elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema kuanzia mwezi ujao wakazi wa Mkoa wa Arusha, wataanza kufurahia huduma ya usafi ri wa treni ya abiria. Kamwelwe alisema wakazi hao ambao walikuwa wakisikia usafiri huo kwa wenzao wa Mkoa wa Kilimanjaro, sasa wajiandae kupata usafiri huo mwezi ujao.
Alisema serikali iko katika hatua za mwisho kukamilisha usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam – Moshi hadi Arusha, kwa lengo la kutaka wakazi wa Kanda ya Kaskazini kuwa na usafiri wa uhakika katika vipindi vyote vya masika na kiangazi. Alisema serikali inataka kupanua wigo wa huduma ya usafiri kwa nia zote angani, barabarani na treni na baadaye majini, lengo ni kutaka mwananchi kujivunia kodi anayolipa kwa maendeleo ya nchi.
Kamwelwe alisema wanapanua huduma hiyo ili wananchi watumie usafiri huo ambao ni wa kuaminika, starehe na bei inayohimilika na wengi. Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), wanamalizia ukarabati na uwekaji wa alama kwenye kipande kidogo kilichobaki kufika Arusha, kwani tayari eneo kubwa kutoka Moshi hadi Arusha limekamilishwa.
“Mkuu wa Mkoa (wa Arusha – Mrisho Gambo) nakuhakikishia kwamba mwezi ujao (Januari 2020) nakuletea usafiri wa treni hadi hapa kwako kwa ajili ya watu wa hapa na wa mikoa ya jirani,” alisema Kamwelwe akitoka kwenye utoaji taarifa ya maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) utakafanyika mwakani jijini hapa. Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema sehemu ya reli inayoendelea kukarabatiwa kutoka Moshi kwenda Arusha ya urefu wa kilometa 86, kilometa 76 tayari zimekamilika na bado kilometa 10 pekee.
“Bajeti na kila kitu kipo. Lengo letu ni kwamba mwishoni mwa mwezi huu (Desemba) Kamwelwe alisema amejionea watu wengi walivyofurajia usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam, na sasa nguvu za TRC na serikali zinaelekezwa kununua mabehewa mapya ya abiria kuhakikisha usafiri unakuwa endelevu. Alisema nguvu pia itaongezwa kwa mikoa mingine kuendana na mahitaji, akiitaja mikoa kama Mwanza na Kigoma kuhitaji usafiri huo na mabehewa zaidi.
Treni ya abiria ya Dar es Salaam – Tanga – Moshi, imekuwa gumzo tangu mwezi huu uanze, huku watu wakionekana kufurahia usafiri huo unaoanza jioni na kwenda usiku kucha. Watu wamekuwa wakiburudika na vinywaji mbalimbali na wengine hutumia fursa hiyo kulala kwenye vyumba katika madaraja husika ya ju