Leo nimeona niwakumbushe wale wakongwe wenzangu wa enzi za miaka ya 1980 ambapo kulikuwa na Bendi iliyojulikana kama DAR INTERNATIONAL aka Super Bomboka ambayo iliongoza na Marijani Shaaban.
Hii bendi ndio bendi iliyoongoza kwa nyimbo zilizoenda shule (ujumbe mzito) ambapo hata zikipigwa leo utadhani ni mpya. Nyiimbo nyingne zilikuwa ni ivsa vya ukweli kabisa vilivyomkuta Marijani; nyimbo zilizokuwa visa vya kweli ni; Kaka Mashaka (Mwajuma) na Masudi. Huyo Mashaka, Marijani alimwimba baada ya kuwa amehamia Super matimila kwa Dr Remmy, huyo Mwajuma alikuwa mke wa mashaka na tulikaa naye maeneo ya Mburahati kwa Jongo. Dada alikuwa anampeleka puta Mashaka kikweli.
Wimbo wa Masudi amekuwa jambazai, pia ni kisa cha kweli maana huyo kijana Masudi alimtaimu Marijani wakati akipiga muziki kwenye ukumbi mmoja kule Luhanga (Kigogo) na kumnyang'anya saa. Marijani akaamua kumweka hewani.
Baadhi ya wapigaji wa Dar International wakati huo ni ;Marijani Rajab na Freshi Jumbe. Wadau,
Tukumbushane nyimbo zenye akili za Dar Interantional Super Bomboka.

Du!
Mkuu umenikumbusha majonzi. Nilisikitika sana huyu mwanamuziki alipokwenda mbele ya haki.
Nyimbo zake nyingi zilienda shule kama ulivyosema hapo juu.
Nazikumbuka:
1.Wosia
2.Zuena
3.Asia
4.Mwanameka
5.Mama maria (sina uhakika, kulikuwa na maneno "nani kaenda kwa mama maria, na kuzusha maneno ya uongo, ilikuwa saa tatu za usiku..., Hao, ndio wenye kukaanga mbuyu, kuwaachia wenye meno watafune....I'm not sure for this. Ni long time).

Nilishangaa sana nilipoingia kwenye paper ya National ya Kiswahili ya F4 mwaka 1991 na kuukuta wimbo wa Mwanameka! Ilie paper ilinigonga sana niliondoka na D.