TREND YA AFRICAN POLITICS. Historia Itajirudia Tanzania?



Hii post ulozungumzia hapa AJ.... Inakua supported na Process nzima ya Uchaguzi wa Igunga.... IGUNGA ni fundisho kwa CCM na as much as wameshinda Naamini kama kweli wanafikiria na Kuzingatia Upepo na Muelekeo wa Siasa in relation to Chama chao na Vingine especially CDM; Ni moja ya Tukio ambalo kwa kweli watajua kua inabidi wajipange! Vivo hivo kwa CDM.... Wameshindwa padogo... Naamini nao wamejifunza mengi na kikubwa yatakiwa wakubali waaache lawana na learn from the mistakes and Infact they do have a right ya Kujipongeza for ni asilimia kubwa mno wameweza kamata Ukizingatia the fact kile ni kijiwe cha miaka nenda rudi cha CCM.... Kweli wana haki ya kujipongeza they have done good.
 


Hey thea Sherriff..... as time goes on i believe we learn more about those around us hata kama ni Jamvini.... Yeah hua nafuatilia Siasa but not Kivile kama wadau wengine.... For I am more of an observer (thou i thot you knew this side of me for mara nyingi twagongana International Forum). Thank you for the acknowledgement; appreciated. Nakubaliana na huyo Mdau (The Boss) na nakubaliana pia na uloongezea kwamba No body should be above the law.... A True fact but sadly almost impossible to maintain... Sherrif Do take care too....
 

Tai Ngwilizi,

Nimevutiwa kwa jinsi ulivyochambua ... Forces .. zinazotengeneza mjumuisho wa mfumo wa kisiasa kwenye jamii yetu hasa nguvu ya vyama vya upinzani dhidi ya chama tawala ambacho kina lazimishwa kujitizama na pengine kikiwa kisikivu .. kinaweza kubadika kabisa na kujivua ma_GAMBA ..hence renewed and become a good son we knew before ..(Lol)

Utata , Kigugumizi or the dilemma amabayo iko mbele yetu ....Mfumo mwingine utakao kuja /Chama kitakacho replace CCM .... kuweza kutokurudia baada ya muda au wakati huo huo ...yale yale ya CCM ..kwani ushahidi upo... kwani almost vyama vingi vya kisiasa africa ... vile vilivyopigania UHURU kwa namna fulani baada ya muda viligueka ... na almost .. kufanya mambo yaleyale ..waliyokuwa wanafanya wakoloni kwa jamii zetu ya kiafrica.... CCM kama wana ubavu wasonge mbele ...wabishe kuwa sasa haifanyi jambo hili !!!

Utaona memebers wengi wanachangia ... namna ya kuondoa hiyo dilemma... nini kifanyike ..au ifumbiwe macho na kusonga mbele kikomandoo alafu yote yajipange mbele ya safari na mambo kama hayo...!!

Lakini swali la msingi hivi kweli CHADEMA ... inaona DILEMMA hii .. ninaitolea mfano CHADEMA maana kwa sasa ... sioni Chama au mfumo mwingine wa kisiasa nchini unao weza wenye muelekeo wa kureplace CCM when its half life or its life circle will be over.
 
Mkuu AJ hebu cheki posti namba 78 nimejaribu kuelezea kwanini Tanzania haifai kuwekwa kwenye kapu moja na hizo nchi za Afrika ambazo madadiliko hayakuzaa matunda.
 
Mkuu AJ hebu cheki posti namba 78 nimejaribu kuelezea kwanini Tanzania haifai kuwekwa kwenye kapu moja na hizo nchi za Afrika ambazo madadiliko hayakuzaa matunda.

*Mkuu hebu tuipitie kwa makini kabisa .... !


Mkuu

Niseme sikuwa nimeiptia hii posti kwa undani .... Kwa maoni yangu hapa nimeona mambo kwa upya kidogo.

