TRENI ZA MWAKYEMBE:TRL big up,TAZARA mnatuangusha

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Kwa mujibu wa TBC Mwakyembe amefanya ziara ya ghafla TRL na TAZaRA inaonekana kwa TRL wako on schedule ili treni ianze kazi effective october ila TAZARA kwanza vijana hata posho hawawapi alafu as if hawakue
Ewa maagizo ya waziri wako bize na ukarabati wa behewa saba badala ya 14.
Mbaya zaidi kumbe ela ipo kaahidi atamtimua kazi mtu maana katajiwa milolongo ya jinsi pesa ilimopita kachoka.Kamtaja Shimwela kwa jina kuwa atamtimua kazi if he is not taking the matter seriously!
Isije ikawa ni namna ya kusubortage huu mradi usianze mapema
Jamani mjitume sioni haja ya kufanyiwa surprise visit ndo haya aliyoyasema Nchimbi kuwa sometimes not serious na directives tunazopewa kazini no wonder wawekezaji wanaprefer watu wa nje
 
Sijamsikia Mwakyembe akitaja reli ya Tanga
kwa watu wa Bagamoyo pale Kidomole kungefanyika kidomole stesheni kila siku angesaidia saana
 
Nazani ile inaitaji major rehabilitation bse imetelekezwa mda mrefu tofauti na izi za kushunt watu mjini ambazo ata kwenye bajeti ametenga fungu!
With time ataifufua am sure bse ni lazima tupunguze uwingi wa mizigo inayopita kwa barabara maana kitakwimu serikali hutumia billion 200 kukarabati reli while 300billion kukarabati barabara
 
mwakyembe ni moja ya mawaziri hodari sana.
Naamini atatatua tatizo la foleni dar, serekali ya awamu ya 4 itakua imeweka historia ktk hili.
 
Ndo maana kwenye katiba mpya mi nashauri kuwe na kipengele cha kuunda serikali ya mseto ili watu kama mwakyembe na magufuli wawe wanapeta tu hata kama chama chao kitashindwa uchaguzi
 
Kwa mujibu wa TBC Mwakyembe amefanya ziara ya ghafla TRL na TAZaRA inaonekana kwa TRL wako on schedule ili treni ianze kazi effective october ila TAZARA kwanza vijana hata posho hawawapi alafu as if hawakue
Ewa maagizo ya waziri wako bize na ukarabati wa behewa saba badala ya 14.
Mbaya zaidi kumbe ela ipo kaahidi atamtimua kazi mtu maana katajiwa milolongo ya jinsi pesa ilimopita kachoka.Kamtaja Shimwela kwa jina kuwa atamtimua kazi if he is not taking the matter seriously!
Isije ikawa ni namna ya kusubortage huu mradi usianze mapema
Jamani mjitume sioni haja ya kufanyiwa surprise visit ndo haya aliyoyasema Nchimbi kuwa sometimes not serious na directives tunazopewa kazini no wonder wawekezaji wanaprefer watu wa nje

Mkuu kuhusu utendaji kazi wa TAZARA wala mimi sishangai chochote, huko nyuma niliwahi kuandika kwa kina kuhusu mind set za wafanyakazi (Viongozi) wa Shirika hilo walio pewa dhamana ya kuliendesha! Wanafanya kazi kwa mazoea tu na actually akija mtu independent akawafanyia usahili atashangaa ni kigezo gani kilitumika kuwapa responsibilities ambazo hawana uwezo wa kuzimudu, siwasemi vibaya lakini nakuhakikishia wengi wao ni vilaza TU hawana ubunifu wowote! Wana thrive kwenye majungu tu na nepotism.

Kama Waziri Mzalendo Mwakyembe alifanya makosa ya kuwakabithi fedha za kufufuwa mabehewa bila ufuatiliaji wa karibu namuhakikishia Waziri kwamba fedha hizo zitakwenda na maji au watanunua vitu vya uongo na kweli, na wafanyakazi wanao karabati mabehewa hayo hawatalipwa overtime zao au watapewa hela pungufu, na si ajabu ukakuta fedha hizo zinakuwa-diverted kununuliwa vitu vingine kabisa au mafuta ya kuendeshea train badala ya kufanya kazi iliyo kusudiwa!!! - ni watu wa ajabu sana na hawaogopi mtu.

Mimi namshauri Waziri Mh.Mwakyembe ahunde kikosi kazi kutoka TRL (wafanyakazi wa TRL wako well organised na wana uzalendo wa hali ya juu - na huko mambo ya politics hayapo) ndio waende TAZARA wasaidiane na ma-artisian wenzao kufufua mabehewa, fedha zote za kukarabati mabehewa (ya abaria wa hapa Dar) ya TAZARA Waziri awakabidhi TRL pamoja na usimamizi wa project nzima.

