lukelo sakafu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2015
- 2,938
- 517
Kuna tuhuma dhidi ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuwa matrafiki kawaida hupangiwa hesabu na mabosi wao na wanatakiwa kuziwasilisha akimaliza kazi yake barabarani. Hayo yalisemwa jana na mbunge wa viti maalum Cochesta Mlawaza CHADEMA, kuwa serikali inatakiwa kuwafuatilia askari hawa kwani muda mwingine huwakamata madereva pasipokuwa na makosa ili mradi wapate hesabu waliyopangiwa na wakuu wao wa kazi. JE kwa stahili hii tutafika kweli? Karibuni wakuu
OPERESHENI ya kukamata madereva wa magari wanaofanya makosa ya barabarani, inayoendana na utozaji wa tozo za faini, imewaondoa Askari wa Usalama Barabarani, kwenye jukumu lao la msingi la kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara, na kuwapeleka kwenye ukusanyaji wa mapato unaotiliwa shaka kiasi cha kuibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa barabara nchini.
![]()
Uchunguzi uliofanywa na FikraPevu kwa siku kadhaa sasa umebaini kuwepo kwa mbinu za askari hao wa usalama barabarani kujificha vichakani ili tu kukamata magari yanayokiuka taratibu za matumizi ya barabara kwa lengo la kujipatia fedha, hali inayotia shaka kama fedha zote zinazokusanywa na askari hao zinaingia kwenye mfumo wa mapato ya Serikali au nyingine zinaishia mifukoni mwao.
CHANZO: FikraPevu