Kwa kuwa sote tumekubalina kuwa MABADIKO kwa sasa ni muhimu, ILA tulikuwa tunataka kujihakikishia kwa historia isiyo njema kujirudia Tanznaia kama ilivyojirudia Nchimbalimbali za Afrika nimekusoma kuwa kuna sababu kadhaa kwanini Tanzania isilinganishwe na nchi kadhaa na sabau umezianisha kwa kifupi hapo kwenye alama nyekundu.

Kwa sababu hizo unaotutua KIGUGUMIZI sasa tusonge mbele na mabadiliko kwani sisi*

1. Hatusukumwi kwenda kwenye MABADILIKO kwa minyukano.
2. Hatusukumwi kufanya hivyo huku tukiwa na vyama vichanga (CHADEMA)
3. Tuna sense ya Utaifa ulio komaa wenye umoja na mshikamano .. usioelekea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe..

Kwa mtizamo wa ujumla sioni Tatizo hapa ... Na tarajia vyama vya upinzani wanaoma kama mimi na wewe kuwa ... Minyukano sio tija, kama chama ni kichanga mbele ya safari ..hakuna shaka historia itajirudia... na kuwa vyama vyote vyote vinaona umuhimu wa kupeleka mambo kwa namna isiyo ashiria .. vita vya wenywe kwa wenyewe... ili kuimarisha Utaifa na uzalendo ...vingine historia itajirudia...

Umesisitiza swala la KUDHUBUTU ... baada ya kujihakikishia na kuondoa KIGUGUMIZI cha historia kujirudia. Nafikiri pia kuwa Swala lako tikiliunganisha na lile na Mkandara kuwa .. tuwe na TRUST ... vinaweza kuleta tija ...nafikiri hili nitaliongelea kwa undani baadae... ili kuona kuwa kweli sasa Tanzania tusonge mbele kwa ujasiri kabisa na kufanya MABADILIKO kwani Historia haitajirudia...

Nina swali dogo sana...

Umeonyesha Nchi mbalimbali na MISUKUMO iliyowapelekea ... kukabili na kuleta MABADIKO ... na matokeo yao... Kama unaweza kwa namna fulani hebu nipe summary ya MISUKUMO unayoiona kwa Taifa letu....
 


Hio angle ulotolea Mkandara I understand (First para), but I think uko more centred on end results kuliko hata pre-factors ambazo humfanya Mtu mpaka akawa Kiongozi… Watanzania tuna nature ya kupenda AMANI thou imeonesha kua if we are pushed we a Capable of reaction even if it is just making some Effective constructive Sounds…. Historia yetu inaonesha the way hua ni wepesi saana kumuamini Mtu hasa akiwa na a Charismatic aspect to them…. Nasema kua hua tunakua na TRUST on the simple fact kua ile kitendo cha watu kuenda kupiga Kura it means kuna mtu wanatrust kwamba atafaa katika hio position; Problem tu huja kua mara nyingi saana hao watu ambao Trust is thrusted upon them hua ni Dissapointments kubwa saana in the long Run. Mfano mzuri saana ni huu wa IGUNGA…. Wale watu wa Igunga walikua wana I-trust Saana CCM Kama chama na mkombozi wao; But as much as CCM wameshinda ni dhahiri idadi inayo i-Trust CCM imeshuka at an alarming rate… CCM is in trouble political wise… sababu ya kuvunja that TRUST walipewa na almost all wana Igungaz katika last elections ambazo kipindi hicho Rostam alishinda kwa kishindo!

Kitu ambacho naweza ongeza ni kua Viongozi wetu wengi wa Kiafrica hutuangusha kwa kuvunja TRUST walopewa na Wananchi… yaani mpaka waweza sema kua kuna uchawi pale kwamba mtu akipata tu Uongozi basi akili habadilika na kua more selfish than ever! Hio yooote tokana na ukosefu wa Uzalendo…. Na huu Uzalendo sio tu kwa VIongozi bali hata kwa Wananchi…. INASIKITISHA…. Hakuna kitu kibaya kama Wanachi pamoja na viongozi wa nchi woote wasiwe Wazalendo… Inafanya kila mmoja awe for one’s self.

