Uzembe ambao pia umechangiwa na mwekezaji mbovu. Baada ya kupata mwekezaji mpya tulitumaini ajali hizi za treni za abiria zingetoweka -- kama vile wakati wa ukoloni -- kulikuwa hakuna, au nadra mno, kwani treni za abiria kuleta ajali na kuua kwani zilikuwa zinaangaliwa sana kiusalama.
Hakuna sababu kwa nini hicho kisifanyike hivi sasa. Siku hizi mambo ni bora twende -- treni za abiria zinaendeshwa kama vile ni za mizigo.
Waziri husika -- Shukuru Kawambwa, inapasa ajiuzulu. Ni kweli, hakuwa anaendesha treni hizo au kuwepo katika eneo la ajali, lakini ni bora sasa afungue njia kwa serikali ya JK kuwajibika -- kumsaidia swahiba wake kuleta heshima ktk utawala wake. Najua kuna watu watamtetea kwa hili! Hawa wanaendeleza tu hali ya kutokuwepo utamaduni wa uwajibikaji.
Ubinafsishaji wa TRC kwa mwekezaji huyu umekuwa unalalamikiwa sana, kutokana na huduma duni katika uendeshaji wa shirika hilo na kwamba kuna dalili nyingi ubinafsishaji ulikuwa ni wa kifisadi.
Hivyo ajali hii itaongeza kuwasha moto. Na bila shaka kuna watu humu ktk JF hivi sasa wanaanza kuchonga kalamu zao kuzidi kutetea ufisadi huo na hata ajali yenyewe, kwamba ni ajali tu, haihusiani kabisa na mwekezaji mpya.