaumiwa, tuwe makini kwenye kura tusidanganyike na ahadi za uongo.
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  inaumiza sana niliona kama serikali ilikuwa inafanya mazungumzo na wawakilishi wa wafanyakazi wameamua nini katika mkutano wao wa jana?????????????????????????????????
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Inaelekea huyu mkuu wetu wa kaaya hata mawaziri wake hawamheshimu. Juzi juzi alipotoka Cairo si tumeambiwa alikuwa na kikao na mawaziri wake na amewakemea na kuwaamuru wamalize kero za hii kampuni ya Reli? Inakuwaje tena mpaka sasa waziri husika hajatimiza agizo la Rais? Sasa kama waziri ni binamu yako kama hawezi kazi si unamwambia Shangazi yako kuwa nduguyo ulimpa ujiko lakini anakuangusha! Wakina mama wa kikwere wanaakili sana atakuelewa.
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Unajua mi ninachokiona hawa viongozi wetu ni kama wanatufanyia usanii. Nakumbuka last week, Permanent Secretary wa Wizara ya Miundo mbinu Omary Chambo alikuwa anahojiwa na TBC1 akadai kuwa wizara inataka kuchukua hatua ya kuwahoji hao wadosi wa TRL kwanini mkataba usivunjwe kwa kuwa eti wameshindwa kuonyesha na kuzingatia na kutimiza wajibu wao mpaka inafikia hatua wafanyakazi wanajifanyia mambo watakavyo kama vile hakuna uongozi wa kampuni.lakini nadhani ilikuwa ni janja yao tu kutaka kuwapoza wale ndugu zetu waone kuna kitu kinafanywa na serikali wakati ukweli ni kuwa serikali imenyuti kimya na mambo bado yanakwenda mrama.. I suspect kuna agenda ya siri serikali wanayo na hawa wahindi.. Si bure!!
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kitu cha kujiuliza ni kwamba wakati TRC ipo wafanyakazi walikuwa hawajawahi kukosa mishahara. Sasa Chenge na wenzake wakaamua kuuza TRC na kuzaa TRL, leo hiyo TRL haiwezi kulipa mishahara.....ni aibu.

  Je, hivi serikali ipo?? au haipo?? Kawambwa mbona unajiaibisha? Unashindwa nini kuvunja mkataba?? Uhandisi wako ni bure tu, kwa nini usiombe ushauri kwa magufuli?? au kwa nini usijiuzuru??

  Katika wizara ya miundo mbinu, Omary chambo ndo nyoka na ndo anakwa misha mambo, siyo mtendaji kabisa kazi yake ni kulea kitambi tu. Na kikwete sijui anasubiri nini kuvunja baraza la mawaziri??
   
 10. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ni kweli hawa wafanyakazi wanamadai ya msingi kabisa lakini kitendo chao cha kulitoa treni dar na kwenda kugoma katikati ya safari si cha kiungwana na kinafanana na kile cha madaktari kugoma kutoa huduma ya tiba kwa wagonjwa kwa mgogoro wao na mwajiri.
  leo wafanyakazi wameondoa treni dar wanafika katikati ya safari huko wanagoma ilhali huyu abiria wanayemsumbua huko[kusiko kwao]kalipa nauli yake
  shame on them.
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tena hiyo ndiyo vizuri ili wananchi wajifunze kutochagua chama cha mafisadi (ccm). Tena wangegomea katikati ya msitu wa tabora au pale saranda.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kweli tumefikia mahala hatuwezi kuwa na uwezo wa kuongoza Shirika hili la reli?What do we miss, capacity, human resources, capital or what? Hivi hawa wahindi wanalofanya la maana ni nini? Tusiache mbachao kwa msala upitao!
  Hili shirika ni muhimu na moja ya maeneo ya uchumi ambayo sisi kama nchi hatuwezi kuliacha likiendelea kulala ICU tena kwa kupenda tu.Hivi serikali haijui mbia ni nani mpaka inaliacha shirika liko hohe hae kiasi hiki?
  Kweli kama tuna machozi, tuyatunze maana kuna siku tutajililia wenyewe.Tutakapogundua hatuna mojmba wala shangazi wakutupa mkono bila kuamua kusimama wenyewe.Ingelikuwa ni mimi, hawa jamaa siku nyingi wangekuwa wanakula tambuu kwao India kama kweli wanatokea huko.
   
Loading...