Mkandara katika the Fourth paragraph I beg to differ…. Majority Tanzanian’s kwa sasa wanaamini saana kua kikija chama kingine hivo Uongozi mwingine mambo yoote yatanyoka and everything will change for the better na ule msemo “Maisha bora kwa kila Mtanzania” utakua more applicable than ever… Haya mawazo hayafai kabisa for kama watu watukua na so much hope then they will be in for a disappointment… for the simple fact kua kuiweka hii inchi katika Mstari yahitaji mda, na Uendeshaji wan chi kama tunavoelewa is all about bureaucracies….. na mizengwe zengwe mingi ambayo mingine haina maana. Huo Uongozi mpya mpaka uweze reform sector mbali mbali yahitaji mda; For instance the popular issue of mikataba hii ambayo iko believed kua ni bogus – how long do you think it would take to sort out?? How long do you think it will take to reform the Education System/Health Sector/ and all its related aspects (hivo ni vichache tu – kuna mlolongo wa changes to be done kama kweli wanataka boresha hali ya Wananchi) inabidi Watanzania watambua kazi ya kuweka Tanzania katika mstari sio ya Viongozi pekee bali hata individual efforts zahitajika!

Paragraph ya pili toka mwisho….. aaaissseee!! Yaani still chewing…
 



Mkuu nimependa saana the other side of the shilling Umeprovide…. Rwanda…. Hawa watu wapo exceptional… Great people to have come through walopitia thou badly scathed but they have Survived… Tena waweza fikiria ni mbali but ni hapo tu early 1990s…. Wamebahatika wamepata A Great leader with the right brain in that head of his…. Impressive anavofanya in terms of investors… in terms of the Economy…. in terms of Education….

Hata hivo Mawaza matatu, wengi wape; I think it is good kukumbushana for inchi ambazo wameenda vizuri ni wachache saana (infact sijaona bado kama Rwanda kwa inchi masikini, thou nakubali kua Ghana wana fare vizuri). Na hata hivo Mkuu mie suala zima lilikua katika kutaka kujua how the Uongozi mpya waweza kutackle issue nzima ya Ufisadi. IMO Kama mafisadi wataachiwa hizo walizozichuma; then Ufisadi hautaisha for hao Viongozi wapya believe me you wata adapt; However kuisha kwa Ufisadi pia wategemea saana Matendo ya Uongozi mpya dhidi ya Sector mbali mbali ambazo zinagusa wanachi…. Yale matendo yao ya Mwanzoni na kufanikiwa kwake will say a lot….

Na kwa kuongezea…. Nafikiri Umeona how Ruanda wako serious katika mambo yao… Tumeona how in one way or another this thread is applicable and how wanakuabaliana na mimi kua adhabu kwa Mkosaji ni muhimu NO MATTER position ya muhusika…. Mfano mzuri saana; Hapo hapo Rwanda tunaona jinsi Yule mwanamama former First lady wa the Late Juvenal Hbyarimana anavoliliwa arudi nyumbani kujibu mashtaka dhidi ya kuchochea mauaji ya halaiki pale Ruanda; Ni mda umepita but still the Rwandan Government and its People wanaona kabisa huyo mwanamama anastahili kujibu mashtaka…. (Ndio yale yale niloongelea kua abuse of power haiishii kwa Raisi tu; hapo watoto na First ladies do play a major role once in a while)
 


Hapa kuna hoja imejitokeza ya TRUST .. KUAMINI ... Nafikri imekuja kwa uzito ambao sikuwa nautegemea. Tunaonyeshwa kuwa TRUST ndio siri tu ya UMOJA na hivyo HISTORIA KUTOJIRUDIA

