Treni la kura za maoni-2011 sisi-em

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Siku moja nilikuwa nasafiri na wagombea nafasi mbalimbali za kisiasa pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya chama katika treni la kura za maoni na matokeo toka matawi ya chama. Treni lilijaa pomoni. Seat hazikutosha abiria wengi walikuwa wamesimama kwa kukosa seat. Hata seat moja haikuwa na abiria ila iliwekwabegi kubwa juu yake. Abiria mmoja aliyekosa seat akauliza," Seat hii ina mtu?" Abiria aliyekaa seat ya karibu akajibu, " Ndiyo, ina mtu. mwenyewe ameshuka atarudi mara." Baada kidogo tu treni ikapiga honi na kuanza kuondoka. Kuona hivyo, abiria aliyehoji juu ya seat iliyokuwa na begi ghafla akainama, akaliinua lile begi na kulitupa nje ya dirisha. Abiria aliyekuwa seat ya jirani akauliza kwa kufoka, "Umefanya nini sasa?" Abiria mwenzie akajibu, " Hawezi kukosa vyote, akose treni na akose begi lake, haiwezekani?" Abiria aliyejirani akajibu tena,"Begi langu, lina hela za kuwanunua wajumbe wa KK wanipitishe kugombea ubunge kwa tiketi ya chama cha magamba nimeshindwa kura za maoni,hakika nimekosa vyote sasa!
 
Uwiii!! Pole pole kaka mbavu hizo tusije kubenjuka mbavu.Mwee huo ndo uzuri wa uongo yaani mtu unaongopea eti mwenye beg kashuka,
 
teh teh teh eeeeeeeeee uwiiiiiiiiiiii jamani mbavu zangu mie!!!
 
Back
Top Bottom