Kwa nini Mzalendo Waziri Mwakyembe amesahau kisanga cha kukuta abiria wako stranded usiku wa manane pale Railway station lakini cha kushangaza hakukuta kiongozi yoyote pale wala maelezo ya kulidhisha mpaka Viongozi wanakurupushwa kutoka nyumbani kwao walio kuwa wamelala usingizi fofofo hawana habari kinacho endelea kazini kwao. Swali ni je, Ndugu Mwakyembe ulipo kwenda tena kuangalia maendeleo ya ukarabati wa mabehewa yanayo kusudiwa kusaidia kupunguza msongamano wa magari DAR, alikuta nini pale TAZARA; siwezi kushangaa kama majina ya Viongozi walio husika na sakata la mwanzo la kulaza abaria station ya TAZARA kama siyo majina hayo hayo yanayo tajwa kwenye uzembe huu wa kukarabati mabehewa!! Je mweshimiwa Dr.Mwakyembe unaweza kusema na hii ni bahati mbaya tena, wakati wahusika ni wale wale! Kuna nini hapa?

Kwa nini usi-maintain speed hiyo hiyo iliyokuwa imeanzishwa na Mh.Nundu bila ya kuogopa lawama, mkiendekeza mambo ya softly softly hakuna kitakacho badirika katika Shirika hilo, sisi atutasita kutoa maoni/ushauri wetu kama wazalendo. Nakukatakia heri katika uchapaji kazi WAKO.
 
mwakyembe ni moja ya mawaziri hodari sana.
Naamini atatatua tatizo la foleni dar, serekali ya awamu ya 4 itakua imeweka historia ktk hili.

Itaendeleza kuweka rekodi mpya na historia nzuri kibao ilizoweka mpaka sasa.
 
Kwa mujibu wa TBC Mwakyembe amefanya ziara ya ghafla TRL na TAZaRA inaonekana kwa TRL wako on schedule ili treni ianze kazi effective october ila TAZARA kwanza vijana hata posho hawawapi alafu as if hawakue
Ewa maagizo ya waziri wako bize na ukarabati wa behewa saba badala ya 14.

Kwa nini ma-artisian/technicians hawalipwi posho, kwa nini wako behind schedule! wanashindwa nini na TRL ambao wanatumia vifaa vya mwaka 1947?

Mbaya zaidi kumbe ela ipo kaahidi atamtimua kazi mtu maana katajiwa milolongo ya jinsi pesa ilimopita kachoka.Kamtaja Shimwela kwa jina kuwa atamtimua kazi if he is not taking the matter seriously!

Kwa nini wanataja milolongo ya upatikanaji wa fedha za ukarabati wa mabehewa wakati Wizara ilikwisha toa fedha hizi siku nyingi tu, tatizo ni nini? Hii ni project ya upande wa Tanzania ambayo ime-kuwa funded na G.O.T for a reason sasa nani anaweza kuingilia mwenendo wa project nzima inayohusu Tanzania, watu wanao pashwa kupewa project hii ni Tanzania Region - hivi kweli Wazambia wanaweza kuingilia suala hili? Tatizo letu Watanzania tunajuwa sana ku-manufacture visingizio vya kila design hatuko commited na hatma ya TAIFA letu - tuwe wakweli.

Isije ikawa ni namna ya kusubortage huu mradi usianze mapema.

Mkuu mimi sifikili kama wanafanya subortage ili mradi huu usianze mapema -tatizo hapa ni kutochukulia mambo seriously,kwa nini kwa mfano DMD ambaye ni Mtanzania mwenzetu na mtu mweledi sana anashindwaje kufatilia suala hili kwa karibu sana-na kama akiona kuna njama za kutaka kukwamisha jitihada za Serikali ya Tanzania kuhusu usafiri jijini, kama kuna mbinu za namna hiyo angepashwa ku-report Serikalini the soonest-the question is, alikuwa anafatililia suala hili kwa ukaribu KWELI?

Jamani mjitume sioni haja ya kufanyiwa surprise visit ndo haya aliyoyasema Nchimbi kuwa sometimes not serious na directives tunazopewa kazini no wonder wawekezaji wanaprefer watu wa nje

Well said Mkuu, tatizo kubwa la TAIFA letu ni kutofualitilia Seriously directive wanazo pewa na wahusika.
 
Back
Top Bottom