Najaribu kuangalia kwa undani maana ya TRUST ... katika kujenga jamii iliyo bora na yenye maendeleo ya kweli. Najaribu kuangalia asili ya TRUST ... inakuwaje Mtu awe nayo, asiwe nayo, aipoteze, inakuwaje jamii nzima kama ilivyosemekana isiwe na thamani hiyo ... Na muhimu zaidi ... INAJENGWAJE ..na kuleta matunda yatakayoweza kutuondelea HISTORIA KUJIRUDIA!!

Kabala hata sijaijadili hiyo Trust ... Hivi kwenye historia ya Tanzania hakuna wakati imekuwepo ? Nini Kiliindoa ..?
 

My answer is possibly yes. Why? Because politicians are always politicians whether in the opposition or in the government. Most times when you look carefully at the African situation you see that the solution is mainly centered around leadership. These leaders see the problem and start a campaign to help solve the problem and then they are voted in. They get into office with high expectations from the people but in a very short while, they start the same circle of adding to the problems and most times even turning out to be worse than their immediate predecessors.

Who knows. We might see in Zambia very soon. The new President has already nominated more MPs than he is allowed to by Zambia's constitution. The current constitution allows the president to nominate at most 8 MPs at any given time, but Sata appointed 10. Gender activists are already complaining that women who form the bulk of the population have been sidelined in the new cabinet.

Pili wanadamu tuna kasumba moja. Once we get what we want, we don't take effort to maintain it. Tukishachagua chama kipya madarakani tunaishia hapo na kudhani kuwa they will do everything for us. Tunasahau kuwa they are still politicians just like the one we just overthrew them. We don't pressure them to do exactly what they promised. Matokeo yake wanajingalia wao wenyewe na ndigu zao.

We create problems, which in turn we use them to buy votes from voters. Our political game is based on manipulating the poor and illiterate. We create opportunities of dependency to the government and this way the poor always put the same leader, leadership style in power. We the people make our leaders, new or old, what they are. Our leaders in a large measure a reflection a reflection of the totality of our attitude to everything. Leadership is sustained by fellowship.
 

EMT

hapo niongezee tu kidogo as to why ni VIGUMU saaana kutegemea "maajabu" kwa kubadilisha 'mtawala' aliyepo na mwingine...si tu kwa Africa, lakini pia kwa dunia nzima

Kawaida falsafa nzima ya 'ukombozi' imejikita katika uwepo wa kundi 'gandamizi' na kundi 'gandamizwa' (the oppressor and the oppressed) hivyo daima tunategemea 'minyukano' kati ya hayo makundi mawili. Chukulia kwa mfano, 'utumwa' hujumuisha mtumwa mwenyewe na 'bwana' mwenye mtumwa....wakati wote watumwa huwa wana mapambano, mengine ya ndani ya nafsi na mengine wazi kabisa, ya kutaka kuwa huru,,,na mtazamo wa watumwa siku zote ni kwamba wanaonewa, wananyanyaswa, wananyimwa haki na 'bwana' wao na kikuweli wakipata nafasi, wakajiorganise, wanaweza hata kumuua....pindi ikitokea hivyo ina maana hapo kunahitajika 'uongozi' mpya unaotokana na wale watumwa waliompindua 'bwana' wao

Sasa kwa vile mitizamo ya wa tumwa ni kwamba 'bwana' anafaidi na wao wananyanyaswa, pindi wakipata tu uongozi wanageuka kuwa 'mabwana' wa watumwa wenzao, na kuanza kufanya yale yale yaliyokuwa yakifanywa na'bwana' wa zamani! na wengine waliokosa nafasi mapambano huwa yanaanza tena mara moja

Angalia kwa nchi za kiafrika kwa mfano...mapambano ya kudai uhuru, yaliongozwa na waliokuja kutwaa madaraka baadaye lakini wakidai kuwakilisha matakwa ya wengi. Kilichotokea kwa nchi nyingi, Tanzania ikiwepo, ni kurithi mfumo ule ule kandamizi wa ukoloni, kuanzia sheria hadi utawala, kiasi kwamba wananchi wengi wakawa bado hawajafaidi maana na maatunda hasa ya kuwa huru. na wengi mnafahamu kuwe kulikuwa na mapambano ya siri na ya wazi, dhidi ya utawala ulioingia madarakani, mfano:
  • Uwepo wa vyama vingi baada tu ya uhuru (kabla havijapigwa marufuku na katiba ilofuata)
  • Kuasi kwa Jeshi mwaka 1964
  • Uwepo wa mawaziri 'pinzani' kama kina Marehemu Kambona ambao baadaye 'walikimbia nchi'
  • Tukio la utekaji ndege la kina Maganga mwanzoni mwa 1980s
  • Vuguvugu la hali ya hewa kuchafuka zanzibar 1984 hadi Jumbe 'akatupwa kule'
  • Kuuwawa kwa Karume Sr mwaka 1972
  • Kufukuzwa kwa Seif CCM 1988
  • vuguvugu la vyama vingi na kukubaliwa kwake 1992 pamoja na michakato iliyoendelea hadi sasa
  • Kwamba tunahitaji katiba mpya sasa ni kuonyesha kutokubaliana na katiba iliyopo sasa ambayo baadhi ya watawala kama kina Kombani na Werema waliona haina tatizo hata kidogo
NImetoa hiyo mifano na najua ipo mingi zaidi kuonyesha kuwa kumbe baada ya mapambano ya kudai uhuru, walioapata bahati ya kuuukwaaa utawala waligeuka kuwa ndo 'wagandamizaji' wapya na wengi wakabaki 'wagandamizwaji'...na katika hili, hakuna namna tunaweza kukwepa mapambano haya.

Kwa mantiki hiyo basi, binafsi sitegemi kuwa na mabadiliko ya maana sana hata kama CCM ingeangushwa leo hii kutoka kwenye utawala. Wanaoingia watatoka miongoni mwetu, na siye tumekuwa tukitamani kuwa kama wao pia, kwa maana ya kuwa 'mabwana'...na raha ya kuwa 'bwana' ni lazima kuwe na 'watwana'...na kukishakuwa na makundi hayo mawili, misuguano na mapambano ni lazima...
 

vyama vyote vya siasa ni ubabaishaji tu.....................ccm na chadema wote ni ndege wanaoruka kwa bawa lilelile.......................ila la muhimu ni kuwa yule aliyeko madarakani mambo yanapokwenda mrama basi ni lazima awajibishwe....................afutwe kazi ingawaje tunajuafika atakayemrithi lao ni moja .......kudhulumu tu wapigakura...........................cha muhimu ni utamaduni wa kuwaondoa madarakani viongozi wabovu na vyama vyao...............i.e yawepo mazingira ya uwajibikaji..................katika khali ya kisiasa hapa nchini....................ccm imejenga ngome ya kisheria ya kukifanya chama hicho kiwe hakiwajibiki kwa yeyote na kwa lolote lile................................
 

AshaDii

Ni muda mrefu sana nimekimbia hili jukwaa na zaidi niliamua kuwa mtazamaji tu lakini hii makala yako imenikuna sana kwani ni suala muhimu la kulijadili na limekuja katika wakati mzuri sana na naamini linaweza kuamsha baadhi ya wenzetu ambao ushabiki wa kisiasa na chuki dhidi ya mfumo fisadi tulionao unbawafanya wafungue mioyo yaona kufunga akili zao.

hata hivyo nashindwa kuchagia lolote kutokana na lugha uliyotumia katika hili andiko lako. Tafadhali jitahidi kuihariri na kuandika kiswahili kinachoeleweka. Naamini wewe ni mtanzania na mswahili na ukiamua kutulia unaweza kabisa kuandika vizuri zaidi. Mchanganyiko wa lugha kama wako unaweza kutafsirika kama kudharau kiswahili na hivyo kutothamini utanzania wako ama kutaka kujionyesha kuwa wewe ni msomi mkubwa na hivyo kutoa picha ya kuwa hauna mshiko wa kutosha na siasa na jamii yako. Kuchanganya lugha ni kawaida lakini hii yako imevuka mipaka....


Asante kwa kichochea mjdala hiki na natumai wale vichwa maji hawatakuja na sumu zao, siasa majitaka na ukada pofu wao....
 


Kaizer,

You managed to make me contemplate*deeply,

Mkuu hiyo staili uliyoingia nayo naona imeweza kuonyesha haswa NATURE na FORCES ... zinazopelekea Historia za Tawala mbalimbali kujirudia. Kwamba issue inatokana haswa na ASLI YA MWANADAMU mwenyewe ... always kuna MISUGUANO inayoendelea Moyoni au Hadharani na kuwa ni jambo lililoko , litakuwepo na limekuwpo as long as mwanadamu yupo. Kwa mtizamo wangu, huu ni mtizamo muhimu sana ilikujua na kuweza ku manage mabadilko ya kijamii na kisiasa kwa Taifa letu. Kwa kuwa ni kweli kuwa hata iwe kundi gani kwenye jamii lazima kuna MISUGUANO inayoendelea MOYONI au HADHARANI ... Personaly inanisisimua sana kutambua hilo. Maana nafikiri hiyo Principle inaweza kutumika vizuri au vibaya kwenye ujenzi wa Uongozi uliopo au Utakao kuja kwa Taifa Lolote. Ni maamuzi tu hiyo kanuni itumike vipi.

Sasa itakuwaje kwani kama at any given time and space Uongozi wowote wa Kijamii lazima element za*oppressor*and oppressed .. Zitakuwepo karibu karibu tu , wala sio mbali ... na ndio msingi wa MABADILIKO.*

NA

Niogezee nafikiri ndio msingi wa swala ambao limeongelewa sana na MKANDARA na ASHADii .. Swala zima la TRUST .. yaani kuwa nayo au kutokuwa nayo. Kwamba kwa kuwa kuna Constant strugle internaly and externaly ... to have a constant total TRUST is an inevitable*phenomenal.

Basing on this analysis and coming back to the theme of the Thread ... Historia kujirudia kama mataifa mbalimbali ya Kiafrika!

Kwa mtizamo huu tusemeje , historia ya kile kilichotokea kwenye tawala zilizopita kitaacha kujirudia kweli?

Ndio maana angalia post yangu ya awali hapo juu nikatoa mitizamo mitatu ... Namna ya kumaliza hili tatizo.. AU?
 

Asha, which brings us to the point ya umuhimu wa LEADERSHIP. Nimeandika leadership in capital letters kwa sababu kazi ya kiongozi ni kubuni na kuonyesha njia. Tumekwisha kubaliana kwamba nchi yetu ina maadui wakuu watatu ujinga, umaskini na maradhi.

Sasa kwa kuwa we are in uncharted waters jukumu la viongozi wetu ni kubuni njia ya kupita ili tufike kwenye neema. Viongozi wetu wakituelekeza kwenye korongo tutaishia mabonde kwinama , wakituelekeza kwenye tambarare iliyojaa tende na asali tutaishia kwenye shibe.Na ndio maana viongozi wetu tunawapisha barabarani wapite, tunawapigia saluti, wakiingia ukumbini tunasimama etc

Sio kwa sababu wametuzidi umri, pesa au elimu la hasha ni kwa sababu tunaamini kuwa wao ndo wametushika mikono kutuelekeza kwenye nchi ya ahadi. Kuongoza sio mchezo, mi nawashangaaga wanaokimbilia kutaka uongozi bila kuzingatia uzito wa majukumu wanayoyaomba.
 

Kwenye red hapo,Bi Asha,ushawahi kusoma kitabu iitwacho 'Animal Farm'?
 

Bishanga,

Nafikiri hawa LEADERSHIP wetu watakusoma na kukuelewa .. Lol
Personaly hawa viongozi wa sasa , hata sijui wametokea wapi, sidhani hata wanawatambua hao maadui uliowataja.. maana silazima uwe na tofauti na Adui ili uweze kumtambua. Sasa kama THE ENEMY IS YOU ... how can you*differentiate*with THE YOU YOURSELF ...? Kwa kweli tuko kwenye hali ya vichekesho..

Ndio maana Tunahitaji MABADILIKO na sasa viongozi katika hayo mabadiliko siwataturudisha katika hali ile ile ya ya majonzi kabla ya MABADILIKO ..? *Mimi nafikiri labda tuachane na WAO (viongozi) ..tujiangalie SISI (tunaongozwa) ... Labda kunakitu hatujakielewa na kukitilia maanani nini? Maana kwakweli kama Hapa Tanzania Viongozi hawajiweke wenyewe ...kila mara tunawapigia kura ... na Kuwashangilia kwa vifijo kuwa SASA MAISHA BORA HayOOOOO ...Loh Kumbe?
 


EMT… I Like this post… As usual long and deep insight…. This post explains in one way or another as in why I always say I have NO Political party…. It is why I don't acknowledge CCM and why I don't trust CDM.. I always say the only distinction amid the two parties is that One is in control while the other fighting for that control… One thing I don't like about CDM (as much as it is the only at least reliable party) is their tendency of using any misfortune as an agenda of further campaigns… Hua wananikwaza hapo tu!

Hio paragraph ya tatu… yaani I feel for my fellow Tanzanians… They have so much hope… So much faith that the solutions to all the problems today can be solved just by having a new Political party with it's brand new leader and in a shor t time…. This attitude is going to cost the majority for they will be soo disappointed once they see the reality. This is a developing nation and they have to know that a lot of factors play part to its development let alone in every sector so that the reach every citizen…..
 
Reactions: EMT

Hayo maswali yako AJ... Naona limejibiwa vizuri saana hapa chini na Kaizer kwa Urefu kabisa..... Ingawa illo la pili kwa Tanzania yetu hii bado haijafanikiwa..



Kaizer Asante for this post na a deep insight umetoa.... I like it for the simple reason kua umeweza orodhesha baadhi ya Matukio muhimu ambayo yana paint vilivo uongozi toka Uhuru mpaka tulipo sasa hapa Nchini kwetu.... Maelezo yako hapa yananifanya nikumbuke Kitambu cha "Animal Farm" ambacho Bishanga kanitajia hapo juu… Yaani yaweza enda sambamba kabisa na Synopsis ya hio hadithi…. A great book with Great analogies and beautifully put hasa kuhusiana na Watawala Vs Watawaliwa…. Na the way hao watawaliwa huwa wakipata nafasi hio ya Utawala; and how inevitably hugeuka kama Watawala wa Kwanza kabisa ambao waliwatoa kwa nguvu zoote ama kua hata Worse!!

The events you have provided imekua ni vielelezo tosha kabisa ya kuweza gusia pale mimi, Mkandara na Azimio tulipozungumzia swala zima la TRUST…. Hivo basi tukiliangalia saana hili suala kwamba toka Uhuru kumekua na such events…. Sio ajabu kua tuna hali mbaya kama Uongozi umeadapt each and everything kwa the so called Oppressors wa kipindi hicho mpaka kutufanya tugombee Uhuru.

Hii yaweza kua na Mionekano miwili….


  • Pessimicism; Kua we are doomed kwamba what ever way we look at our future it is bleak for Viongozi woote wako hivo… na kama ulivo ongea wee na EMT, Kwamba Viongozi hubweteka and once in power they do not care ni nini wanafaya kwa Wananchi… hivo kuwafanya wajisahau or kutojali kilichowaweka pale.... ama tu kushindwa Uongozi.


  • Optimistic; Kwamba there is hope…. Kwamba the solution ni kwamba Ikitokea tu kwamba Chama kingine kikashinda kikija na sera zake mpya na Uongozi mpya then everything will be OK…. (Thou a day dream); Suala ambalo siamini kabisa... na suala ambalo fellow Tanzanians inabidi walitambue mapema.....

Hio in color if you don't mind… Naomba maelezo yake in brief for that is news to me….
 


Mkuu Omarilyas I am humbled Mkuu kwamba hii thread imekutoa pangoni hivo Nashukuru kwa hio acknowledgement umenipatia….. Nimesoma bandiko lako nikashangaa na kuseme huyu Member nae mbona kanionea jamani na nimeandika kwa Kiswahili; Nikaona nisome upya hilo bandiko langu la kwanza na Kutambua kua kweli bana nimechanganya Mno kwa mtu yeyote ambae anapenda asome Kiswahili asilia… Hivo Asante kwa kunikumbusha na siku nyingine nitafanya hivo (bandiko lolote/makala yoyote mhimu lazima iwe kwa Kiswahili sanifu). Ningependa saana niweze iandika upya but mda ni mfinyu; labda siku nyingine nitafanya hivo na nikutumie kwa njia ya PM….

Naomba utambue kua ninapoandika naandika hua wala hata siko makini wakati huo ni lugha gani naandika hivo inatokea tu…. Hivo napenda gusia kua Kwa yeyote ambae atafikiria kua nimeandika hivo ili nionekane Msomi namuonea huruma kua ni vigezo gani anatumia?? Maana Usomi haufafanuliwi ama kutambuliwa kwa Jinsi gani wazungumza lugha ngeni… Bali kwa Ufahamu wa vitu/mambo yakuzungukayo hasa kama ni muhimu na inahusu maisha ya kila siku… Na hio ndio inatusumbua Watanzania tulo wengi…. Wengi kwa sasa tumepata Shahada za Elimu ya juu… lakini katika hio idadi ni wachache ambao ni wasomi. Kwa Upande mwingine kwamba itaonekana nadharau Kiswahili (Siwezi mshangaa huyo mtu kufikiria hivo) kwani ukweli ni kwamba tulo wengi na hasa hiki kizazi cha utandawazi mara nyingine hudharau lugha zao na walikotoka…. Ila tambua kua I am proud of My roots…. Napenda kua ni Mtanzania na najivunia kwa hilo…. Kwa sababu hio defines me kama mwanadamu sababu najua hata nifanyeje sitaweza fuzu kua Mzungu…. Hivo basi naweza kua Modern kwa Mengi lakini siku ya mwisho ni Mtanzania……

Nimependa saana maelezo yako hapo nilipoweka rangi… inasikitisha kua Walo wengi hakuelewi kabisa unapojaribu kosoa vyama vya pande zoote. Yaani wengi wamekosa kabisa utambuzi wa kusema kua waweza kua hicho Chama na yapasa kikikosea ukikosoe….. Wengi wamekua ni washabiki hivo kufanya hio hali uloongelea itokee kwa saana.

Napenda niongeze kua tafadhali naomba mchango wako nione unasimamia wapi na unaamini vipi kuhusiana na Hii mada kwani naamini kweli kabisa Umeshanipata nini nilikua na wakilisha….. Natanguliza shukrani
 
Kwenye red hapo,Bi Asha,ushawahi kusoma kitabu iitwacho 'Animal Farm'?


Ndio Bishanga.... Napenda nijue from your perspective what hasa triggered mentioning the book apart from the obvious....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…